KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO?” SEHEMU YA 11

Na Abel Suleiman Shiriwa.
Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA.
Kwa sehemu ya 4 FUNGUA HAPA
Na kwa sehemu ya 5 FUNGUA HAPA na sehemu ya 7 ni FUNGUA HAPA
iLIPOISHIA: Nikastukia nimepigwa kofi Paaaaa, Niliinuka pale Nikakunja ngumi, nikasema, wewe mpumbavu huwezi kunipga kofi kwa habari zako kijinga hizo, nikapige dufu, kwani umeambiwa me ni Musilamu?
Wakati naongea hayo, kumbe mama alinisikia, akafungua mlango wa chumbani, akatukuta mimi na Mzee (kaka) Naomba pia hapa nieleweke kuwa, ninaposema mzee sina maana baba mzazi, bali ni kaka yangu, jina lake anaitwa mzee, mama akasema, ‘Mnataka kupigana ndani ya mwezi wa ramadhani kulikoni? Halafu wewe Aboubakar huyo si ni kaka yako, inakuwaje unamkunjia ngumi? Nikakwambia, “Sasa yeye atanipigaje kofi, kwani ni lazima me kwenda kupiga dufu?” Mama akasema, nimekusikia, unasema, kwani wewe muislamu, ina maana wewe siyo muislamu?”” Nikamwambia, “Ni usingizi, maana mzee kanikurupusha kutoka usingizini, sasa aliponipiga lile kofi, akili yangu ikawa kama imepooza, badala ya kumwambia, Kwani me mtoto mdogo mpaka unipige kofi, nikajikuta nimeropoka kuwa kwani me ni muislamu?” Akasema, “Haya toka huko ujiandae muondoke” Nikamjibu kuwa, “Siwezi kwenda huko, kwani hapa nimeshakwazika, tusije tukapigana huko, ikawa aibu, waache wenyewe tu waende, basi ikawa njia yangu hiyo ya kukwepa kwenda kwenye dufu.
Wao wakaondoka zao, mimi nikajilalia zangu, baadae nikasema, nikisema niwaambie sasa hivi kama nilivyopanga, itakuwa shida, ngoja tu nitulie kwanza, nikija kuonana na Kina Ernest, nitawaambia wanisaidie katika hili, maana nami nikataka niwe nahubiri kama wao, ila tu nikawa sina njia ya kuwapata kwa sababu sikuwa na simu wakati huo, basi mwezi wa Ramadhani ukamalizika. siku moja nikiwa na bro aitwae Juma, tumetoka kukoboa na kusaga mahindi, kule Kariakoo (MWANZA) maana Mwanza napo kuna kariakoo kubwa na ndogo, kama unaelekea Kilimahewa, ukitoka green view, kwa juu kama unaelekea Mkudi.
Wakati tumeshika mfuko wa unga huku na huku, njiani nikakutana na Ernest, akaniambia, ‘We Aboubakari vipi?” Nikastuka, nikamwambia “Pouwa” Akaniambia, “Nilikuwa nakutafuta sana, nataka twende Ukerewe tukahubiri” Nikaona hapa sasa kunataka kusanuka, maana bro Juma anamjua Ernest kuwa ni Muhubiri wa Kikristo, sasa hivi anavyosema kwamba, anataka twende Ukerewe ili tukahubiri, si atakuwa ameshaharibu, maana Juma anajua me bado muislamu, kimoyo moyo nikawa naomba asije kutaja neno kuokolewa kwangu, Nikaamua kuwahi kabla hajaongea mengi, Nikamwambia “Sawa nitakutafuta, maana hapa nipo fasta kidogo, nipo na brother, halafu nikamuoneshea Ishara ya kumkonyeza ajue kuwa hali si shwari” Natumaini kuwa alinielewa, akasema “Sawa Aboubakari” tukaondoka zetu, Njiani Bro akaniuliza, ‘Yule pale si ni kafiri wa Simbaulanga, sasa imekuwaje tena akuambie uende Ukerewe ukahubiri?” Nikacheka Nikamwambia, “Kaka nawe bhana, ina maana hujui kuwa wale jamaa wakihubiri peke yao huwa hawana mvuto kwa watu, ndiyo maana anataka mimi niende pamoja nae huko Ukerewe, ili nikamchangamshe kwa maswali, si unajua tena Bila maswali hawapati changamoto, halafu pia hawajui kuwa mimi nikienda kule Watasilimu Wakristo kibao”Akasema, “Sawa nimekuelewa” Tukaenda mpaka home, moyoni mwangu, natamani nirudi kule nikamtafute Ernest, maana niliposikia kuna safari ya kwenda Ukerewe, nikajua bila shaka lazima, nitakuwa nimepata mpenyo mzuri wa kuwa huru hata kwenda church, sasa nikawa najiuliza, nitampaje tena? Kwake sipajui, nitafanyaje? Nikakosa majibu…………..
‘KABLA SIJAENDELEA NA USHUHUDA, NGOJA NISEME BAADHI YA MAMBO AMBAYO NIMEYAPATA KUYAJUA KWA UNDANI WAKE BAAADA YA KUWA MKRISTO’
Wakati nipo kwenye uislamu, wakati wa kuswali, katika ile Tashahudi kubwa, ambayo ndiyo hitimisho la swala, nilikuwa nikisalimia, kulia na malizia kushoto, Hiyo inaitwa, (Taslamatan) Salamu mbili, na hiyo ni nguzo ya mwisho ya swala, ambapo unasema, Assalaam Aleykum WaLrahmatu Lllah, (Amani ya Allah iwe juu yenu) hata kama niko peke yangu, ni lazima nisalimie hivyo, sasa nikawa najiuliza, namsalimia nani wakati niko peke yangu? Baadhi ya Maustadhi, walinifundisha kuwa, tunawasalimia, malaika, na kumbe ni Malaika pamoja na Majini, Nilipokuja kukisosma Kitabu cha IRSHADUL MUSLIMIIN Ule Ukurasa wake wa 9 Nikagundua kuwa, kumbe majini nayo huwa tunayasalimia ndiyo maana hata kama mtu una sawali peke yako, ni lazima pia usalimie hivyo, pia kupitia ushirikiano wa Uislamu na majini, nikaja kugundua siri kubwa, ambayo ukiwa katika uislamu huwezi kuijua, mpaka uwe umetoka humo, ndipo utaweza kufahamu jambo hilo.
Ni Kuhusiana na Issa Bin Maryam, kufananishwa na YESU, Kiburi chote cha Waislamu, kukataa kuwa Wakristo, wakiamini kuwa, hata Yesu nae pia yumo kwenye Uislamu, akimtaja Issa bin Mariamu, wakisema wao sifa yao ni kuwaamini Mitume na Manabii wote, ukiwaulza mitume gani? Wanakutajia
Adamu
Nuhu
Ibrahimu
Luti
Is-haqa (Isaka)
Ismaili (Ishamel)
Yaqubu (Yakobo)
Tusufu
Yunusi Yona)
Ilyasi (Eliya?
Musa
Haroun (Haruni)
Daudi
Suleimani (Sulemani)
Zakaria
Yahya (Yohana)
Issa (ambae wanadhani ndiye Yesu)

Hawa ni watu ambao katika Biblia wameelezwa kwa mapana, sasa Muhammad katika kuanzisha kwake Imani ya Kiislamu mwaka wa 610, akaamua kutangaza kuwa hao wote walikuwa waislamu, (maana anajua wameshalala mautini) Hawana uwezo wa kuamka na kukanusha, japo kuwa kwa mujibu wa Biblia, katika hao wote hakuna hata mmoja ambae aliwahi kuwa muislamu, (Nitakuja kueleza utofauti wa hao kwa mujibu wa Biblia na quran) Ili uone utofauti ulivyo, ila kwa mtu ambae si msomaji, anaweza akadhani kwamba waliotajwa ndani ya Biblia, basi kwa uhalisia wake pia wametajwa na kwenye Quran, kitu amabacho sicho, siku nitakapoelezea utaweza kunielewa, maana kuna wengine humo siyo mitume wala siyo manabii, Ila Quran imewaita Mitume na Mnabii. Nikirejea kwenye Pointi yangu ya msingi, kuwa, Kupitia uhusiano wa waislamu na majini, niliweza kutambua hila ambayo aliifanya Mhammad, kwa kumfananisha Issa na Yesu, yaani ni sawa na fedha bandia, ambayo hufananishwa na fedha halali, kama si mchunguzi unabambikiwa fedha hiyo mbadia ukadhani ni Fedha halali, kama alivyosema Mtume Paulo.
2 Korintho 11:14 Wala si ajabu. Maana Shetani
mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa
nuru.

15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao
wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki,
ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi
zao.

Kitendo cha shetani kujigeuza na kuwa mfano wa malaika wa Nuru, haina ugumu pia kwa watumishi wake nao pia kujigeuza na kuwa mfano a watumishi wa haki, Naomba ieleweke kuwa kwa mujibu wa uislamu, shetani hajawahi kuwa malaika, wala majini siyo malaika, Dhana ambayo imewafanya waislamu wengi wapofuke macho yao ya rohoni washindwe kutambua kuwa hawa Majini (mpepo) ni malaika walioasi na kutupwa hapa duniani, wakisuboro siku ya hukumu,
Ufunuo 12: 7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.

Ibilisi huyu baada ya kutupwa hapa duniani yeye pamoja na malaika zake, (Majini) alishuka akiwa na ghadhabu nyingi sana, sasa hasira zao za kufukuzwa huko mbinguni, wakazihamishia kwa wanadamu, na kutaka kuwapoteza ili waweze kuingia nao motoni, moto ambao umeandaliwa special kwa ajili ya Ibilisi na malaika zake (majini)
Mathayo 25:41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.
Sasa shetani kwa kutaka watu wasijue kuwa yeye ni malaika aliye asi, Mwaka wa 610 baada ya Kristo, akaanza kuwatuminisha watu kuwa, sifa ya Malaika hawezi kumuasi Mwenyezi Mungu, kwa kupitia aya hii ya Quran.
Quran 66: 6. Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Allah kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.
Kwa hivyo wakati bado nipo kwenye uislamu niliamini hiyo kama ambavyo ndugu zangu waliomo katika uislamu wanaamini sifa ya malaika ni kutokuasi, bila kujua hao majini ambao huwasalimia wakati wa swala ndiyo malaika walioasi, ambao wapo hapa duniani kifungoni.
Yuda 1:6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
Hapa kwenye makao yaliyo wahusu, makao hayo ni mbinguni, ambako hapo kwenye Ufunuo 12:7-9 Tumeona walifukuzwa, baada ya kuondolewa, tukaambiwa, makao yao hayakuonekana tena Mbinguni, ni sawa na samaki ukimtoa nje ya maji, na kumweka nchi kavu, maana yake umemtoa kwenye makao ambayo yanamuhusu na kumweka kwenye makao yasiyo muhusu kwa maana hiyo unakuwa umweka kwenye mateso ya kumwangamiza, ndivyo ilivyokuwa kwa majini, Hapa duniani, ni sehemu ambayo wao hawakustahili kukaa, ili kujua hivyo, hata kwenye quran yalisema kuwa yalitaka kurudi Mbinguni, lakini yakakutana na ulinzi mkali..
Quran 72:8. Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.
Ulinzi huo ambao waliukuta, ambao uliwafanya washindwe kurejea Mbinguni, Biblia ulishasema zamani hata kabla majini hayajaongea kupitia Quran.
2 Petro 2:4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
Kwa hivyo mbingu zina ulinzi majini hayawezi kurudi kule milango yao ya toba imekwisha kufungwa,, hapo yalipo yanajua kuwa, yenyewe yanasubiri moto, katika kuwapumbaza watu, ni sharti lao kusema, Majini siyo malaika walio asi, ili watu wajue kuna tofauti baina ya majini na malaika walioasi, ila yenyewe yanajua hivyo, na pia yanajua siku ya mwisho lazima yatupwe motoni, kwani ujio wa Yesu, uliwaumiza sana, walijua kuwa Yesu, amekuja kuwatesa kabla ya Muhula wao, kama ambavyo yalijileza hapa.
Mathayo 8:28 Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.
29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?
Majini (malaika walioasi) Wanajua Muhula wao wa kuteswa upo, na ambae atawatesa, ni Yesu, kwa hivyo wakawa wanashangaa imekuwaje Yesu, awahi kuja kabla ya Muhula wao ambao amewekewa kabla ya mateso? Hawakujua kuwa Ujio uo wa Yesu kwa wakati huo, ulikuwa ni kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu kutoka na vifungo vya hayo majini, sasa majini kwa kujua kuwa, yenyewe, hayana nafasi katka ufalme wa Mungu, yakawa yanatafuta nafasi kwa Yesu, angalau yaweze kupata nafasi, kwa kumuita Mwana wa Mungu, lakini yakagonga Mwamba, kama maandiko yasemavyo.
Marko 11:11 Na pepo wachafu, kila walipomwona, walianguka mbele yake, wakalia wakisema, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.
12 Akawakataza sana, wasimdhihirishe.

Ni majini tu ndiyo ambayo hayakuruhusiwa kumuita Yesu, mwana wa Mungu, kwa maana wao ni wachafu,na hawana nafasi ya kutubu, lakini mwanadamu, mwenye nafasi ya Kutubu, yeye anayo ruhusa ya kumuita Yesu Mwana wa Mungu.
Yohana 9:35 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?
36 Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?
37 Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye.
38 Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia.

Majini baada ya kuwa yamekosa nafasi kwa Yesu, yakaamua yatafute namna ya kuwapoteza zaidi watu, ndipo huo mwaka wa 610 baada ya Kristo, yakafanikiwa, kwani alipokuja Muhammad, yakaona ndo nafasi yao hasa, kutangaza Yesu siyo Mwana wa Mungu, kwa sababu kule yamekatazwa
1. Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!
2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.
3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana
Baada ya kuiamini tu, hapo hapo yakaanza kutangaza kua, Mola wao hana mwana, kwa hivyo yo yote mwenye kuifuata Quran ni lazima akiri kuwa, Mola wa majini, hana Mwana,, baada ya hapo yakasilimu na kuwa maislamu.
Quran 72:14. Na hakika wamo katika sisi (Majini) Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu,
Kazi yao baada ya kusilimu, ikawa ni kutangaza na kueneza Uislamu, na kuufundisha Uislamu.
UKISOMA KITABU KINACHOITWA, ASILI YA
MAJINI NA VITIMBI VYAO NA NAMNA YA
KUJILINDA DHIDI YAO,
KILICHO ANDIKWA NA DR, AHAMAD H. SAKR,
NA KUFASIRIWA NA ABU JA’FAR CHIFU,
NA KUCHAPISHWA NA KAUTHAR PRINTERS
ULE UKURASA WA 118 KINASEMA.

S 24. Je, majini huwa wanatoa Da’awa kwa ajili
ya kueneza uislamu?
J 24. “Ndiyo majini wanao Da’iyah wanaoeneza
na kufundisha ujumbe ulio teremshwa kwa
mtume Muhammad, ambao ni Dini ya Kiislamu.
Katika sehemu mbili za Quran Allah
anatufahamisha kuhusu Da’iyah wa kijini, hizo ni
Surah Al-Ahqaf na Surah Al-Jinn”
Na kweli yalianza kwenda kwa watu wao kuwaringania waweze kusilimu wawe waislamu

29. Na wakati tulipo waleta kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur'ani. Basi walipo ihudhuria walisema: Sikilizeni! Na ilipo kwisha somwa, walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya.
30. Wakasema: Enyi kaumu yetu! Sisi tumesikia Kitabu kilicho teremshwa baada ya Musa, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake, na kinacho ongoza kwenye Haki na kwenye Njia Iliyo Nyooka
Majini yakaanza na uongo kwa kusema, eti Quran imekuja baada ya Musa, wakati, Zaburi ilifuata baada ya Mussa kwa imani ya mafundisho yao, Tukiendelea na hoja yetu, ya sababu ya Issa kufananishwa na Yesu, majini haya baaa ya kuanza kueneza Uislamu, pia yakatoa msimamo kuwa, ndani ya Msikiti wa kutajwa ni Allah tu
Quran 72:
18. Na hakika misikiti ni ya Allah basi msimuabudu yeyote pamoja na Allah,

Kwa hivyo mle msikitini, hakuhitaji atajwe Yesu, ila Allah, Katika namna ya kuyalinda majini, Muhammad akaamua kuchukua jina la Isa, la kumnasibisha, na Yesu, fuatilia Khutuba siku ya Ijumaa Msikitini, huwezi kusikia wakisema, Yesu, bali watasema, Issa Ibn Maryam, kwa sababu gani? Ni kwa sababu Majini yamo msikitini, Jina la Yesu, ni moto kwa majini, maana ndilo jina pekee lenye uwezo wa kuyatimua hayo majini.
Marko 16: 17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
Kwa hivyo Wakilitaja Jina Yesu kwa uwingi ndani ya Msikiti, basi itakuwa ni Purukushani kwa majini, maana watakuwa wanawatesa ndugu zao wa kijini, kwani kila jina la Yesu litajwapo, ni shida kwao, mfano mzuri watu wenye mapepo wajapo kanisani, huombewa na kuyatimua, maana mle siyo mahali pake, sehemu yao ni msikitini, Kwa hivyo Muhammad akawafundisha Waislamu, kuwa Yesu ni Issa Bin maraya, wakati Issa Tafsiri yake, ni wekundu ambao umezidiana na weupe, (ALBINO) na Yesu, Tafsiri yake, Mungu, anaokoa, au Bwana ni Mwokozi, hivyo uliitapo jina la Issa, halina athari hata chembe kwa majini, ila la Yesu, hapo patachimbika, HIYO NDIYO SABABU KUBWA SANA, ya Issa kufananishwa na Yesu, Ili kuyanusuru majini msikitini, nimekuja kuelewa, baada ya kuwa Mkristo, ila kipindi bado nipo kule, nilikuwa sijui cho chote kuhusu hilo, nilijua Issa ndiye Yesu, na Yesu ndiye Issa, kumbe hamna maana Yesu Kiarbu hitwi Issa, bali Yasu’u (Mungu anaokoa) TURUDI KWENYE USHUHUDA SASA baada ya tafakari hiyo ki ufupi.
Nikawa na shauku sana ya kumuona Ernest Ili twende Ukerewe,ila nikajipa moyo kuwa, ipo siku nitamuona, Baada kama siku 3 Nikaamua niende pale Kanisa la Batpist Kona ya Bwiru, kwa Mchungaji Madereke, nikawaulize namna ambavyo naweza kumpata Ernest, nafika pale, nikakutana na Hassan Issa Kalenga, (Yule alie tangulia kuwa Mkristo kabla yangu) ambae niliapa siku ile ambayo alikuwa anaritadi kuwa,, siku nikimuona nitamchoma kisu, akashangaa sana kuniona, akaniambia, “Hongera kwa kuungana nami katika safari ya kwenda mbinguni” Nikamwambia, “Ahsante, Ila una bahati kweli, maana kama tungeonana kabla ya mimi kumpokea Yesu, hakika dhamira yangu ya kukuchoma kisu, huenda ingetimia maana nilikuwa na hasira nawe sana” Akasema, “Ni Mungu tu ndiye hakupanga tuonane nawe, ila leo imewezekana” Akaniambia kuwa, Ernest alimwagiza anitafute twende Ukerewe, akasema, “kwani Ernest na Mjuni wao tayari wameshatangulia wameniambia nikutafute ili twende wote, sasa me kwenu sipajui”, Nikamwambia “Twende ukapajue” Kweli nikampeleka, akapaona, ila tu hakuingia ndani.
Nikamsindikiza, huku tukipanga namna ya kwenda Ukerewe, nikawambia, basi atakapokuwa, yuko tayari, basi aje anistue, Halafu nikamuuliza, “Unaishi wapi” Akasema, anaishi kwa Mchungaji Maderke, tukaagana, me nikaondoka zangu kurudi home, baada ya siku mbili,nikiwa ndani, nikaja kuitwa, kutoka nje, namkuta Hassan, Sikutaka kumkaribisha ndani, maana wangenishitukia, pengine inawezekana wakawa wameshasikia habari zake, Nikamwambia “Vipi?” akasema, “Safi, Ebhana eeh Safari imeiva twende zetu Ukerewe” Nikamuuliza, “Nauli unayo?” Akasema, “Hapa nina 2500 tu” Nikamuuliza “Nauli bei gani?” Akasema,”Tsh 350”n Ukijumulisha na Dalala, itakuwa 3800 Bado kula, Nikamwambia, “Mimi hapa sina hata 100, akasema, ‘Twende Kwa Mchungaji Madereke tukamuombe Nauli” Ilikuwa ni siku ya Jumanne, Tukaondoka mpaka Kona ya Bwiru, tukamuona Mchungaji Madereke na kumweleza shida yetu, akasema, tumemkuta hayuko vizuri kifedha, tusubiri siku ya Jumapili atufanye changizo, Tukamwambia ngoja tukafanye mchakato sehemu nyingine, kama tutakwama, basi tutakuja hiyo Jumapili,
Tulipotoka pale, nikamwambia Hassan, nimepata Wazo, twende home, wewe utanisubiri nyumba ya Jirani, mimi nikaongee na mama nimpange ili anipe Nauli tuweze kwenda Ukerewe, akasema, “Atakupaje Hela ya kwenda Kuhubiri Injili?” Nikawambia Nitamwambia, naenda kufanya Da’awa ya Kiislamu, kwa hivyo atanipata tu, maana anapenda sana” Tukaondoka zetu mpaka Home, Yeye akabaki kama nilivyomwambia, mimi Nikaingia ndani na kumkuta Mama, anasoma Quran, nikamsalimia, kisha nikamwambia nina shida, Akaniuliza “SHIDA GANI?” Nikamwambia, “Wale Makafiri kina SIMBAULANGA, nimeambiwa kuwa, wapo Ukerewe, sasa kule wanawaritadisha sana waislamu, (Kuwatoa kwenye uislamu na kuwafanya kuwa Wakristo) kwa sababu hawana uwezo wa kujenga hoja,wanapobanwa kidogo tu wanaritadi, sasa kuna muislamu mmoja alishawahi kunishuhudia nikijadiliana nao, aliponiona, akaniomba sana twende” Akasema, “Umemuonea api?” nikawambia, wakati nimetoka hapa, yule jamaa aliyekuja kuniita, ndiye aiyetumwa nae, ila nauli ndo sina” Akasema, Nenda ukamuite huyo ambae anataka mwende nae Ukerewe, Ili niongee nae, Nauli nitakupa, maana siwezi kukuruhusu uondoke, bila mimi kujua wapi uendako, na nani unaenda nae” Nikawambia, sawa, Nikatoka Nimepowa, nikijisemea, “Huu sasa mtihani, nitampata nani? muislamu gani nitamuendea nimwambie ajifanye ndiyo yeye halafu akubali?” Nimeshaona milango ya mimi kuwa huru kiimani umeshawadia, maana kupitia safari hiyo, nitafanikiwa, sasa hili la kumtafuta huyo mtu, linataka kunikwamisha, Nikamfuata Hassan nikamweleza, akasema, kweli mtihani huu, na safari yenyewe ni leo, akasema, kuna jamaa yangu mmoja hivi twende tukaongee nae, tumwambie ajifanye ni Muislamu, ndiye ambae utaenda nae, Nikasema, ni Wazo zuri, na kweli, tukamfuata tukamkuta, tukamweleza hali halisi, akakubali ila akasema, mimi sijui cho chote kuhusu Ukerewe, wala kuhusu Uislamu, me nikamwambia, hutoulizwa sana, cha msingi wewe ukifika pale, Salimia, ‘Assalaam Alyekum” Akasema, sawa, hao tukaondoka zetu, Hassan tukamwacha nyumba ya jirani ameketi kwenye msingi, sisi tukaingia ndani, na yule Yule mpendwa, tulivyoingia ndani, nikamkuta Ustadhi, BASHRI, ambae alinifundisha Thaqaafa, amekaa anaongea na mama, yule mpendwa akasalimia, bada ya Kusema, Assalaam Aleykum, yeye akasema, “Salama leko” moyo ukalipuka, Paaaa, Salama leko tena? Mama Mama na Ustadhi hawakuitikia, waamtazama kwa mshangao, Nikasema, kimeshasanuka, wakianza kumuuliza maswali kuhusu Uislamu, Mkristo huyu atajibu nini huu si ndo mwanzo wa kuumbuka?........... UTAENDELEA
Usikose sehemu ya 12 ya Ushuhuda huu ujue kama nilifanikiwa Kwenda Ukerewe ama Laa….

Comments