ATAKAYELIPOKEA NENO LA UFALME ATADUMU KATIKA UFALME WA MUNGU.

Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe!
Katika usiku wa NENO LA UZIMA Mungu Roho Mtakatifu aseme nasi usiku huu katika Neno lake ili tuzidi kukaa katika mapenzi yake.
Mathayo 13:1-23.
1 Siku ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari.
2 Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
3 Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda.
4 Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;
5 nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina;
6 na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.
7 Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;
8 nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini.
9 Mwenye masikio na asikie.Sababu ya kusema kwa Mifano
10 Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?
11 Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.
12 Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
13 Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
14 Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema,Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa;Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito,Na kwa masikio yao hawasikii vema,Na macho yao wameyafumba;Wasije wakaona kwa macho yao,Wakasikia kwa masikio yao,Wakaelewa kwa mioyo yao,Wakaongoka, nikawaponya.
16 Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia.
17 Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.Maelezo ya Mfano wa Mpanzi
18 Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.
19 Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.
20 Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha;
21 lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa.
22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
23 Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.Mfano wa Magugu katikati ya Ngano.

Ukisoma maneno hayo ya Yesu aatakutufundisha juu ya kulipokea "NENO LA UFALME" ambalo limebeba Utawala mpya,Uongozi mpya,Maisha mapya na neno hilo la ufalme linahitaji liingie katika miiyo yetu.
Neno hilo ni "MBEGU" ambayo inapandwa katika moyo wa mwanadamu, ukosmo Luka 8:11 na 1 Petro 1:23 utaona maana halisi ya Neno la Mungu kama mbegu linapandwa miiyoni mwetu.
MIIYO YA AINA TATU INAYOWEKEWA VIZUHIZI KUPOKEA NENO LA UFALME.
-NJIANI.
Ni moyo unapokea Neno lakini shetani huja na kuliondoa ndani hiyo mtu huyu hawezi kuwa na maisha ya wokovu.

-MWAMBANI
Ni moyo ambao hauna mizizi ya neno ndani yake,hulipokea na kwa sababu haliwekewi mazingira ya kuliiltunza ili liweke mizizi na kukua.

-MIIBA
Ni moyo unapokea Neno lakini moyo huo unalizuhia hilo neno kwa shughuri za dunia hii,hivyo moyo huo hawezi kulitunza Neno maana masumbu ya dunia yanazuhia Neno lisikae ndani.

Kama moyo wako utakuwa "UDONGO" mzuri basi utapenda kulipokea Neno kila siku na litakaa moyoni mwako na litazaa sana na maisha yako ya wokovu yatakuwa imara siku zote na ndipo utadumu katika "UFALME WA MUNGU"
Weka moyo wako kupata neno kila siku ili ukuwe kiroho.
MUNGU AWBARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments