TUNZA UJASIRI ULIONAO MBELE ZA BWANA ILI USIPOTEZE THAWABU ILIYOKO NDANI YA UJASIRI WAKO.


Bwana Yesu asifiwe!
Namshukuru Mungu kwa kunipa ujumbe huu nami haja ya moyo wangu ni kuona na nashirikisha mwili wa Kristo (kanisa) kile Roho Mtakatifu ananifundisha.
Karibu tujifunze na Mungu Roho Mtakatifu akufunulie akili upate kuelewa kile anachotaka ukielewe katika somo hili.
Na Emmanuel Kamalamo.
Tusome pamoja Waebrania 10:35 anasema,,"Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu"
Ukisoma mstari huu ndani yake kuna kitu cha thamani na cha ajabu sana kinaitwa "UJASIRI" na huo ujasiri unaweza ukautunza au ukautupa lasivyo asingeseme,,"MSIUTUPE" maana yake unaweza kuwa nao na ukautupa.
Ndani ya "UJASIRI" kumebebwa kitu kinaitwa "THAWABU KUU" Ukisoma katika kiingeleza anasema hivi,,,,"Therefore do not throw away your confidence, which has a great reward."
Kiswahili anasema hivi,," Kwa hiyo, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatieni tuzo kubwa" Sasa ukilinganisha na maneno ya Waefeso 6:10 anasema "Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake" Utaona neno hili "HODARI" limetumika katika Waebrania 10:35 kama "UJASIRI" ambao ndani yake tunapewa "TUZO KUBWA" hapa baadaye.
NINI MAANA YA UJASIRI/UHODARI.
UJASIRI-Maana yake ni uwezo alionao mtu wa kujiamini mbele za Bwana juu ya maisha yake yasiyo hukumiwa na dhambi moyoni mwake.
Ukisoma 1 Yohana 3:21 anasema hivi,,"Wapenzi, miiyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu"
Sasa jiulize swali hili pamoja na mimi, Ni nini kina hukumu moyoni? Kama si kusema..."KUHUKUMIWA MOYONI"...kuna letwa na "DHAMBI" iliyo moyoni ambayo inapoteza UHODARI/UJASIRI wa mtu mbele za Bwana. Kama umepoteza "UJASIRI" ndani yako maana yake "UMETUPA UJASIRI" wako kwa kuruhusu dhambi iingie ikae maishani mwako, na madhara yake "THAWABU/TUZO KUU" unaipoteza ukiwa hapa hapa duniani.
Utauliza, "Kamalamo unamaanisha nini? Na maanisha hivi, Kama umepata "UJASIRI" wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, maana yake umefutiwa dhambi, na moyoni mwako umepewa "UZIMA WA MILELE" Sasa unaporuhusu dhambi unapoteza "UZIMA WA MILELE" uliyo ndani, na maandiko yanatwambia,,,"....MNA UZIMA WA MILELE NINYI MNAOLIAMINI JINA LA MWANA WA MUNGU" (1 Yohana 5:13)

SABABU ZA KUTUNZA UJASIRI ULIONAO NDANI YAKO.
Ni kukufikisha katika TUMAINI/TARAJA ulililoandaliwa kulipata hapo baadae.
Waesfeso 3:12 "Katika yeye tuna ujasiri na uwezo wa kukaribia tumaini kwa njia ya kumwamini"

Huwezi kulikaribia "TUMAINI" uliloliweka ndani ya Kristo kama huna "UJASIRI NA UWEZO" unaokupa wewe kutarajia unachokitarajia katika Kristo.
Hakikisha haupotezi "UJASIRI" wako usije ukashindwa kukaribia tumaini lako uliloliweka kwa Yesu. Maana ujasiri na uwezo ndivyo vinakutengezea madhingira ya kukaribia tumaini lako. Ujasiri na uwezo unavipata ukiwa ndani ya Yesu.
UJASIRI UNARUHUSU KUPEWA NEEMA YA KUKUSAIDIA.
Waebrania 4:16 "Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji"
Katika maneno hayo kuna..."KITI CHA NEEMA" na kuna....KUPEWA REHEMA..na pia kuna...KUPATA NEEMA. Kazi moja wapo ya kiti cha Neema ni sisi "TUPEWE REHEMA" kiingileza anasema,,, "GIVEN MERCY" Mercy inamaana ya "HURUMA"
Kwa manti hiyo kiti cha NEEMA kinatoa "HURUMA NA NEEMA" vinavyomsaidia mtu mwenye ujasiri ndani yake kutumia "NEEMA INAYOTOA MSAADA" wakati wowote mahali popote anapohitaji msaada wa kutoka kwenye "NEEMA" aliyonayo.

Maandiko yanasema hivi,,"Wapenzi, miiyo yetu isipotuhukumu tunaujasiri kwa Mungu. na lolote tuombalo, twalopokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake" (1 Yohana 3:21-22)
Ukiomba na hauna ujasiri ndani yako huwezi kupokea unachokiomba, kwa sababu "NEEMA" ya kukusaidia haipo, kwa nini haipo?....Kwa sababu huna uwezo wa kusimama mbele za Bwana. Kasome Biblia yako utaambiwa..."TWAJUA YA KUWA MUNGU HAWASIKII WENYE DHAMBI; BALI MTU AKIWA NI MCHA MUNGU, NA KUYAFANYA MAPENZI YAKE HUMSIKIA HUYO" (Yohana 9:31)
KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA, BAADA YA KUFA NI HUKUMU.(Waebrania 9:27)
MUNGU AKUBARIKI
ekamalamo@gmail.com

Comments