UZINZI NA UASHERATI MPAKA LINI?

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Nakukaribisha katika kujifunza Neno la uzima.
Wanadamu Wengi Wanawake, Wanaume Na Vijana Wanatamani Kuacha Uasherati Lakini Hawawezi Kuacha. Unajua Ni Kwanini Hawataki Kuacha? 
Ni Kwa Sababu Hawajaamua Kuacha, Maana Aliyeamua Kuacha Kitu Lazima Atakiacha Tu.
Biblia iko wazi kabisa juu ya kuwaonya wanadamu ili waache mabaya na kumpendeza MUNGU.
1 Kor 6:18 '' Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. '' 
-Tumepewa agizo na amri kwamba tuukimbie uzinzi na uasherati.
-Kila mmoja anatakiwa kuacha uzinzi na uasherati.
-Kila mmoja anatakiwa asifurahie kuitwa kahaba au kuitwa malaya au kuitwa kiwembe au kuitwa basha bali kila mmoja atubu na kuacha dhambi hiyo mbaya.
unajua ni kwanini tunatakiwa kuikimbia zinaa?
Ni kwa sababu.
1Kor 6:16a ''Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? ''
-Ndugu kama hujui kwamba aliyeungwa na kahaba na yeye ameubeba ukahaba, basi tambua leo.
-Kama unatamani kuacha ukahaba lakini unaona kuna kitu kinakuzuia ni kwa sababu tu hujaamua kwenda mbinguni, ungeamua kwenda uzima wa milele ungeacha.
-Wengi wanafuga dhambi na kumpangia MUNGU siku yao ya kutubu. Kuna mtu anafanya maovu mengi tu lakini ukimwambia kwamba tubu na kugeuka anakuambia kwamba labda mwakani atatubu. Ukimuuliza kwamba ''je una uhakikka kwamba mwakani utakuwepo'' anasema ''labda tu'' kwahiyo kutubu ni labda na kuwa hai hiyo siku ya kutubu anasema ni labda tu. ndugu zangu hiyo ni hila ya shetani kuhakikisha kwamba wanadamu hawaendi uzima wa milele.
MUNGU anachukia sana uovu huu.
MUNGU hapa anasema '' Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba. Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake.-Yeremia 5:7-8 ''
-Ndugu, kama inakuhusu tubu leo na geuka, BWANA YESU yuko tayari kukusamehe kama ukiamua kumpokea na kutubu na kuanza kuishi maisha matakatifu.

- Kufuga Dhambi Ni Kujipeleka Jehanamu Mwenyewe. Unajua Kabisa Kwamba Unayoyafanya Ni Machukizo Kwa MUNGU Lakini Dhambi Hizo Unazifuga Mpaka Zimekua Na Umri Mkubwa Lakini Kutubu Hutaki. Siku Zote BWANA Anatuma Watumishi Wake Ili Tu Wewe Utubu Na Kumpokea YESU Lakini Wewe Umefanya Mgomo Baridi.BWANA anachukia uzinzi, ona hapa katika neno la unabii ambalo lina maana sana hata muda huu 
Ezekieli 23:1-3,8,11,14,18  '' Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba. .....Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake. Wala hakuyaacha mambo yake ya kikahaba tangu siku za Misri, kwa maana wakati wa ujana wake walilala naye, wakayabana matiti ya ubikira wake wakamwaga uzinzi wao juu yake. ..... Na umbu lake, Oholiba, akayaona hayo walakini alizidi kuharibika kuliko yeye, kwa kupendelea kwake, na kwa uzinzi wake, uliokuwa mwingi kuliko uzinzi wa umbu lake. .... Naye akaongeza uzinzi wake; kwa maana aliona watu waume, ambao sura zao zimeandikwa ukutani, sura za Wakaldayo zilizoandikwa kwa rangi nyekundu; ....  Basi alifunua uzinzi wake, na kufunua uchi wake; ndipo roho yangu ikafarakana naye, kama ilivyofarakana na umbu lake.''
-Ndugu kama inakuhusu basi tubu na kugeuka, uzinzi ni mbaya na wazinzi hawataurithi uzima wa milele labda watu kwanza.
-Umetenda sana dhambi hii, MUNGU amekuvumilia sana lakini leo anakuonya kupitia neno lake. Ndugu, Geuka, BWANA YESU atakusamehe na utaitwa mtakatifu badala ya jina lako lililozoeleka la kahaba au malaya. 
 Mathayo 5:27-30 ''  Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. ''
-Ndugu, kama inakuhusu tubu na kugeuka.
-Kata mkono wako unaokukosesha yaani ailisha hata safari ya kwenda kuzini mliyoahidiana na yule ndugu.
-Ng'oa jicho lilaokukosesha yaani futa hata namba za huyo anayekulazimisha mwende kuzini, mshtaki hata kwa wazazi wako ili tu akome tabia yake hiyo mbaya. 
Ndugu, Kufuga Dhambi Ni Kujipeleka Jehanamu Lakini Kutubu Na Kumpokea BWANA YESU Ni Kujipeleka Mbinguni. Wokovu Ni Kwa Ajili Yako Na Sio Wengine, Uzima Wa Milele Ni Kwa Ajili Yako Binafsi Na Sio Vinginevyo, Unaweza Ukaukosa Uzima Wa Milele Kama Tu Utaendelea Kufuga Dhambi Hadi Dhambi Hizo Zitazaa Jehanamu. BWANA YESU Anakuita Leo Ndugu Yangu, Mpokee Na Jina Lako Litaandikwa Kwenye Kitabu Chake Cha Uzima.
Marko 10:11-12 ''  Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake; na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.'' 
-Ndugu, kama inakuhusu tubu na kugeuka, BWANA YESU atakupokea kama ukitubu na jina lako litabadilika, badala ya kuitwa mzinifu utaitwa mtakatifu. wafuate wachungaji wakusaidie.

 Jiulize, Ukiwa Unaumwa Sana Kisha Ukaenda Hospital, Doctor Akakutibu Kisha Akakuambia Usile "Tena Chipsi Maana Zinazidisha Ugonjwa". Nakuambia Hata Kama Unazipenda Vipi Chipsi Lakini Hutakula, Hata Kama Ulikuwa Huwezi Kuishi Bila Kula Chipsi Wakati Huu Utaacha, Hata Kama Kuna Mtu Anakushawishi Utakataa, Utasema "Nikila Nitakufa" .

 Sijui Kwanini Tunayatii Sana Ya Wanadamu Kuliko Ya MUNGU?. Ni Heri Tungemtii MUNGU Zaidi. 
Wewe Mgonjwa(mwasherati) Mara Nyingi Umeenda Hospitali(kujifunza Neno La MUNGU), Daktari(BWANA YESU) Amekutibu(Umeombewa Na Kufunguliwa), Daktari Amekushauri Uache Kula Chipsi(uache Kuzini) Mbona Hutii?.
1 Kor 6:13-15 '' Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini MUNGU atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa BWANA, naye BWANA ni kwa mwili. Naye MUNGU alimfufua BWANA, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya KRISTO? Basi nivitwae viungo vya KRISTO na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! ''
-Ndugu mpendwa, kama inakuhusu tubu na kugeuka.
-Kama huwa unaenda kanisa ili kujificha tu wasikujue kwamba wewe ni mzinzi au mwasherati, tubu na kugeuka.
-Kama unatumika madhabahuni huku unafanya uzinzi au uasherati, tubu na kugeuka.
-Kama unaimba au huwa unahubiri harafu unauchafua mwili wa KRISTO, tubu na kugeuka.
BWANA YESU anakutaka ugeuke na kutubu leo. 

 Ndugu, Kama Umeamua Kabisa Kuacha Uzinzi Litii Neno La MUNGU. Kuna Hukumu Kwa Wazinzi.
Waebrania 13:4 '' Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.''
-Wewe kama ni mwanandoa lakini unaisaliti ndoa yako kila mara, tubu na kugeuka. kuna adhabu kwa wazinzi kama hawatatubu.
-Ndugu, kama inakuhusu, tubu na kugeuka, BWANA YESU atakupokea na jina lako litabadilika kutoka kuitwa mzinzi na kuwa mteule wa MUNGU.

2 Petro 2:14-15''wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana; wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;''
-Macho ya uzinzi?
ndugu tubu maana wewe kila binti akipita lazima umpigie mluzi maana una jicho la uzinzi.
-Ndugu tubu na kugeuka.
Najua inakuhusu ndio maana unatakiwa utubu na kugeuka, BWANA YESU atakupokea na utaanza kuitwa mtakatifu ukiwapigia mluzi wanadamu ili uwaambie kwamba '' Twendeni kanisani''

MUNGU Yuko Tayari Kumsamehe Yule Aliyeamua
 1 Kor 6:9-11 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la BWANA YESU KRISTO, na katika ROHO wa MUNGU wetu.''

 Hakuna Mbingu Ya Wavaa Hirizi wala wazinzi, Tupa Hirizi Na na acha hirizi  na Mpokee BWANA YESU Utaokoka.
Nimesema hivyo maana kuna watu hata huvaa hirizi ili kwa njia za kichawi wawapate vijana au mabinti na kufanya nao uzinzi.
Ndugu kama inakuhusu tubu na kugeuka, BWANA YESU atakupokea.
Ufunuo  18:3-6 '' kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na MUNGU amekumbuka maovu yake.Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu.''
-Ana heri yule ambaye atabadilika baada ya kujifunza neno hili la MUNGU.
-Kikombe kimejaa na kilichobaki ni kutubu tu na kumpokea BWANA YESU.
Mwenye sikio la kusikia na asikie.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
mabula1986@gmail.com 

+255714252292.
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments