SONGA MBELE KATIKA KRISTO YESU NA KAMWE USITAMANI KURUDI NYUMA

Na Alex Simion Makuli.

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu.
Karbu tena tujifunze Neno la Mungu kupta ufahamu na maarifa ya kutusaidia kusonga mbele katika safari hii ya wokovu
UTANGULIZI WA SOMO
"KUTOKA 2:23 HATA BAADA YA SIKU ZILE NYINGI MFALME WA MISRI AKAFA WANA WA ISRAEL WAKAUGUA KWA SABABU YA ULE UTUMWA, WAKALIA KILIO CHA KUMFKIA MUNGU KWA SABABU YA ULE UTUMWA"
"KUTOKA3:7 BWANA AKASEMA HAKIKA NIMEYAONA MATESO YA WATU WANGU WALIOKO MISRI , NAMI NMEKUSKIA KILIO CHAO KWA SABABU YA WASIMAMIZI WAO, MAANA NAYAJUA MAUMIVU YAO ,NAMI NIMESHUKA ILI NIWAOKOE NA MIKONO YA WAMISRI"
Katika maandiko haya tunona Biblia inazungumzia habri za wana waisraeli wakiwa utumwani Misri .Wana waisraeli waliishi kwa mateso makubwa sana katika nchi ya misri hatimaye waliamua kumlilia Mungu ili awaokoe katika mateso na utumwa waliokuwa wakitumikishwa na wamsri.
Ni kweli Mungu aliyaona mateso yao na alisikia kilio chao akamua kuwaokoa kwa kumtumia mtumishi wake Musa ili awapeleke katika nchi ya ahadi ya Kanani
KIINI CHA SOMO
"KUTOKA 14:10-14 HATA FARAO ALIPO KARBIA WANA WA ISRAELI WAKAINUA MACHO YAO, TAZAMA WAMISRI WANAKUJA NYUMAYAO WAKAOGOPA SANA, WANA WA ISRAELI WAKAMULILA BWANA WAKAMWAMBIA MUSA,JE KWA SABABU HAPAKUWA NA MAKABURI KATIKA MISRI HUKO ILI TUFIE JANGWANI? MBNA UMETUTENDA HAYA,KUTUTOA KATIKA NCHI YA MISRI?,NENO HILI SIO TULILOKWAMBIA HUKO MISRI TUKISEMA TUACHE TUWATUMIKIE WAMSRI?. NI AFADHALI KUWATUMIKIA WAMSRI KULIKO KFA JANGWANI".
Ndugu mpendwa hawa ni wana waisreli ambao mwanzoni walimulilia Mungu ili awatoe katika utumwa na mateso, lakini katika safari yao ya kuelekea nchi ya ahadi baada ya kufika katika Bahari ya Shamu wanakata tamaa.Wana waisraeli wakasahau yale yote ambayo Mungu aliwatendea, wakasahau zile ishara ambazo Mungu alizifanya katika nchi ya Misri , wakamlalamikia Musa. Pia wakatamni kurdi nyuma katika yale mateso ambayo walitumikishwa mwanzoni. Badala ya kusonga mbele lakini wao wakatamani kurudi nyuma hata ikiwezekana warudi tena katika kuwatumikia wamsri.
Katika maisha yako ya kiroho inawezekana umekutuna na Bahari kama wana waisraeli na ukashindwa kuendelea kusonga mbele na hata ukatamani kurudi nyuma.Mungu bado ni mwema na anakuwazia mawazo mema , yeye peke yake ambaye anaweza kuigawanya bahari n akukupa njia ya kusonga mbele
Usikubali kurudi nyuma kwa sababu ya majaribu , wala fedha isikufanye ukarudi nyuma, wala mafanikio yasikufanye ukarudi nyuma, wala utajiri usikufanye ukarudi nyuma. Nataka nikwambie kwamba moyo wa mtu ni wa muhimu sana mbele za Mungu kuliko mali, fedha, utajiri.
Bwana Yesu anatupenda sana na hataki tupotee, kamwe usikubali kumwacha Yesu kwa sababu Bahari/majaribu au kwa sababu ya utajiri/fedha/mali au kwa sababu ya umasikini, haya mambo yote ya kupita lakini ufalme wa mbinguni ni wa muhimu sana.
Ndugu yafaa nini ukaupata ulimwengu huu wa fahari yake yote, mwisho ukaangamia katika Jehanamu na kukosa uzima wa milele?
Mwisho , wewe ambaye hujamupokea YESU KRISTO kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako bado mulango wa Rehema upo wazi usisubili kesho okoka leo ili upte uzima wa milele.Kwa leo naishia hapo ila Mungu akitupa kibari tutajifunza zaidi. Mungu akubarki sana na akupe imani ya kusonga mbele na sio kurudi nyuma
Ni mimi ndugu yako katika KRISTO YESU Ndugu Alex Simion Makuli.

Comments