KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

Na Eliapenda Mremi

Biblia imetaja mifano mingi sana ya wanaume kwa wanawake waliopewa uwezo usio wa kawaida wa Kimungu katika utumishi..kwa mantic hiyo basi tunajifunza kuwa KARAMA ZA ROHO ni kama zawadi..yaani haziwezi kufanyiwa kazi ndipo zipatikane bali Roho humgawia yeyote kama apendavyo yeye.
1Kor12:8-10
Kwa mujibu wa scripture karama za Roho Mtakatifu zipo 9 na tutazichambua kwa uchache..Tunaweza kuzigawa katika makundi matatu ambayo ni
{1}ZA KUZUNGUMZA=Aina za lugha, tafsiri za lugha na unabii
{2}ZA UFUNUO=Neno la hekima, neno la maarifa na mapambanuo ya roho
{3}ZA NGUVU=Matendo ya miujiza, imani maalumu na karama za kuponya.

¤Ukweli ni kuwa karama za kusema ndizo zenye kudhihirika kwa wingi sana makanisani, zile za mafunuo hudhihirika kidogo sana sawa na zile za nguvu.
1Kor12:4-7
AINA ZA LUGHA/TAFSIRI ZA LUGHA

Ni muhimu sana sana tuelewe tofauti kati ya matumizi ya lugha na lugha binafsi..sio kila wakati mtu anaponena kwa lugha basi karama ya utafsiri wa lugha hutumika..Hata kanisa la Corintho walikuwa wanakusanyika pamoja na kunena kwa lugha wote kwa mara moja bila tafsiri yoyote (ona 1kor14:6-12)..Mtu binafsi anapoomba kwa lugha yeye tu ndiye hujengwa (ona 1kor14:4a) but karama ya mtafsiri lugha inapotumika kanisa nzima hujengwa (ona 1kor14:4b).
KARAMA YA KUPAMBANUA ROHO
Hii mara nyingi humwezesha mhusika kuona na kutambua kinachoendelea katika ulimwengu wa Roho..Mhusika anaweza kuwaona angels au demons kwa macho yasiyo ya damu na nyama kama ilivyotokea kwa mtume Paulo (mdo18:9-10).
Wakati Elisha na mtumish wake walipokuwa wanatafutwa na jeshi la Shamu wakajikuta wamenaswa ktk mji wa Dotani, mtumishi wa Elisha alipotazama juu ya kuta za mji aliona makundi ya askari yakijikusanya akapata waswas (2waf6:16-17) ila Elisha alipotazama yeye aliona tofauti kabisa..kwa mfano huu unaweza kuona utendaji kazi wa karama hii..Mwisho hii karama SIO ya utambuzi kama wengi walivyozoea kuiita.

Karama za kusema-UNABII
Karama ya unabii ni uwezo usio wa kawaida wa kusema kwa UVUVIO wa Kimungu..kila mara maneno ya nabii huanza na Bwana asema na kumalizia asema Bwana.
Karama hii sio sawa na kuhubiri wala kufundisha ingawaje Mahubiri na mafundisho yaliyovuviwa yana kiwango fulani cha unabii kutokana na upako wa Roho Mtakatifu. Karama ya unabii yenyewe hujenga, hufariji na kutia moyo (1kor14:3) hivyo basi karama ya unabii peke yake haina ufunuo wowote..yaani haifunui chochote kuhusu wakati uliopita, uliopo na ujao tofauti na neno la hekima na neno la maarifa.. Karama za roho mtakatifu hushirikiana yaani karama ya neno la hekima na karama ya neno la maarifa zinaweza kufikishwa kwa mhusika kwa karama ya unabii. Tunaposikia unabii unaoelekeza matukio yajayo si tu kuwa tumesikia unabii bali pia tumesikia neno la hekima na maarifa lililofikishwa kwetu kwa karama ya unabii.

MAAGIZO KUHUSU KARAMA ZA UFUNUO/NGUVU (unabii, neno la hekima/maarifa/aina za lugha/uponyaji)
Paulo alitoa maagizo machache kuhusu hizi karama kama ifuatavyo
1kor14:29-33..Kama ambavyo Korintho walivyokuwa wanatumiwa ktk karama ya kutafsiri lugha pia walikuwepo wenye karama ya unabii katika mafunuo. Hawakuwa manabii kama wale wa agano la kale au kama agano jipya kama Agabo (ona mdo11:28..21-10)Wao huduma zao zilikuwa za kanisani kwao TU..hivyo iliweza kuwepo zaid ya manabii watatu wa aina hiyo ktk kanisa moja sasa hapo ndipo Paulo aliweka mipaka ya huduma ya kinabii

Hii inaonyesha kwamba Roho alipokuwa anatoa karama ya Kiroho ktk kusanyiko mtu zaid ya mmoja angeweza kujitoa ili kupokea karama hizo..kama si hivyo mashauri ya Paulo yangeishia kwa Roho Mtakatifu kutoa karama ambazo zingefurahiwa na kusanyiko lote, maana lile kanisa iliwekwa idadi ya manabii waliokuwa na ruhusa ya kusema..kama wangekuwepo manabii zaid ya watatu wale wengine japo wamezuiwa kusema wangesaidia katika kupambanua (au kupima) yaliyokuwa yakisemwa.
Paulo akasema kwamba hao manabii wote wangeweza/ruhusiwa kutabiri kwa zamu (ona 1kor14:31) na akasema kuwa roho za manabii HUWATII manabii wenzao (ona 1kor14:32)..Hii inaonyesha kuwa nabii anaweza kujizuia asimwingilie mwingine na kumkata kauli hata kama amepewa unabii au ufunuo na Mungu kwa ajili ya kusanyiko. Paulo aliposema kwa maana hiyo nyote mwaweza kuhutubu mmojammoja (1kor14:31) kumbuka alikuwa akisema kwa habari ya nabii aliyepokea unabii..sasa leo kuna watu wamepotosha maana ya maneno haya ya Paulo na kusema kuwa kila aaminiye anaweza kutabiri katika kusanyiko.. SIO KWELI..karama ya unabii sio kwa kila mtu bali ni Roho Mtakatifu hutoa kama apendavyo yeye.
Siku za leo kanisa (mwili wa Kristo) linahitaji sana sana msaada wa Roho Mtakatifu na nguvu zake na karama zake..Paulo anasema takeni sana karama za Rohoni lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu (1kor14...) basi mtumishi afanyaye watu kuwa wanafunzi na anayetamani kutumiwa na Mungu kwa ajili ya utukufu wake atamani mno karama za Kiroho na udhihirisho wake
MUNGU AWAJAZENI KILA MNACHOKIHITAJI KWA KADIRI YA WINGI WA FADHILI ZAKE KAMA APENDDVYO.. AMEN!.

Comments