UKOMBOZI WA KUJITOA KWA DAMU YA YESU KATIKA MATESO YA SHETANI.(pasaka tatu za ukombozi)

Na Mtumishi Daniel Wa Deliverance Ministry.

1. Pasaka ya Musa
2. Pasaka ya Suleimani
3. Pasaka ya Yesu.

Kutoka 12 – 11
Tena mtamla hivi mtakuwa mmefungwa viuno nyenu mmevaa viatu venu miguuni na fimbo zenu mikononi mwenu nanyi mtamla kwa haraka ni Pasaka ya Bwana.
(Pasaka huleta hukumu juu ya wale ambao humpinga Mungu ndio maana utaona hata Farao alipewa hukumu ya Pasaka ni hukumu juu ya miungu)

Kutoka 12 – 26:27
Kisha itakuwa hapo watoto wenu watakapo wauliza Nnini maana yake utumishi kwenu? Ndipo mtawambia ni zabihu ya Pasaka ya Bwana kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri hapo alipo wapiga wamisiri akaziokoa nyumba zenu, hawa watu wakainama vichwa vyao na kusujudu. (Hivyo Pasaka ni kuchinja au kumwaga damu kwa ajili ya ukombozi hii ndio maana halisi ya Pasaka)

Kutoka 12 – 31
Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, ondokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli enendeni kamtumikiene Bwana kama mlivyosema. (kwenye Pasaka kuna kuachiliwa na kwenda kuwa Mtumishi hivyo Farao ambaye alikua munga wa Misri
alijua hilo ndio maana aliwambia tokeni katika watu wangu.)

Kutoka 12 – 32
Twaeni kondoo zenu na Ng’ombe zenu kama mlivyosema enendeni mkanibariki mimi pia.(kondoo humanisha nini humanisha utawala hivyo walipewa utawala na maandiko husema kuhusu baraka kwa mtu ambae yuko kinyume huwa laana hivyo kwa Farao ilikuwa laana kwake inapokuwa Pasaka unarudishiwa mali zako zote ambazo Shetani alizichukua)

Kutoka 12 - 43
Bwana akamwambia Musa na Haruni amri ya Pasaka ni hii mtu mgeni asimle, lakini mtumishi wa mtu awae yote alienunuliwa kwa fedha ukisha kumtahiri ndipo atamla Pasaka. Akae kwenye hali ya mgeni na mtumishi alieajilwa asimle Pasaka.(utaona ukitaka kuwa mtu wa Mungu inakubidi kukana uasili wako na kujiunga na Israeli kwa kutahiriwa hapo ndipo inakuwa kuingia katika agano la damu kwa hivyo hata wakati wa sasa ili kushiriki Pasaka yakupasa kuingia ukoo wa Daudi kwa hutahiriwa kwa kukubali kwa kukiri kwa kinywa chako kua Yesu ni mkombozi na mwokozi wako ndipo utaingia katika agano la msalaba la Yesu kufa msalabani)

UTAKASO
Kutoka 19 – 9
Bwana akamwambia Musa, tazama, mimi naja kwako katika wingu zito ili watu hawa wasikie nitakapo sema nawe, nao wapate kukuamini wewe nawe hata milele Musa akamwambia Bwana hayo maneno ya watu. Bwana akamwambia Musa, Enenda kwa watu hawa ukawatakase leo na kesho wakazifue nguo zao, wawe tayari kwa siku ya tatu Bwana atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote { ukishapoke Pasaka nawe huwa katika utakaso hapo huwa na uhusiano na Mungu)

2 Mambo ya nyakati 35: 1:3
Naye Yosia akamfanyia Bwana Pasaka huko Yerusalemu wakachinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, Akasimamisha makuhani katika malinzi yao, akawatia moyo kufanya utumishi wa nyumba ya Bwana akawaambia Walawi waliowafundisha Israeli wote waliotakasika kwa Bwana wekeni sanduku takatifu katika nyumba aliyoijenga Suleimani mwana wa Daudi mfalme wa Israeli hamtakuwa na mzigo mabegani sasa mtumikieni Bwana Mungu wenu na watu wake Israeli.
(Kushiriki moja kwa moja katika ufalme wa Mungu, utaona kwamba kabla ya hapo kuwa katika Israeli yote uwepo wa Bwana kuanzia pale Musa aliposhuka katika mlima wa Sinai aliwapa watu anaowaongoza kazi ya kubeba Agano la Mungu ambalo lilikuwa ndani ya sanduku hivyo ukombozi wa Taifa la Israeli ulikuwa ndani ya damu yao.Kazi hiyo ilikuwa juu ya Walawi mara walipochoka kubeba au kulinda sanduku kulikuwa na madhara katika taifa la Israeli lote)
Hadi siku ile ambayo waliweka sanduku la Agano katika nyumba aliyojenga Mfalme Suleimani ndipo kubebwa kwa Agano kwa mara ya kwanza katika mabega kulikoma.
Lakini kulikuja agano la pili ambalo ni Yesu kristo ambaye na yeye alibeba agano mapegani mwake kwa kubeba dhambi zetu hadi pale siku ya kufa kwake msalabani.Hivyo uzao wa Daudi ndio ulileta ukombozi kwa mara ya pili.
Pasaka ni kuchinja kwa kumwaga damu ndio maana unaona Yosia alifanya Pasaka katika hekalu.Nae Yesu alikuwa Pasaka pale goligota kwa kufa juu ya msalaba.

Isaya 52-1
Amka amka jivike nguvu zako ,Ee sayuni jivike mavazi yako mazuri ee Yerusalem mji mtakatifu kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi.
(Unajisi au kutokutahiriwa ni nini? Ni kutokukubali kuwa mzao wa Daudi kwa kuungana nae katika uzao wake)

Isaya 53 – 4 :7
Hakika amechukua masikitiko yetu amejitwika huzuni zetu.Lakini tulimdhania ya kuwa amepingwa amepingwa na Mungu, na kuteswa. Bali amejeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake.Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona sisi sote kama kondoo tumepotea kila mmoja wetu amegeuka njia yake mwenyewe na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.

Luka 22-1:2
Ikakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu iitwayo sikukuu ya Pasaka. Na wakuu wa makuhani na waandishi wakitafuta njia ya kumuua maana walikuwa wakiwaogopa watu.
(Utaona hata hapa walioshiriki kumuua Yesu bado walikuwa ni makuhani wale wale ambao walishusha sanduku kule kwenye hekalu)

Luka 22-7
Ikakaribia sikukuuu ya mikate isiyotiwa chachu ambayo ilipasa kuchinja Pasaka. Akamtuma Petro na Yohane akisema nendeni mkatuandalie Pasaka tupate kula.
(Yesu anashiriki kuandaa Pasaka yake mwenyewe)

Luka 23-33
Na walipofika mahali paitwapo fuvu na kichwa ndipo walipomsurubisha yeye na wale wahalifu moja upande wa kuume na moja upande wa kushoto.

Luka 23-45:47
Jua limepungua nuru yake pazia la hekalu likapasuka katikati. Yesu akalia kwa sauti kuu akisema Ee Baba mikononi mwako naiweka roho yangu.Alipokwisha kusema hayo alikata roho.Yule akida alipoona yaliyotukia alimtukuza Mungu akisema Hakika yake mtu huyu alikuwa mwenye haki.
(Kumwagika kwa Damu ya Yesu kwaleta ukombozi mwingine kwa kupasu kwa pazia hekaluni)

Marko 16-2
Hata alifajiri mapema siku ya kwanza ya juma wakaenda kaburini jua lilipoanza kuchomoza wakasemezana wao kwa wao ni nani aliyeviringisha jiwe hili mlangoni pa kaburi.(Utaona ufufuko waleta tumaini jipya kwa Ukombozi wetu)
Pasaka ni kufutiwa dhambi na kuletewa uzima tena kwa kukubali kuzaliwa mara ya pili kwa kumkiri Yesu na kurudi katika urithi wa kiti cha Enzi
Ameni

 

Comments