SISI NI WASHINDI.


"Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?"
= > 1 YOHANA 5 : 4 - 5

Wana wa Mungu, kwa neno hili ni dhahiri kwamba mtu awaye yote, anayemwamini Yesu Kristo; ameitwa kuishi maisha ya ushindi katika ulimwengu huu. Na moja kati ya sifa za kuzingatia ili tuishi maisha ya ushindi ni matumizi ya ukiri wetu kila kuitwako leo.
"Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashibishwa mazao ya midomo yake. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake".
{MITHALI 18 : 20 - 21}

Kwa hiyo, tunapaswa kuwa makini, tusikiri mambo manyonge kama tunahitaji kuona ushindi katika maisha haya. Kwa maana,
"Atakaye kupenda maisha, na kuona siku njema,
Auzuie ulimi wake usinene mabaya,
Na midomo yake isiseme hila".
{1 PETRO 3:10}

Kama umelewa na umepeta imani, kwamba ni mapenzi ya Mungu uwe mshindi na umepaswa kuona siku njema; basi anza siku yako kwa kukiri mambo mema maishani mwako hata kama unaona giza, kama mfalme Daudi alivyokuwa akifanya;
"Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA
Katika nchi ya walio hai".
{ZABURI 27:13}

USIPO JIPANGA KUSHINDA; JIPANGE KUSHINDWA !!
MUNGU akubariki.
By Gideon Mwangaza.

Comments