HATAU ZA KUKUFIKISHA KUWA MWANAFUNZI WA YESU NA NA KUWA MKRISTO HARISI.


Bwana Yesu asifiwe!
Namshukuru Mungu anayeni nafasi za namna hii
kwa ajili ya kufundisha maneno ya uzima, Mpango
wa Mungu ni watu wote waokoko na kuingia
mbinguni.
Fuatana nami katika somo hili, na umwambie Roho
Mtakatifu akufunulie siri hii ya uzima na tumaini la
Kristo liwe ndani yako kwa njia ya Imani.

Tuanze kwa kusoma Neno la
Mungu. Mathayo 28:19 "Basi, enendeni mkawafanye
mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina
la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Na
kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi;
na tazama, mimi nipo nanyi siku zote mpaka
ukamilifu wa dahari".

Na Emmanuel Kamalamo.
Hili ni agizo ambalo Yesu analitoa kwa wanafunzi
wake wahakikishe wanawafanya watu kuwa
WANAFUNZI. Ndiyo maana Paulo anasema...
"Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu
vipawa... Naye alitoa wengine kuwa MITUME; na
wengine kuwa MANABII; na wengine kuwa
WAINJILISTI; na wengine kuwa WACHUNGAJI na
WAALIMU; kwa kusudi la kuwakamiliasha
watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata
mwili wa Kristo ujengwe".Waefeso 4:8-12.
Kwa hiyo agizo hili ndilo kuu sana kwa ajili kutimiza

kusudi la Yesu kuja duniani kuuokoa ulimwengu.
Kuwa mkristo si jina tu kuitwa mkristo hiyo uelewe
kama ulikuwa hufaham. Kuwa MKRISTO ni ngazi ya
juu sana aù CHEO cha juu sana ambacho unakipata
baada ya kufahuru kutoka ngazi ya darasa la
UANAFUNZI. Maandiko yanatwambia kwamba,,
"HATA NA SISI TUTAKAPOUFIKIA UMOJA WA
IMANI NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA
MUNGU, HATA KUWA MTU MKAMILIFU, HATA
KUFIKIA KWENYE CHEO CHA KIMO CHA UTIMILIFU
WA KRISTO" Waefeso 4:13.

Nikupe mfano huu utaelewa, huwezi kufika ngazi ya
ELIMU YA CHUO KIKUU kama umeferi form Six,
Ukipita form Six unaingia chuo kikuu, Kadharika
"CHEO CHA UTIMILIFU WA KRISTO" unakipata kwa
kuwa MWANAFUNZI anaye kaa darasani na
KUFUNDISHWA NENO LA MUNGU ambalo litajenga
IMANI yako katika kumfahamu MWANA WA MUNGU
YESU KRISTO, maana twafahamu "Imani chanzo
chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la
Kristo" Warumi 10:17.
Kama hupati mafundisho wewe si mwanafunzi wake
huna daftari na kalamu utarudishwa nyumbani
maana uandiki. Pia na upande huu wa Yesu Kristo
kama hukai darasani wewe utarudi nyuma na
hutakuwa mwanafunzi utakaye fikia kiwango cha
kuitwa MKRISTO.
Kawa ulize wayahudi waliomwani Yesu miongoni
mwa wayahudi wote waliokuwa wanamsìkiliza
watakwambia... "TUKIKAA KWENYE NENO LAKE
TUTAKUWA WANAFUNZI WAKE KWELI KWELI"
Yohana 8:31.

HATAU ZINAZOKUPELEKEA
KUWA MKRISTO

.MAFUTA YALIYO NDANI YAKO
YATAKUFUNDISHA KUISHI KAMA KRISTO.

1 Yohana 2:27-"Nanyi, mafuta yale mliyoyapata
kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya
mtu kuwafundisha…. Lakini kama mafuta yale
yanavyowafundisha habari za mambo yote"
Kristo maana yake "MPAKWA MAFÙTA"au
"MASIHI" ok! Kristo si jina la YESU, Kristo ni nafasi
ya UPAKO WA MAFUTA yaliyowekwa juu yake
akaitwa "KRISTO" Yaani YESU MPAKWA MAFUTA.
Ndiyo maana huwezi kukemea pepo kwa kusema
"TOKA KWA JINA LA KRISTO" ujue pepo hatoki,
maana yake anajua MAKRISTO wengi, ukisema kwa
JINA LA YESU KRISTO pepo anatoka, kwa sababu
umetaja YESU aliyepakwa mafuta.(Isaya 61:1)
Uposema wewe ni MKRISTO unamaanisha
umepakwa MAFUTA, na hayo mafuta yatakufanya
uwe mtu wa tofauti maana yake umetengwa kwa ya
YESU. Na ndipo maisha yako utaishi kama YESU
KRISTO na watu watakuita MKIRISTO.
Ndivyo walivyoitwa WANAFUNZI wa Yesu
"WAKRISTO" pale katika mji wa ANTIOKIA. Mdo
11:26 "WAKAKUSANYIKA PAMOJA NA KANISA NA
KUWAFUNDISHA WATU WENGI. NA HAPO
WANAFUNZI WALOITWA WAKRISTO KWANZA
HAPO ANTIOKIA.

Maana wanafuzi hawa walifundishaw NENO LA
MUNGU na wakaishi kama NENO (YESU) Kunena,
kutembea kuvaa nk. Wakaonekana watofauti na
wengine, watu wakasema "WANAISHI KAMA YESU
KRISTO" inaonekana hawa ni WA KRISTO.
Usijiite MKRISTO tu kama huna MAFUTA
yanayokufundisha kubadili maisha yako na kuishi
kama Yesu Kristo. Paulo alishi kama Yesu ndiyo
maana akawa na ujasiri wa kusema, "MNIFUATE
MIMI KAMA MIMI NINAVYOMFUATA KRISTO.
1 Wakorintho 11:1.
Huwezi kusema wewe ni Mkristo wakati bado una
kunywa POMBE,MWASHERATI,MZINZI,MUONGO,
MWIZI, JAMBAZI, nk
Kubari kukaa kwenye NENO use Mwanafunzi WA
Yesu na uwe Mkristo aliye hai.

KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA BÀADA YÀ KUFA
HUKUMU
(Waebrania 9:27)

MUNGU AWABARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments