HUKUMU HAINA HURUMA YAKOBO 2:13.

https://scontent-lhr3-1.xx.fbcdn.net/hphotos-xpa1/v/t1.0-9/11233539_766073950176122_6232038127824421597_n.jpg?oh=690f83a56220a46f43584e3c6f5d7a53&oe=55C1DA1C
Na Godfrey Miyonjo.

BWANA YESU asifiwe.
Wapendwa ni kweli kabisa kuwa Mungu wetu anatupenda sana, naye ni mwingi wa rehema kwetu, tena si mwepesi wa hasira sasa, lakini ifahamike kuwa haitakuwa hivi siku ya hukumu.
Kumekuwa na watu chini ya jua wanajidaganya pale waendeleapo kutenda dhambi.
Wengine husema kuwa “kama Mungu angekuwa na hasira si angemwangamiza kabisa shetani?”
Utawasikia wakisema “kwanini Mungu alimruhusu shetani atudanganye?”
Mara husema “Ooooh! Tutajitetea kwa machozi siku ile ikifika bhana, naye Mungu atatuhurumia, kwa vile tutakavyokuwa tunalia”
Wengine husema “waovu ni wengi sana kuliko wema, Mungu atatuhurumia siku ile ikifika”
Wengine utawasikia “Mungu mwenyewe atujua kuwa sisi ni dhaifu, hivyo hawezi akatuhukumu”
Haya ni maneno ya kujifariji tu, na faraja hii haitoki kwa Mungu bali yatoka kwa shetani.
Kwa maana imeandikwa “Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiye na huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu” YAK 2:13.
Faraja itokayo kwa Mungu ndiyo hii:
1.Wakati uliokubalika nalikusikia
2.Siku ya wokovu nalikusaidia
3.Wakati uliokubalika ndiyo sasa
4.Siku ya wokovu ndiyo sasa.

Na ndiyo maana ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
HUKUMU HAINA HURUMA, AMUO KUOKOKA LEO KABLA HAIJAJA SIKU ILE YA KUTISHA.

Ni mimi ndugu yenu katika Kristo
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu).

WhatsApp 0757649495.

Comments