YESU NDIYE MWOKOZI WA WATU WOTE.

Na Emmanuel Kamalamo

>>KUZALIWA KWA YESU.
Ni tofauti na wanadamu waliozaliwa.Yeye alizaliwa kwa ROHO MTAKATIFU na yeye si asili ya mwanadamu bali ni asili ya Mungu.

Vivyo hivyo na sisi tuliompokea Yesu tunazaliwa upya KWA ROHO MTAKATIFU.Tunapokea Aisili ya kiungu kwa sababu tumezaliwa KWA ROHO MTAKATIFU.

>>MAISHA YA YESU.
Yalikuwa maisha yaliyojaa UTAKATIFU bila dhambi, na aliongozwa na ROHO MTAKATIFU siku zote.

Na sisi tuliompokea Yesu tunapaswa kuishi maisha ya UTAKATIFU.Maana amesema,,"Mtakuwa watakatifu kama mimi nilivyo mtakatifu" Kwa hiyo UTAKATIFU tunaupata tunapoishi kwa kuongozwa ROHO MTAKATIFU,maana wote wanaoonfozwa na Roho Mungu hao ndiyo wana wa Mungu.

>>KUTESWA KWAKE NA KUFA KWAKE.
Kweli kifo chake kilikuwa cha tofauti na na watu wote, kiasi kwamba dunia yote ilitikiswa na kukawa na GIZA kwa masaa matu.
Hivyo na sisi tuliompokea Yesu tutateswa kwa ajili ya Kristo na pi lazima tufe pamoja na Kristo. Tunakufa katika maisha ya dhambi kama Yesu alivyoifia dhambi na haimtawali tena. Vivyi hivyo na sisi tukifa pamoja naye dhambi haitatutawala.

>>KUFUFUKA KWAKE YESU.
Ni jambo ambalo limekuwa la KIHISTORIA tangu ulimwengu kuumba.Ni hakika Yesu alifufuka yu HAI yu HAI mpaka sasa. Ni uthibitisho yakwamba mauti haina NGUVU kwake. Hivyo na sisi tuliompokea Yesu tumrfufuka pamoja na Kristo,mauti haina NGUVU kwetu.

Yesu anasema..MIMI NDIMI HUO UFUFUO NA UZIMA.YEYE ANIAMINIYE MIMI AJAPOKUFA ATAKUWA ANAISHI; NAYE KILA AISHIYE NA KUNIAMINI MIMI HATAKUFA KABISA HATA MILELE, JE! UNAYASADIKI HAYO?
PASAKA WETU ALIKWISHA KUTOLEWA NI YESU KRISTO.
MUNGU AKUBARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments