UTUKUFU NA HESHIMA KUU NI ZA BWANA YESU.

Na Peter M Mabula , Maisha ya ushindi Ministry.


BWANA YESU asifiwe.

Naomba tumpe BWANA YESU utukufu na heshima siku zote za kuishi kwetu maana alitupenda kwanza YESU tulipokuwa tungali tuna dhambi, akaja kutuokoa. YESU ndiye aliyeanza kutuchagua sisi ili tu tuhusike na uzima wake wa milele.
Kuthibitisha hilo BWANA YESU anasema 
Yohana 15:16 ''   Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni. ''

-Hakuna upendo zaidi ya huu.

BWANA YESU aliacha enzi yake na mamlaka yake ya kiungu mbinguni ili tu aje atuokoe wanadamu ambao tulikuwa kwenye dhambi na tukielekea jehanamu bila kujua.
Wafilipi 2:5-7 '' Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya KRISTO YESU;  ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya MUNGU, naye hakuona kule kuwa sawa na MUNGU kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;  bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; '' 
-Hakuna hata mmoja anayeweza kuacha cheo kikuu na kuja kuwa kama mtumwa mbele ya wanadamu aliowaumba ili tu kuwakamilishia wokovu wale wanadamu wanataopenda.
-Hakuna nayelazimishwa kwenda uzima wa milele ila jambo la kujua ni kwamba Uzima wa milele haupatikani nje na BWANA YESU.

Kuna wengine BWANA YESU alituokoa tukiwa ndio tunaanza kuingia kuzimu, tuko kwenye giza nene ila akatuchomoa na kuturudisha uzimani ili tumtumikie.
1 Petro 1:3-8 '' Ahimidiwe MUNGU, BABA wa BWANA wetu YESU KRISTO, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake YESU KRISTO katika wafu;  tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. Nanyi mnalindwa na nguvu za MUNGU kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake YESU KRISTO.   ''



-Kama kuna siri ambayo wanadamu wengi hawaielewi basi ni kuhusu uzima wa milele.

Hakuna uzima wa milele nje na YESU KRISTO. Kama wanadamu wote wangeuelewa vizuri uzima wa milele basi hakika wote wangemkimbilia BWANA YESU na kuokolewa.
Warumi 10:11,13 ''Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka.   ''



Hata leo dini nyingi hutumia tu kauli za YESU  na kufurahi ila hawajui kwamba hakuna uzima nje na YESU KRISTO.



shetani alipanga tumsindikize jehanamu lakini BWANA YESU akatushika mkono na kututoa kwa shetani na sasa tuko kwenye nuru yake ya ajabu.
1 Petro 2:9-11 '' Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya MUNGU, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la MUNGU; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. ''



Tukijitenga na YESU tumejitenga na uzima wa milele.

YESU KRISTO ni MUNGU mwenye nguvu na ndiye mwamuzi wa wote.
Yohana 5:21-23 '' Maana kama BABA awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na MWANA awahuisha wale awatakao. Tena BABA hamhukumu mtu ye yote, bali amempa MWANA hukumu yote; ili watu wote wamheshimu MWANA kama vile wanavyomheshimu BABA. Asiyemheshimu MWANA hamheshimu BABA aliyempeleka. '' 
-Hii ni siri kubwa sana kutoka kwenye andiko hapo juu.
Heshima ya BABA ndiyo Heshima ya MWANA.
MWANA ndiye atakayehukumu siku ya Mwisho.
Ukijitenga na MWANA wa MUNGU umejitenga na uzima wa milele.
Kama kuna mabye hapaswi kukimbiwa wala kukwepwa basi ni BWANA YESU KRISTO.

Siku kama ya leo unakumbuka nini?

-Je unakua kiroho au unadidimia kiroho?

-Je bado umeshikilia msimamo wako wa kwenda uzima wa milele au umekubali  dhambi zikushike mkono?
1 Yohana 2:15-17 '' Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele. ''



Wengi wanarudi nyuma kwa kuanza kuipenda dunia lakini ni hatari maana kuna humumu.

Hatutakiwi kuishi kwa ajili yetu bali tuishi kwa ajili ya KRISTO.



Watu wengi hudhani ya kuwa kuna kutubu au kutubishwa baada ya kufa.

hakuna kitu kama hicho na wanaoombea marehemu asamehewe dhambi zao hawajui walitendalo.
Wagalatia 9:27 '' Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; ''



Siku kama hii ni ya kujitafakari na kuishi katika mpango wa MUNGU wa uzima.



Siku ile ya Mwisho YESU atakuja na malaika zake wote.

Je mgeni wa nani siku hiyo?

Siku hiyo sisi sote tutakuwa wageni, Mwenyeji atakuwa ni BWANA YESU na atatuambai uridhini uzima wa milele ulio tayari kwa ajili yenu.

Wewe je unayemkataa YESU leo utakuwa wapi?
1 Thesalonike 4: 16-17 ''16 Kwa sababu BWANA mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya MUNGU; nao waliokufa katika KRISTO watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki BWANA hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na BWANA milele.   ''
-Unayedhani YESU ni Nabii tu siku hiyo utajua kwamba YESU KRISTO ni MUNGU mkuu na ni MUNGU Mwenyezi.
Ufunuo 1:7-8 ''Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.  Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema BWANA Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. '' 
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments