WOKOVU NINI NINI? NA KUOKOKA NI NINI?




Ole Wangu, Maskini Mimi! Ni Nani Atakayeniokoa Na Mwili Huu Wa Mauti? (Rum.7:21)
SISI JE ! TUTAPATAJE KUPONA TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII ?
(Waebrania 2:3)
Nini Maana Ya Kutojali ?
Ni Kupuuzia.
Ni kulifanya jambo kuwa halina umuhimu wowote.
Ni kuliona jambo kuwa ni la kupoteza muda tu halina faida yoyote na kwamba haliwezi kuathiri kitu
Somo Hili Linafafanua Majibu Ya Maswali Yafuatayo
1. Wokovu maana yake nini?
2. Kuokoka maana yake nini ?
3. Nini tofauti ya Wokovu na Ukombozi ?
4. Nini tofauti ya Kuokoka na Kuongoka ?
5. Tofauti kati ya Dini/Dhehebu na Wokovu ni nini?
6. Ni nini matokeo ya Kuujali au Kutokuujali Wokovu.
6.1. Faida za kuokoka – kuujali Wokovu.
6.2. Hasara za kutokuokoka – kutokuujali Wokovu.
6.3. Je, zipo hasara zozote za Kuokoka ?
7. Mtu / Mwanadamu anatakiwa aokoke lini ?
7.1. Akifa au Akiwa hai ?
7.2. Kabla ya hukumu au baada ya hukumu ?
7.3. Mungu atakapoamua au aonavyo mwenyewe ?
8. Kuokoka kwa mtu ni uamuzi wa nani? Mungu au Mtu mwenyewe?
9. Nifanyeje ili nipate kuokoka ?
10. Mtu atahakikishaje kwamba kweli ameokoka akiwa bado yupo duniani?
11. Sababu gani ambazo wengi huzitoa ili kusema kwamba hawawezi kuokoka?
12. Vikwazo au maadui wa kuokoka /wokovu ni akina nani?






1. Maana Ya Wokovu:
Ni hali au tendo la kuokoa au /na kuokoka.
Kuokoa (To Save) ni kuponya au kuepusha na hatari au kifo, mfano vita na ajali, magonjwa yasiyo na tiba,
maadui, na wanyama wakali.
Hivyo basi, kwa maana ya kiroho,
Kuokoka (To Be Saved) ni kuepuka au kupona na hatari kubwa kuliko zote maishani mwa mwanadamu
milele.
Hatari kubwa maishani mwa mwanadamu ni Dhambi na Mauti ya Kiroho.
2. Maana Ya Kuokoka
Kuokoka
Kwa maana ya kiroho kunamaanisha pale mwanadamu anapoyapokea mambo makuu matatu kutoka kwa
Mungu kwa Imani katika Kristo Yesu ;- Mambo hayo ni yafuatayo:-
1. Kupokea Msamaha wa Dhambi (Forgiveness of sin) kutoka kwa Mungu kwa imani katika Yesu Kristo.
(1Yoh. 2:12.)
2. Kupokea Ondoleo la Dhambi (Remission of sin) kwa kuoshwa / kutakaswa (Sanctification) kwa imani
katika Damu ya Yesu Kristo. (Efe. 5:27).
3. Kuhesabiwa haki (Justification) mbele za Mungu kwa imani katika Yesu Kristo. (Rum.3:21-26)
3. Tofauti Ya Kati Ya Kuokoka Na Kuongoka Na Kukombolewa.
Kuongoka (Proselytised)
o Ni badiliko la mwanadamu kutoka kutotokuwa na msimamo wa kiimani, (au msimamo aliokuwa
nao kiimani, au dini fulani au dhehebu fulani) na kuamua kuifuata imani nyingine.
Mfano;
Kutoka uislamu kwenda ukristo.
Kutoka uyahudi kwenda ukristo.
4. Tofauti Kati Ya Dini, Dhehebu, Na Wokovu.
Dini/Dhehebu
o Ni njia au mpango wa kiimani wa mwanadamu, (japokuwa waweza kuwa wa kweli au wa uongo,)
ambao mwanadamu anaamini umetoka kwa Mungu unaohitaji juhudi ya mwanadamu pia; ilikumuwezesha mwanadamu kumtafuta, kumuona, na kumfikia Mungu katika maisha haya ya duniani
na ya ulimwengu ujao-ili mwanadamu asipotee na kuangamia milele. (Rum. 10:1-3; Kol.2:23.)
Hivyo basi zipo dini za Uongo ambazo wanadamu wanaamini lakini mwisho wake ni kupotea (Mith. 14:12; 16:17;
Zab. 14:2), na tena ipo dini ya kweli ambayo wanadamu wanatakiwa kuiamini lakini haitoshi au haiwezi kumwokoa
mwanadamu (Yak.1:26,27;Isa.43:10-13).
Wokovu
o Ni njia au mpango wa Neema ya Mungu (zawadi, upendeleo wa Mungu) kwa mwanadamu, ili aweze
kumfikia Mungu kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, na si kwa mawazo au njia za kibinadamu.(Isa.
55:8-9).
Hivyo basi, hakuna Wokovu wa Uongo kwa Mungu, bali ni kweli tupu na hakika katika Kristo Yesu. (2Kor.1:19-21).
5) Kombolewa/Ukombozi (Redeemed,Ransomed/Redemption)
o Ni kulipiwa deni au kufutiwa hati ya mashitaka ili mtu atoke utumwani,au kifungoni.
o Hivyo;-Kutoka chini ya utumwa wa shetani na utumwa dhambi (Kol.:2:13-15).
6) Kuokoka/Wokovu (To Be Saved/Salvation)
Ni kupokea rohoni mambo makuu matatu yaliyotajwa hapo juu, yaani;
o Msamaha wa dhambi,
o Utakaso,
o Na kuhesabiwa haki
Mbele za Mungu kwa imani katika Kristo Yesu.
7) Mwanadamu Anatakiwa Kuokoka Lini?
Akiwa hai si baada ya kufa kwani baada ya kufa mtu ni hukumu si wokovu tena. (Ebr 9:27; 2Kor. 6:2)
Mwanadamu wakati wake wa kupokea mambo matatu muhimu kwa wokovu yaliyotajwa hapo juu; yaani msamaha
wa dhambi, ondoleo la dhambi, na kuhesabiwa haki ni wakati akiwa hai, na si baada ya kufa. (2Kor 6:1,2)
Kwani baada ya kufa mtu anakwenda mojawapo kati ya sehemu zifuatazo:
1. Kuzimu / mahali pabaya peponi, kama ni mwenye dhambi ili kusubiri hukumu ya wenye dhambi.
2. Paradiso / mahali pema peponi, kama ni mwenye haki / aliyeokoka, ili kusubiri hukumu ya
watakatifu.
3. Mbinguni - baada ya ufufuo wa kwanza wa wale walioko Paradiso, na baada ya hukumu ya
watakatifu.
4. Jehanamu / motoni - baada ya ufufuo wa pili na hukumu ya wenye dhambi
. Kuokoka Au Kutookoka Ni Uamuzi Wa Mungu Au Mwanadamu?
Ni uamuzi na Uchaguzi wa mwanadamu mwenyewe na sio atakapoamua Mungu Mwenyewe
(Kumb 30:11-20)
9) Nifanye Nini Ili Nipate Kuokoka? (Mdo. 16:30-31; 2:37-42)
Sasa, kwakuwa maneno haya yamewaka na kuchoma moyoni mwako, chukua hatua ya imani kama
ifuatavyo:-
Tubu Msimamo wako usiokuwa wa kweli kiimani na umwamini BWANA Yesu Kikwelikweli.
Omba Msamaha wa dhambi na utakaso kwa damu ya Yesu (Zab 51:)
Kubali Ubatizo wa Roho Mtakatifu na uombe/uombewe ili BWANA Yesu akubatize.
Dumu katika Neno la Mungu
Usitende dhambi tena. Amini ya kuwa Mungu amekusamehe dhambi zako
na sasa umeokoka! Usitende dhambi tena.
Sema/Kiri kwa kinywa chako kwamba umeokoka;
Kufanya hivi si majivuno wala kujisifu (na wala usiwe na nia hiyo moyoni mwako) Bali ni agizo la
Mungu!
Kwani unapokiri unayatimiza Maandiko yafuatayo:-
Unamtukuza Mungu kwa wokovu aliouleta. (Fil.2:11)
BWANAYesu naye atakukiri mbinguni mbele ya Mungu na Malaika wake (Luk.12:7-12)
Unamtangaza BWANA Yesu – Mwokozi kwa wengine ili nao wajue kuwa yuko.
Ni sawa na kuvaa vazi safi jeupe ili usiguse uchafu tena. Waovu hawatakushirikisha maovu yao,
kwani watajua ya kuwa wewe sasa ni mtu wa tofauti.
10) Uhakika Wa Wokovu/Kuokoka.
Mtu atahakikishaje kama kweli ameokoka akiwa bado yupo duniani?
A. Ushuhuda Wa Neno La Mungu
Mungu hasemiUongo. (2Kor.1:20; Yak.1:16-18;)
Neno la Mungu limehakikishwa halina makosa.
B. Ushuhuda Wa Roho Mtakatifu
1. Ushuhuda Wa Ndani/Moyoni
a. Bubujiko la furaha, amani, raha. Ujasiri, wepesi na kujisikia uhakika wa kwenda mbinguni kiasi hata
kunaona kama vile unakawia kuondoka!
2. Ushuhuda Wa Nje
a. Ishara ya kunena kwa Lugha mpya,
b. Ajabu, miujiza na matendo makuu ya Mungu
i. Uponyaji wa
1. (Wagonjwa,
2. Viwete, vipofu, viziwi,
3. Wakoma,
4. Ufufuo wa wafu,
5. Mapepo kutii.
ii. Kubadilika tabia na mwenendo.)
(Mt 11:1-5; Marko 16:16-17. Ebr 2:4; Mdo 5:)
11).Maadui/Vikwazo Vya Kuokoka.
A).Kuto Kuamini-Ebr.3:12-19;
Hofu, mashaka, wasiwasi, kusitasita, kukosa ujasiri, kulihesabu neno la Mungu kama ni upuzi (jambo lisiliomaana
la kupoteza muda tu) (1Kor.1:18, Ebr 13:16-17.)
.Kukata Tamaa. (Ebr.3:12-14; Mt. 24:13)
Kuishia njiani, kuzimia moyo, kufa moyo, kuto kuvumilia.
Kuiacha bidii ya (upendo wa) kwanza.
Kukimbia kuteseka pamoja na Kristo.
.Kufuata Imani Potofu.
Mafundisho ya mashetani na Roho zidanganyazo. (1Tim. 4:1-6.)
(Moyo wa mwanadamu, Yer 17:9. Wajumbe wa Ibilisi. 2Kor.11:14,15)
Kuwafuata Viongozi vipofu wa kiroho/kiimani.
Kufuata imani ya wengi/watu maarufu bila kuiangalia misingi ya kweli ya kiimani ya Neno la Mungu. (Mt.7:13,14)
Kufuata tu dini, dhehebu, au imani fulani wakati moyo si safi mbele za Mungu. (Rum 10:1-4)
Kufuata kitu fulani badala ya imani ya kweli (E.g. Mali/utajiri, ishara, miujiza, maajabu, ishara, heshima/cheo, na
anasa/starehe.Yoh.6:26-40)
C).Kuto Kumtii Mungu
Kukosa uaminifu kwa Mungu, Neno la Mungu, na Roho wake Mtakatifu; uongozi wa kiroho kupitia wajumbe wa
kweli wa Mungu.
Kuuacha mwenendo mtakatifu, kutokujikana nafsi, kuto kusikiliza na kuyafanya kwa bidii maagizo ya Mungu.
Kufanya yasiyo mapenzi ya Mungu (hata kama ni mema machoni pako)
Kujifunza siku zote bila kubadilika.
D).Kutazama Nyuma
Kama mkewe Lutu.
Kuyaangalia yale ya dhambi uliyoamua kuyaacha na kuyatamani tena. (Vitunguu saumu)
Kuyarudia tena makosa na dhambi ulizoacha. (Matope, Matapishi).
Kuyakumbuka makosa uliyoyatubu na kujiona bado una dhambi hujasamehewa, wakati Mungu aliisha kusamehe,
kukuondolea dhambi na kukuhesabia haki.
Kuyaangalia /kuyakumbuka matendo mema uliyojaliwa kuyatenda na kuona kama umetenda vya kutosha mbele za
Mungu kukufanya mwenye haki, kisha ukauzoelea wokovu na kutenda dhambi.
Eze.18: Samsoni (Amu.14:)
E).Unafiki
Kujifanya mwenyewe kuwa mwenye haki mbele za watu wakati kiroho ni mchafu, unanuka, na hufai mbele za
Mungu. (Luk. 18:
Kufuata mikate-mali, cheo, kujijengea jina, kuoa/kuolewa, misaada, n.k.
Unakuwa ukionyesha mema kwa watu, hadharani, wakati sirini unafanya kinyume, ukisahau kwamba Mungu
anakuona huko sirini na Yeye ndiye atakayekuhukumu!
Kuwaambia wengine watende mema wakati wewe mwenyewe hutendi (Fuata maneno yangu si matendo yangu)
Hivyo unakuwa kama kibao cha kuwaonyesha tu watu njia wakati wewe mwenyewe huendi mbinguni, bali unakuwa
mtu wa kukataliwa (1Kor.9:27)
Kuitumia imani ya wokovu (ukristo) ili kuficha maovu-kujifanya malaika wa nuru kumbe
ni mitume wa uongo (wajumbe wa shetani)

12) Sababu Ambazo Wengi Huzitoa Kama Vizuizi Vya Kuokoka Duniani
(Baada ya mahojiano ya ana kwa ana na watu mbalimbali.)
Mimi bado sijaamua nitaokoka baadae.
Jibu Mith. 27:1, Yak.4:14, 2Kor.6:2, Mhu.9:12.
Nitaokoka lakini mpaka nipate kwanza pesa, nyumba, gari,au nioe.
Jibu: Luk.12:16-20 Mk. 8:36.
Nitaokoka nikiwa mzee, maana nikiwa mzee tamaa zitaisha.
Jibu: Mhu.12:1, 10:14 Mt.24:42,44.
Siwezi kuacha dini ya baba yangu au dini yetu.
Jibu: Eze.20:18, Mk7:8-9.
Lakini kunywa pombe kidogo haikukatazwa, bali kulewa ndiyo kumekatazwa.
Jibu: Mith.23:20, Isa.5:22-24.
Sigara, tumbaku, na ugoro kwani ni dhambi? Si naweza kuendelea kutumia?
Jibu: Isa 55:2; 50:11.
Lakini mimi ni mkristo, nilibatizwa nikiwa mtoto, mafundisho ya dini yangu siwezi kuyaacha.
Jibu: Tit.1:16, Luk.6:46, Rum.6:13-14.
Wote tunamwamini Mungu mmoja ila tunatofautiana tu katika kumueleza Yesu, hivyo wote tutakwenda
mbinguni.
Jibu: Yak.2:19, 1Tim2:5, 1Yoh.15:23, Yoh.14:6.
Wokovu na utakatifu si hapa duniani hivyo haiwezekani mtu kuokoka akiwa hapa duniani.
Jibu: Zab.16:3, 1Pet.1:8-12, Luk.19:9-10, Yoh.5:34, Tit.2:11-12; 3:3-4, Fil4:13.
Mimi ni muamini wa kanisa, natoa sadaka, nasali mara… kwa siku, tena mimi ni kiongozi wa….
Jibu: Mk.7:6, Amo. 5:21-22, Eze.33:31-32.
Mimi nikiokoka nitakuwa masikini maana walokole (waliookoka) wote ni masikini.
Jibu: Mt.27:57, 3Yoh.1:2, Hag.2:8.
Lakini Kucheza muziki, mpira, kwenye sinema,si dhambi.
Jibu: Isa.5:12, 14.
Niliwahi kuokoka kisha nikaacha kwa sababu ninapenda dhambi.
Jibu: 2Pet.2:20-22, Ufu.2:4-5.
Mimi niliwashinda wengi waliowahi kunishauri kuokoka, nimeshindikana, utaweza wewe? Hata muhubiri
maarufu….. ameshindwa.
Jibu: Mith.29:11.
Mimi ngoja nikamuulize…kwanza, nikaombe ruhusa kwanza kabla ya kuokoka.(e.g.
baba,mama,mume,mke,rafiki,)
Jibu: Gal.6:5; 1:15-17, Luk.20:34-36, Mt.11:12.
Mimi siwezi kuokoka, mbona walokole wengine wanafanya dhambi?
Jibu: Rum.14:12, Zab.37:37.
Ninafikiri iko siku nitaokoka, nitaokoka siku moja.
Jibu: Rum.9:16, Zek.4:6.
• Arehemuye anasema/anataka sasa, siyo siku unayotaka wewe,
• Utakapotaka wewe yeye hataki kwani muda wake umekwisha kupita. (2Kor.6:2)
Mimi familia yangu ni kubwa, bila kula rushwa siwezi kuitunza lazima nipate rushwa.
Jibu: Mt.6:25,33, 1Pet.5:6-7.
Lakini kuokoka si ni kutangatanga tu? Yesu akirudi si atanikuta ninatangatnga?
Jibu: Mt13:45, Mdo.26:4-5,9-18.
Mimi kuokoka napenda, lakini napika au nauza pombe.
Jibu: Isa.5:11; 55:11, Mk.9:42-43.
Mimi baba yangu ni mchungaji, nitamdharirisha baba yangu.
Jibu: Zek.14:16-20.
Ninyi ni manabii wa uongo, wanaosema wameokoka (walokole) ni manabii wa uongo.
Jibu: Yoh.13:34-35, Hes.22:18, Eze.2:7; 13:9-10, Isa.48:22.
Wanaookoka ni masikini, wenye shida, na wasiosoma, Mimi ni tajiri siwezi kuokoka.
Jibu: Mt.27:57, Mdo. 17:12.
Kanisa letu ndilo la kwanza, dini yetu ndiyo ya kwanza; sasa kuokoka kumetoka wapi?
Jibu: Yoh.14:6; 10:29, Mdo 2:37-42.
Hivi kweli inawezekana kuokoka?
Jibu: Mt.19:25, 26.
Kuokoka ni dini mpya, mbona zamani haikuwepo?
Jibu: Mdo.2:46-47.
13). Matokeo Ya Kuujali Wokovu.
Faida Za Kuokoka.
Zipo faida nyingi sana, zisizohesabika, bali hizi ni baadhi tu kati yake!
a) Kukombolewa, yaani Kulipiwa deni (Kufutiwa mashitaka) ili kuondolewa chini ya kongwa la utumwa wa shetani
na dhambi. (Kol. 2:12-15)
b) Kuhamishwa kutoka utumwa wa shetani na kuingizwa katika ufalme wa Mungu, ndiyo maana BWANA Yesu
alianza mahubiri yake kwa neno hili “Tubuni na kuiamini Injili…”(Mt
c) Kuzaliwa Upya kiroho, yaani kuzaliwa mara ya pili; ili kufanyika Mwana wa Mungu na kuwa kiumbe kipya.
(Yoh.1:12,13; 2Kor. 5:17)
d) Kutumikiwa na Malaika wa Mungu; (Ebr.1:13,14)
e) Kulindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani. (1Pet. 1:3-5; Zab.34:7)
f) Kupewa ahadi ya Baba, yaani Roho Mtakatifu na Ujazo (kutawaliwa/kuongozwa) wa Roho Mtakatifu.(Mdo.2:37-
40 )
g) Kuwa Mtakatifu ungali bado upo duniani na Kumpendeza Mungu, jambo ambalo wengi leo wanasema
haiwezekani; LAKINI, (Zab.16:3):
(a) Yasiyowezekana kwa Mwanadamu kwa Mungu yanawezekana.(Mt. 9:25)
(b) Yote yawezekana kwake yeye aaminiye (Marko 9:23).
(c) Tunashinda na zaidi ya kushinda kwake yeye atupendaye. (Rum. 8:31-39).
(d) Ni neema ya Mungu si kwa uwezo wa Mwanadamu. (Efe.2:8-9)
h) Kuwa wanafunzi wa Kweli-Kweli wa BWANA YESU. (Yoh. 8:31,32)
i) Kusikilizwa na kujibiwa maombi mbele za Mungu.
j) Kuwa na mamlaka na amri juu ya nguvu za shetani, mapepo, majini, magonjwa, sumu, na nguvu zote za
uharibifu (Marko 16:17-20; Luka 10:17-20)
k) Kubarikiwa maishani- milele.
l) Kuruzukiwa na Mungu kuurithi uzima wa milele.
m) Kuepushwa na janga kuu litakaloupata ulimwengu wote, nalo ni,
(1) Dhiki kuu,
(2) Moto wa milele - Jehanamu.
(3) Hukumu ya milele.(Rum. 8:1)
Hatari Za Kutokuokoka.
Zipo hatari/hasara nyingi sana, zisizohesabika, bali hizi ni baadhi tu kati yake!
a) Kuwa mtumwa wa dhambi na wa shetani.
b) Kushindwa kuacha dhambi, kuwa mwenye dhambi, na kufa na dhambi.
c) Kutokuzaliwa Mara ya pili.
d) Kukosa ulinzi wa nguvu za Mungu.
e) Kuwa mwana wa Ibilisi/Shetani.
f) Kusumbuliwa na mapepo na mashetani.
g) Kuikosa ahadi ya Mungu Baba (Kumkosa Roho Mtakatifu)
h) Kulaaniwa maishani-milele.
i) Kufutwa jina katika kitabu cha uzima wa milele.
j) Kutokusikilizwa na kutokujibiwa maombi mbele za Mungu.
k) Kuukosa Urithi wa Uzima wa milele.
l) Kutupwa katika ziwa liwakalo moto wa kiberiti (Moto wa milele, au Jehanamu).
m) Kuingia gizani kwenye kilio na kusaga meno milele.

 

Comments