UPANGA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

Na Godfrey Miyonjo

“Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu” WAEFESO 6:17.
BWANA YESU asifiwe milele.
Wapendwa ikumbukwe kuwa imeandikwa “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa……….” HOSEA 4:6.
Mungu aliyasema haya kwasababu ya makuhani ambao walikuwa hawatimizi wajibu wao wa kuwafundisha watu kweli ya Mungu.
Mungu alisema na anaendelea kusema hata leo kwakuwa Mungu anajua kuwa mtu asipoijua kweli hakika mtu huyo hayuko huru (yupo chini ya muuaji shetani) na wakati wowote ataangamizwa.
Ni vigumu sana kwa wasiopata neema ya kumjua YESU kuyaelewa haya.
Ndiyo maana BWANA YEASU aliposema habari ya utumwa mahali flani watu hawakumwelewa.
“Basi YESU akawaambia wale wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli, tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru” YOHANA 8:31-32.
Hao wayahudi walishindwa kuelewa kwakuwa walikuwa hawajui kuwa kuna utumwa wa mwilini na utumwa wa rohoni.
Lakini mimi na wewe tunapaswa kujua kuwa kuna utumwa wa mwilini na utumwa wa rohoni.
Na tukisha yajua haya tuje sasa na tujitafutie “MAPANGA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO”
Watu wengi leo hatuna mapanga katika ulimwengu wa roho.
Watu wengi leo wanaangamizwa (wanauawa) kizembe kwakuwa wamelikataa neno la Mungu.
Imeandikwa “ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu” EFESO 6:17. hivyo anayelikataa neno la Mungu huyo hana silaha katika ulimwengu wa roho.
Biblia haitufundishi kupambana kwa jinsi ya mwili, bali inatutaka tupambane kwa jinsi ya roho.
Ndiyo maana imeandikwa “Hatimaye mzidi kuwa hodari katika BWANA na katika uweza wa nguvu zake, vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuweza kuzipinga hila za hila za shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya ya majeshi ya mapepo wabaya katika ulimwengu wa roho” WAEFESO 6:10-12.
Hivyo tunapaswa kujua kuwa hata kama tumeokoka lakini hatuna neno ndani yetu hakika tutapigwa vita na mwisho wa siku tutaanguka (tutarudi nyuma) au tutauawa.
Ndiyo maana imeandikwa Pia “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote,……..” WAKOLOSAI 3:16.
Rafiki yangu tambua leo UPANGA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NI NENO LA MUNGU.
Na hii ni Kwa wanadamu wote Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
ASIYE NA UPANGA NA ANUNUE SASA KWA BWANA YESU, NA ALIYE NA UPANGA NA AHAKIKISHE UPANGA WAKE UMENOLEWA, ILI KUWEZA KUPAMBANA SIKU YA UOVU.

Ni Mimi ndugu yenu katika Kristo
Godfrey Miyonjo (Mtu wa Milki ya Mungu).

Comments