IJUE HUDUMA YAKO NA ANAYETOA HUDUMA KATIKA MWILI WA KRISTO. NA INAVYOTENDA KAZI

Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe.!
Ni furaha yangu katika Roho Mtakatifu kupenda
kuujenga mwili wa Kristo katika mafundisho ya neno la Mungu na kwa kadri ya Neema yake aliyonipa nami sina budu kuuitumia Neema hiyo kwa ajili ya watu wengine.

Mungu anapoweka kitu ndani yako ni kwa ajili ya
kulijenga kanisa lake. Sifundishi ili watu wajue
nafahamu kufundusha la asha! Bali nafundisha ili
watu wamjue Kristo kupitia MAFUNDISHO
nayopewa na Roho Mtakatifu wake, maana kwa jinsi ya kibinadamu itanifaidia nini nipoteze muda kwa kukaa na kuandika masomo haya na silipwi na mtu awaye yote, kibinadamu unaweza kuacha; lakini kwa sababu najua ni "WITO" Bwana amenipa nami tumika kwa kadri ya Neema nami nitalipwa na Bwana siku ile.
Karibu katika somo hili ns Roho Mtakatifu akupe kuona kile anata uone katika somo hili katika Jina la Yesu Amen.

Mara nyingi wakristo wengi wameshindwa kujua
WITO WA HUDUMA zao. Na baadhi kuingia katika
huduma ambazo hawakuitwa katika wito huo na
hatimaye kuona kazi ya Mungu ni ngumu.

AINA ZA HUDUMA.
Kuna aina tano za Huduma zinazotenda kazi katika
mwili wa Kristo.
1.MITUME
2.MANABI
3.WAINJILISTI
4.WACHUNGAJI
5.WAALIMU. (
Waefeso 4:9-12)

Majukumu ya Huduma hizi ni kuwakamilisha
WATAKATIFU (WALIOOKOKA) ili na wao washiriki
kudanya kazi ya Mungu kwa karama na vipawa
anavyokirumiwa na Roho Mtakatifu.
JE HUDUMA USOMEWA KATIKA VYUO AU KUPEWA
NDANI YA KANISA?
Jibu ni hapana. Huduma haisomewi wala haipewi na
mtu ndani ya kanisa. Bali Mungu ndiye uumpa mtu
Huduma. Nabii Yeremia alipewa Huduma ya KINABII
kabla hajaumbwa wala kuwekwa tumboni, maandiko
yanasema..."KABLA SIJAKUUMBA KATIKA TUMBO
NALIKUJUA, NA KABLA HUJATOKA
TUMBONI,NALIKUTAKASA; NIMEKUWEKA KUWA
NABII WA MATAIFA" ( Yeremia 1:5)
Kabla Yeremia hajaumbwa alikuwepo katika
mawazo ya Mungu na kazi atakayopewa, lasivyo
Mungu asingesema..."KABLA SIJAKUUMBA KATIKA
TUMBO" maana yake Yeremia alikuwepo na Mungu
alimjua. Na alipoingizwa tumboni alitakaswa. Nini
maana ya "KUTAKASWA" Kutakaswa maana
yake...."KUSAFISHWA NA KUTENGWA KWA AJILI YA KUSUDI
MAALUMU"

Wapo pia waliopewa Huduma tangu tumboni kama
vile YOHANA MBATIZAJI (Luka 1:15) ,SAMSONI
(Waamuzi 13:5), SAMWELI ( 1 Samweli 1:11)
Ndiyo maana waliopewa HUDUMA tangu tumboni
wanapoitwa wanakataa, Mungu huwa anafunga
KUFANIKIWA KWA KAZI ZA MIKONO YAO lengo
waje kwenye HUDUMA. Na wanapotii nakuingia
kwenye Huduma eidha UTUME,NABII,UIN
JILISTI,UCHUNGAJIA AU UALIMU ndipo Mungu
uwabariki.
VYUO SI SAHIHI?
La asha! Ni sahihi. Vyuo vina waalimu ambao Mungu
uwatumia hao kuwaandaa watumishi walipewa
huduma ndani yao na jinsi ya kuitumia huduma na si
kukupa huduma, anayetoa Huduma ni
Mungu....."ALIPOPAA JUU BALITEKA MATEKA,
ALIWAPA WANADAMU VIPAWA.....NAYE ALITOA
WENGINE KUWA MITUME; NA WENGINE KUWA
MANABII; NA WENGINE KUWA WAINJILISTI; NA
WENGINE KUWA WACHUNGAJI; NA
WAALIMU" (Waefeso 4:8,11)
Wanafunzi wa Yesu walifundishwa na Yesu Kristo
mwenywe.. Paulo alipoitwa alikaa chini ya Anania na
wanafunzi wengini pia na Mitume.(Mdo 9:17,27)
Paulo kakaa kwa mitume alikuwa anapewa msingi
ulio imara katika Kristo.

Mpendwa fuatana nami katika somo ili uweze kujua Mungu kakuitia hudama gani na ujue jinsi zinavyotenda kazi kwako.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA BAADA YA KUFA HUKUMU.(Waebrania 9:27)
MUNGU AWABARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments