BWANA YESU
atukuzwe ndugu yangu.
Karibu
tujifunze Neno la MUNGU.
Leo
tunazungumzia maombi jambo ambalo ni la lazima kwa kila mteule wa KRISTO.
Maombi ni
maisha na maombi ndio mkono mrefu zaidi wa kupokea kutoka kwa MUNGU.
 ''BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia-Zaburi 5:3'' 
Hata kama
huwa hufundishwi kuhusu maombi lakini naomba utambue leo kwamba maombi ni jambo
la lazima tena la kila siku katika maisha yako ya wokovu.
 ''Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama
 wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa BWANA.-Yakobo 1:6-7'' 
Usipoomba
wakati uko salama tambua kwamba ipo siku utaomba tena kwa kufunga siku kadhaa
baada ya kupatwa na magumu ambayo kama ungeomba muda huu badi hakika mabaya
hayo yangekuja kwako hiyo baadae.
Maombi ni
kuzungumza na MUNGU.
 ''Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye 
MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale 
wamtafutao-Waebrania 11:6''.
Maombi
huboresha uhusiano wako na MUNGU muumbaji wako.
Kinachoonekana
kwako kwa nje ni matokeo ya kile kilichoko ndani.
BWANA YESU anasema '' Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA 
atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, 
nitalifanya.-Yohana 14:13-14''
Maombi
huzalisha utulivu na amani hivyo maombi ni muhimu sana.
Usipopenda
kuomba basi jiandae na magumu ya kiroho maana shetani na watoto wake hapendi
wewe uwe salama tena ukiwa katika wokovu.
 ''Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu-Marko 11:24''.
-Maombi hayatakiwi kuwa ya kipindi fulani tu bali siku zote.
Biblia inakushauri.
ombeni bila kukoma;-1 Thesalonike 5:17 ''
HATARI 7 ZA MTU ASIYEKUWA NA MAOMBI.
         1. 
Usipoomba  unawaimalisha adui zako.
 ''Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.-Yohana 15:7'
''Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.-Zaburi 63:1''
      3. 
Usipoomba  maana yake unafurahia kushindwa kwako.
''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.-1 Yohana 5:14''  
Usipoomba  utabaki kufedheheshwa siku zote.
‘’ Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.-
Mithali 18:21 ‘’
           5. 
Maombi
yanaweza kukuwakilisha mahali huwezi kufika kwa njia ya kawaida. Usipoomba
hutaweza kufika huko
''Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote 
tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;-Waefeso 3:20''  
            6. 
Kama
unataka kufanya mabadiliko ya jambo lolote katika maisha yako kwanza ni lazima
uombe kubadilishwa kwanza wewe kabla ya kuyapokea mabadiliko hayo unayoyataka.
Usipoomba badiliko litachelewa sana kufika.
''Na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.-1 Yohana 3:22'' 
           7. 
Usipoomba
hutaweza kuwa na macho ya kiroho hata uweze kuwatambua na kuwashinda adui zako.
''Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.-Waebrania 4:16''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku 
nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio 
kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na 
utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi 
kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko 
KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana. 
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
Comments