IJUE HUDUMA YAKO NA ANAYETOA HUDUMA KATIKA MWILI WA KRISTO NA INAVYOTENDA KAZI. (SEHEMU II)

Na Emmanuel Kamalamo.
Bwana Yesu asifiwe!
Namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi nyingine
kuendelea na somo letu ambalo kama kanisa katika
mwili wa Kristo tunapaswa kufahamu jinsi ya
kumtumikia Mungu katika HUDUMA tulizo pewa.
Na ni muhimu kujua unatumika katika Huduma ipi
uliyopewa Mungu au umewekwa na watu, au kwa
ajili ya Pesa? Maana maandiko yasema wazi..."KWA
SABABU WALIO HIVYO HAWAMTUMIKII BWANA
WETU KRISTO,BALI MATUMBO YAO WENYEWE..."
Warumi 16:18. Kwa manitiki hiyo ujue kabisa si kila anayeingia katika huduma yakiutumisha ameitwa na Mungimu, bali baadhi yao wameingia kutafuta maslai.

Mwanzo tuliangalia aina za Huduma, na tukaona
kuna hudama tano na tukasoma kitabu cha
Waefeso 4:9-12.

Tukaangalia je Huduma usomewa vyuoni au kupewa
ndani ya kanisa? jibu ni hapana Huduma anatoa
Mungu mwenyewe. Waefeso 4:8-11.
Tukaangalia kwenda vyuo ni sahii? Ndiyo ni sahihi ili
kuweza kukusaidia namna ya kuitumia huduma uliyopewa na Mungu.
Mfano Wanafunzi wa Yesu walifundishwa na Yesu kwa kukaa chini yake miaka.
Paulo alikaa chini ya Anania na Mitume. Mdo
9:17-28.

UTAJUAJE WEWE UNA HUDUMA IPI
AMBAYO MUNGU AMEIWEKA NDANI YAKO?

Mungu akikupa mojawapo ya Huduma tano (Utumeme, Nabii, Uiinjilisti,Uchungaji, au Ualimu ) ndani
yako utakuwa na MSUKUMO/MZIGO wa kutaka
kutimiza Huduma hiyo kwa njia ya vitendo. Na kila Huduma ina
utendakazi wake, huko mbele tutaziangalia.

Pia Mungu anaweza kusema na wewe kupitia
UNABII kukwambia kukwambia Huduma yako.

1.UTAKUWA NA USHAWISHI WA NDANI KATIKA
ROHO.

2.UTAKUWA NÀ KARAMA YA ROHO INAYOENDANA
NA HIYO HUDUMA.

3.UNAPOIFANYA HUDUMA HIYO UNASIKIA AMANI
NA FURAHA HATA KAMA INAUGUMU.

4.UNAVUTIWA NA KUATHIRIWA NA WATUMISHI
WENYE HUDUMA KAMA YAKO.
Unapoona hali ya namna hiyo inakupasa
uichochoe.Paulo anamwambia Timotheo..."USIACHE
KUITUMIA KARAMA ILE ILIYOMO NDANI YAKO,
KWA UNABII NÀ KWA KUWEKEWA MIKONO YA
WAZEE" 1 Timotheo 4:14.

Mahali pengenine Paulo anamwambia Timotheo,,," KWA SABABU HIYO UICHOCHEE KARAMA YA MUNGU, ILIYO NDANI
YÀKO KWA KUWEKEWA MIKONO YANGU"
2 Timotheo 1:6.

Usijaribu kufanya Huduma ambayo si wito wako
utakwama, maana huna NEEMA ya kukusudia katika
Huduma hiyo...Paulo anasema..."KWA NEEMA YA
MUNGU NIMEKUWA HIVI NILIVYO; NA NEEMA
YAKE ILIYOKU KWANGU ILIKUWA SI BURE, BALI
NALIZIDI SANA KUFANYA KAZI KUPITA WAO
WOTE; WALA SI MIMI, BALI NI NEEMA YA MUNGU
PAMOJA NAMI" 1 Wakorintho 15:10....Bwana Yesu asifiwe!!

Wewe kama ni Kiongozi wa Kanisa usijaribu kumuweka mtu
kuwa MCHUNGAJI,MTUME, MWINJILISTI
NABII AU MWALIMU kwa kumuoña kwa nje, je
Mungu amekwambia? Maana Neema ya kumsaidia
katika huduma hiyo haipo, maana ukimpeleka kijiini atakambia maana NEEMA ya kuchunga mazingira ya namna hiyo haiko juu yake bwana. Pai wewe unamuona Dada
kila wakati anakemea DHAMBI yeye ukimpa nàfasi
wote mnapigwa SALA YA TOBA Askofu mpaka
Mzee wa kanisa alafu unasema..."NIMEPATA
MCH.MSAIDIZI AU WA KUMFUNGULIA KANISA"
Uwe na uhakika atatawanya kondoo maana hukujua
ana huduma hipi ndani yake, maana kila siku yeye ataona dhambi ndani hana NEEMA ya huduma ya uchungaji ya Roho ya upole ya kurejesha pole pole kwa kwa fimbo ya kichungaji.
Ni Muhimu kuwekwa kwenye Huduma yako ndani
ya kanisa ili kazi ya Mungu iende sawasawa. Ezekia
aliwapanga watu sawasawa na Huduma zao. Soma kitabu cha 2
Nyakati 31:2 maandiko yanatwambia,,,"Ezekia akaziweka zamu za makuhani
na walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadri ya
huduma yake.."

JE, HUDUMA TANO ZINATENDAJE
KAZI KATIKA MWILI WA KRISTO?

Fuatana nami katika somo lijalo nawe utabarikiwa.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA BAADA
YA KUFA HUKUMU. (Waebrania 9:27)

MUNGU AKUBARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments