UTAMBUE WENYEJI WAKO ULIKO NA KUISHI KATIKA UTARATIBU WA WENYEJI WAKO UKIWA DUNIANI.

Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe!
Karibu tujifunze pamoja Neno la Mungu ili tuzidi kukua katika maisha ya kiroho.Ombi langu Mungu akufunulie siri iliyoko katika somo hili upate kuelewa kile anachoaka uelewe kama alivyonifunulia mimi,Karibu na Mungu akubariki.
Ebu tusome pamoja kitabu cha Wafilipi 3:20 maandiko yanasemahivi,,"Kwa maana sisi,wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi,Bwana Yesu Kristo"...Bwana Yesu asifiwe!
Ukisoma maneno hayo ya Paulo utagundua anaz ungumz ia maswala ya ..ULIMWENGU WA ROHO...Ambako kuna utaratibu wake ambao mtu aliyeokoka anapaswa kuishi kwa utaratibu wa...,WENYEJI WAKE..na wakati huo akiwa duniani. Ukisoma Waebrania 6:4 kuna kitu cha ajabu hapo anasema,,"KWA MAANA HAO WALIOKWISHA KUPEWA NURU,NA KUKIONJA KIPAWA CHA MBINGUNI, NA KUFANYWA WASHIRIKA WA ROHO MATAKATIFU; angalia haya neno..." NURU,KIPAWA CHA MBINGUNI,WASHIRIKA WA ROHO" Haya mambo ni ya mbinguni umepewa kutoka katika "WENYEJI WAKO" yaani Mbinguni. Nikisema hivi utanielewa, kama uko ndani ya Yesu basi ujue uko mbinguni na wewe.Utauliza "Emmanuel umejuaje? Kasome biblia yako maandiko yanasema..."AKATUFUFUA PAMOJA NAYE, AKATUKETISHA PAMOJA NAYE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO,KATIKA KRISTO" (Waefeso 2:6)
Mungu anapotaka tutazama sisi anatuona "NDANI YA YESU" ndiyo maana ambao hawajaokoka hawako katika ulimwengu wa roho, kwa sababu hawako ndani ya Yesu maana Yesu ameketi lakini wao hawajaketi, kwa nini hawajaketi? kwa sababu hawako "NDANI YA YESU"...Glory to Jesu!

Swala la kuwa mwenyeji maana yake "MADHINGIRA" ya huko unayajua huwezi kusema wewe ni mwenyeji wa Dodoma kama Bungeni hupajui, unaposema wewe ni mwenyeji wa eneo flani maana yake maeneo hayo umehi kukaa na kujua taratibu zake. Kadharika huwezi kuwa "MWENYEJI WA MBINGUNI" wakati hujapewa nuru ndani yako na huna "USHIRIKA" na Roho Mtatatifu.
Lakini kama wewe ni mwenyeji wa Mbingu,,,ooh! uwe na uhakika utaishi kwa taratibu za wenyeji wako ukiwa duniani, maana yake nini? maana yake umeketi pamoja na Yesu mbinguni hivyo naisha yako yataonekana kimbinguni mbinguni maana utakuwa tofauti na watu wa dunia hii, kwa sababu wewe si wa hapa duniani una mfumo wa maisha ya mbinguni.....Bwana Yesu asifiweeee,!

UTAJUAJE KAMA UNAISHI KATIKA UTARATIBU WA WENYEJI WAKO WA MBINGUNI NA UKIWA DUNIANI?
Fuatana nami katika somo lijalo.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA BAADA YA KUFA NI HUKUMU.(Waebrania 9:27)
NUNGU AKUBARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments