ONDOKA UANGAZE ISAYA 60:1.

Na Godfrey Miyonjo.

ISAYA 60:1.
BWANA YESU asifiwe.
Ewe uliyepata neema ya kumjua Mungu huu ni wakati wako wa kuangaza.
Huu ndiyo wakati wa kutangaza habari njema za YESU, habari ziletazo wokovu kwa kila mtu aaminiye.
Biblia inasema “kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu” MHUBIRI 3:1.
Mungu hakutuweka duniani kwa bahati mbaya, wala Mungu hakutuokoa ili tupoteze muda chini ya jua.
Lipo kusudi la Mungu lililomfanya atuokoe.
Alituokoa ili tuwe watumishi wake, tuwe mawakili wa siri zake hapa duniani.
Katika utumishi (uwakili) huu tulioitiwa hatupaswi kuogopa chochote wala lolote.
Hatupaswi kuwaogopa wachawi, wapunga pepo, wenye mamlaka (viongozi), wasomi, wasiosoma, wazee, vijana, N.K,
Ni kutangaza habari za Mungu wetu hadi watu wote wamjue Mungu wa kweli aliyeziumba mbingu na nchi.
Wamjue Mungu aliyefanya kila kinachoonekana navyote visivyoonekana chini ya jua.
Ni injili kwa kila kiumbe, ni kwenda kwa kila mtu ambaye BWANA ametutuma kwake, na kusema kila neno tuliloamuriwa na BWANA. YEREMIA 1:7.
Ninatambua kuwa kuna vizuizi vingi, wapo wapingaji wengi, lakini
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
ONDOKA UANGAZE, WALA USIOGOPE KWASABU YA HAO, KWAKUWA BWANA YU PAMOJA NAWE.

Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu).

Comments