Naitwa David Stamen. Mimi ni Mwingereza. Naishi hapa Uingereza. Kwa mara ya kwanza nilikuja Tanzania mwaka 1991. Nilikaribishwa kuhubiri na kufundisha semina katika makanisa huko mkoani Iringa na tokea hapo nimekuwa nikija Tanzania mara moja au mbili kwa mwaka nikihubiri pamoja na kufundisha Injili ya Bwana Yesu pamoja na kusaidia kazi ya Bwana makanisani. Nafanya kazi hasa katika mkoa wa Morogoro na nategemea kuanzisha huduma huko Dar Es Salaam. Ninafundisha na kufanya semina kwa wachungaji, viongozi na watumishi wengine wa Mungu, pamoja na vijana na wanafunzi mashuleni. Huduma hii imefika hadi katika makanisa ya maeneo ya Wamaasai. Katika kufanya kazi hii siwakilishi chama chochote wala shirika au hata dhehebu kutoka hapa Uingereza. Isipokuwa nilijiunga na waumini waliopo mkoa wa Morogoro na hapo kwa sasa ndio makao yangu makuu kihuduma. Lakini nafanya kazi ya Mungu pamoja na waumini wa kweli mahali po pote ninapokaribishwa hapo Tanzania. Najua moyoni wangu kuwa Mungu ameniongoza kufanya kazi hii hapo Tanzani ninao moyo na wito wa kumtumikia Bwana Yesu huko Tanzania kwa kadiri ya neema yake. Huwa sitozi pesa wala sitafuti pesa yoyote kwa huduma hii. Najitoa bure tu kwa ajili ya kazi ya Bwana. Zaidi ya hayo yote ninawasaidia makanisa na waumini kwa mahitaji mengine, kama yatima na wajane.
Hapo chini, nipo Dumila kwenye nyumba ya mtafsiri wangu, mchungaji Jorom Gondwe.

Nafurahi sana kuwepo pamoja na washirika porini na kuhubiri Injili! Mimi na mtafsiri wangu huko Mororoi, karibu na Dumila.
Niliwasaidia waumini wa Mororoi kujenga jengo lingine (hapo chini).

Nilihemishiwa kulala katika nyumba ya asili. Nimefanya hivyo mara nyingi!

Kanisa lilipo Dumila. Mchungaji Jorom Gondwe analitumikia kanisa hili.

Semina kwenye kanisa la Kibaoni, karibu na Morogoro. Kiongozi Francis Msendekwa Ndezi analitumikia kanisa hili.

Tuliwasaidia waumini maskini wakati wa njaa. Na ninawasaidia wajane na yatima.


Nilifundisha kwenye semina ya CASFETA huko Morogoro. Wanafunzi wa shule ya sekondari na chuo kikuu.

Hapo chini tunaona vyoo bila milango kwa ajili ya wanafunzi 500 wa shule ya msingi huko Gairo. Niliwahurumia sana!

Niliwasaidia wapate milango. Walifurahi saaaana!

Zaidi ya hayo tunahubiri Habari Njema ya Yesu Kristo!

Kanisa huko Gairo. Ninawatembelea kila mwaka pia. (Hapo chini)

Haya kwa ufupi tu! Ni baraka kwangu na furaha yangu kumtumika Bwana Yesu hapo Tanzania,

Comments