KUOKOKA NA KUONGOKA.


Watu wengi huniuliza tofauti ya KUOKOKA na KUONGOKA.
hebu karibu ujifunze na uwasaidie na wengine.

1. Kuokoka/Wokovu
Ni kupokea rohoni mambo makuu matatu yaani;
=Msamaha wa dhambi,
=Utakaso,
=kuhesabiwa haki
Yote haya matatu hufanyika Mbele za MUNGU kwa imani katika KRISTO YESU pekee.

2. Kuongoka (Proselytised)
Ni badiliko la mwanadamu kutoka kutotokuwa na msimamo wa kiimani, na kuamua kuifuata imani nyingine.
Mfano;
Kutoka uislamu kwenda ukristo.
Kutoka uyahudi kwenda ukristo.
kwa hiyo kuokoka ni jambo la muhimu zaidi maana ndilo jambo la ukakika wa uzima.

Kwa maana nyingine napenda niseme hivi.
JE KUNA TOFAUTI GANI KATI YA
KUONGOKA NA KUOKOKA ?
MAJIBU ;
Kuongoka ni kugeuka kwa mwenendo wako
wa kwanza na kufuta mwenendo mpya
baada ya kusikia neno la Mungu.
Tofauti kati ya kuongoka na kuokoka ni hii;
• Kuongoka sio NEEMA ya Mungu kwa yule
aliyeongoka,Bali ni jitihada zake pindi
anapoukulia wokovu. Baada ya kuokoka.
• Bali Kuokoka ni KIPAWA/NEEMA ya
Mungu mwenyewe kwa watu wake, Hapa
tunasoma Waefeso 2 : 8-9
“ Kwa maana mmeokolewa kwa neema,
kwa njia ya imani; ambayo hiyo
haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha
Mungu;
wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije
akajisifu. ”

Mwanadamu Anatakiwa Kuokoka Lini?
Akiwa hai si baada ya kufa, kwani baada ya kufa mtu ni hukumu si wokovu tena. (Ebr 9:27; 2Kor. 6:2)
Mwanadamu wakati wake wa kupokea mambo matatu muhimu kwa wokovu yaliyotajwa hapo juu; yaani msamaha
wa dhambi, ondoleo la dhambi, na kuhesabiwa haki ni wakati akiwa hai, na si baada ya kufa. (2Kor 6:1-2)

-Kuokoka Au Kutookoka Ni uamuzi na Uchaguzi wa mwanadamu mwenyewe na sio MUNGU, Ni hiari yako kuokoka au kukaa kuokoka lakini ni hasara kuu kwa anayekataa kuokoka.
Faida Za Kuokoka.
Zipo faida nyingi sana, zisizohesabika, bali hizi ni baadhi tu kati yake!
a) Kukombolewa, yaani Kulipiwa deni (Kufutiwa mashitaka) ili kuondolewa chini ya kongwa la utumwa wa shetani
na dhambi. (Kol. 2:12-15)
b) Kuhamishwa kutoka utumwa wa shetani na kuingizwa katika ufalme wa MUNGU, ndiyo maana BWANA YESU
alianza mahubiri yake kwa neno hili “Tubuni na kuiamini Injili…”(Mt
c) Kuzaliwa Upya kiroho, yaani kuzaliwa mara ya pili; ili kufanyika Mwana wa MUNGU na kuwa kiumbe kipya.
(Yoh.1:12,13; 2Kor. 5:17)
d) Kutumikiwa na Malaika wa MUNGU; (Ebr.1:13,14)
e) Kulindwa na nguvu za MUNGU kwa njia ya imani. (1Pet. 1:3-5; Zab.34:7)
f) Kupewa ahadi ya BABA, yaani ROHO MTAKATIFU na Ujazo (kutawaliwa/kuongozwa) wa ROHO MTAKATIFU.(Mdo.2:37-
40 )

Hatari Za Kutokuokoka.
Zipo hatari/hasara nyingi sana, zisizohesabika, bali hizi ni baadhi tu kati yake!
a) Kuwa mtumwa wa dhambi na wa shetani.
b) Kushindwa kuacha dhambi, kuwa mwenye dhambi, na kufa na dhambi.
c) Kutokuzaliwa Mara ya pili.
d) Kukosa ulinzi wa nguvu za MUNGU.
e) Kuwa mwana wa Ibilisi/Shetani.
f) Kusumbuliwa na mapepo na mashetani.
g) Kuikosa ahadi ya MUNGU BABA (Kumkosa ROHO MTAKATIFU)
h) Kulaaniwa maishani-milele.
i) Kufutwa jina katika kitabu cha uzima wa milele.
j) Kutokusikilizwa na kutokujibiwa maombi mbele za MUNGU.
k) Kuukosa Urithi wa Uzima wa milele.
l) Kutupwa katika ziwa liwakalo moto wa kiberiti (Moto wa milele, au Jehanamu).
m)m) Kuingia gizani kwenye kilio na kusaga meno milele.
Ndugu amua kuokoka leo na BWANA YESU atakupokea.
Ubarikiwe.

Comments