ABEL SULEIMAN:KWA NINI NILIAMUA KUAC HANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO? SEHEMU YA 4

Na Abel Suleiman Shiriwa.


Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA
Baada ya kuona Iddy amezidiwa kwa hoja, nikaawaita waislamu pembeni, nikawauliza, “Tufanyaje maana hapa tumeshaaibika, maana kama huyu Muhadhiri mkubwa kama huyu ameweza kubanwa kiasi hiki, sisi tutawaweza kweli hawa Makafiri”? MMOJA AKASEMA, “Dawa yao hawa ni kuanzisha fujo ili Mkutano wao uweze kufungwa, me nikasema, “Sio busara kufanya fujo, maana sisi waislamu tulipofanya mihadhara mbona wao hawakufanya fujo, sasa ni vipi sisi tuwafanyie vurugu? Hapa cha msingi, tuanze tu kuzomea, na kupiga kele, huku tukimshangilia IDDY, na kisha tumanyanyue pale tumbebe kama shujaa, huku tukipiga TAKBIRA Ili kuficha aibu hii” Wakasema sawa, basi tukarejea tukaanza kupiga kelele, na kuzomea, kuna mzee mmoja alikuwa amekaa karibu na Meza ya msomaji, tukamuona anatetemeka, tukaingia mezani tukamchukua IDDY kwa kumbeba huku tukipiga Takbira, tukapanda nae, mpaka barabarani karibu na shule ya Msingi Mwenge, kwa jamaa wachonga masofa, tukamwambia, “Imekuwaje mpaka uburuzwe kiasi hicho”? akasema, “Makafiri wale maandiko wanayapindisha” Tukamuuliza “Wanayapindisha vipi wakati maandiko yamesomwa na kila mtu amesikia”? Tukamwamia wewe kubali kuwa umechemka, ni kheri waitwe tu kina Mazinge, maana hao ndo tulikuwa na imani nao sana kuliko Wahadhiri wengine, baada ya hayo tuakatawanyika, me mdogo mdogo mpaka Ghana, pale Taqwa, Nikaingia Masjid, na kushika udhu, kisha nikazama ndani na kuswali rakaa mbili za Suna, na kukaa nikisubiri Swala ya Magharibi, KICHWANI mwangu, nikajiuliza, “Hivi wale Makafiri, Quran wamejifunzia wapi?” Muadhini akaadhini, tukaswali, nikatoka nikaenda zangu home nikiwa sina raha, maana niliumia sana, Kesho yake sikwenda school, mida ya saa 4 nikaingia town mpaka Msikiti wa Ijumaa, nikaulize kama kuna uwezakano wa Kina Mazinge kuja.
Nilipofika Msikiti Nikapanda ngazi kwenda mpaka kwenye ofisi ya Sheikh Jabiri Katura, sikumkuta, nikashuka nikaingia msikitini, nikachukua quran nikaanza kujisomea, ili nivute muda wa Swala ya Adhuhuri, maana muda huo patakuwa na wana harakati wengi, na kweli, baada ya swala hiyo, tukaambiwa tusiondoke, akasimama Issa Kalenga, na kutangaza kuwa, “Watukufu waislamu, wale Makafiri wa Dar es Salaam, wameingia tayari hapa Mwanza, kwa hivyo tukiwaacha tu hivi hivi, basi uislamu utakuwa matatani hapa Mwanza, maana wale jamaa wanakufuru sana, kwa hivyo tunahitaji mchango kwa ajili ya kuwaita wenzetu kutoka Dar, Ili waje kuongeza nguvu ya kukabiliana nao” Watu wakatoa zao hela, me sikutoa maana sikuwa na fedha, Mwishoni akasema, Sisi Leo tutaenda Pale Mezani kuuliza maswali, tupo na Jamal Germanus, alikuwa padre huyu, kwa hivyo atatuwakilisha vema, Moyoni nikafurahi kweli, nikasema, afadhali, maana jana nilivyoumia, basi leo nitapata faraja, tukatoka msikitini, nikaenda kupanda gari, mpaka home, nikala, kisha nikaenda kumtafuta rafiki yangu, Ahmad, ili saa 10 twende zetu Furahisha, nikaenda kwao, sikumkuta, nikaambiwa, ameenda kucheza mpira, uwanja aliokuwa anachezea nilikuwa naujua, nikaendea, nikamkuta, nikakwambia, “Jana nilienda kwenye muhadhara, wa Makafiri, lakini waislamu tulizidiwa” Akashangaa, akaniambia, “Wakristo wameanza lini kufanya mihadhara, wakati wao huwa wanaitisha mikutano wanahubiri na kuwaombea watu wenye majini?’ Nikamwambia, “Hata mimi nimeshangaa, maana jana niliwasikia wakati nipo kwenye gari nikafika home nikaenda, ndo nikawakuta wao, wanasoma quran na Biblia kama Waislamu, halafu mezani kwao kuna lundo kubwa la vitabu vya kiislamu” Akasema, basi ngoja nivae Suruali twende zetu nami nikawaone. “Nikamwambia Poa, Changamka”
Hao tukaanenda zetu Uwanja wa Furahisha, ndo tukwakuta Wakristo wanamalizia kufunga zao vyombo, tukakaa kwenye nyasi tukisubiri waanze, baada ya kumaliza wakaanza kupeleka somo lao, Kila wakisoma Quran nilikuwa na nakASIRIKA, najiuliza, “Hawa jamaa wanashika kitabu cha Mnyazi mungu, sijui wanajanaba, au wametwaharika, baaadae tukawaona Wahadhiri wa kiislamu wanakuja, tukasimama kwa furaha, hao tukawafuata, Tukawasilimia, huku mimi nikiwa nafuraha kubwa kweli kumuona Padre aliyesilimu, nikajua leo Kanisa linaenda Kula mweleka, baada ya Muhubiri wa Kikristo kumaliza kufundisha somo la Yesu sio Isa, basi, wakaitwa mwenye maswali, Jamal, akaenda pale akakaa sisi tukawa nyuma yake, tukaambiwa turudi nyuma, ili meza iwe wazi tumuache msomaji na muuliza masawali peke yao. Hapo nilikuwa na usongo wa kuona kanisa jinsi ambavyo litaangukia Pua, tukasogea pembeni, akapewa maiki akakaribishwa, na kisha akaulizwa, “Jina Lako nani”? AKAJIBU, “Jamal Germanus” dini yako?, akasema Quran 3:19, akaambiwaa we taja kwa mdomo ni dini gani kila mtu akusikie, haina haja ya kusema Quran 3:19 Akasema, “DINI YANGU NI ISLAMU” wakamwambia mambo si hayo bhana, haya tuambie ujio wako meza mezani ni nini au Umekuja Kumpa Yesu maisha yako baada ya kugundua kuwa Yesu sio Isa?” tumpe Mchungaji Maiki akuongoze Sala ya Toba Jamal akasema, “Mimi nilikuwa huko tena nilikuwa kafiri kuliko hata ninyi, kwa hivyo siwezi kuongozwa Sala ya Toba, na Mbwa” Waislamu tulilipuka kwa TAKBIIRA, Yaani Takbiiir, Allahu Akbaru, Akaulizwa, “Kwani wewe umeona hapa kuna Mbwa”? akasema, “Kwani hamjui kuwa Wachungaji wote ni Mbwa? SASA MNATAKA NIMPE Yesu maisha yangu kwa kuongozwa Sala ya Toba na Mbwa”? akaulizwa, kuna andiko lolote ambalo linasema kuwa Wachungaji wote ni Mbwa?” akashika maiki na kusema, “Waislamu Takabiir” Tukaitikia kwa sauti kubwa, “Allahu Akbaru” Akasema, oneni makafiri hawa, hawajui hata maandiko yao, wanauliza kama kuna andiko lisemalo kuwa Wachungaji wote ni Mbwa” AKASEMA, “Msomaji, hebu soma Isaya 56:10-11, Ikasomwa, nayo inasema.
Isaya 56: 10 Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.
11 Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.

Iliposomwa hapo, Waislamu acha tulipuke kwa Takbiir, Allahu Akbaru, Wakaristo waliokuwa wanasikiliza basi wakanywea, Sisi tukawa tunacheka, tunasema, andiko hilo hapo, kumbe Wachungaji ni Mbwa bhana, tukaanza kuwazomea mijibwa hiyo Mijibwa hiyo, Wuwuwuwuwu, Wakasema tulieni basi tuendelee na Mjadala, tukatulia, Jamal akaulizwa, “ Kwa hiyo kwa mujibu wa andiko hilo, kila anaeitwa Mchungaji ni Mbwa sawa”? Jamal akajibu, “Unauliza makofi Polisi, ndo maana yake, kila mchungaji ni DOG” wakamwambia, “Haya mpe maiki msomaji wetu” Msomaji akapewa Maiki, Muhubiri akasema, “Jamani limetolewa hapa andiko, kuhusu Wachungaji Mbwa, Jamal kasema, Kila anaeitwa Mchungaji ni Mbwa, haya msomaji wangu, hebu nisomee Quran 5:116 Suratul MAIDAH (SURA MEZA ILIYOANDALIWA CHAKULA)” andiko hilo likasomwa, nalo linasema.

Quran 5: 117. Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipo kuwa nao. Na ulipo nikamilisha muda wangu Wewe wewe ukawa Mchungaji juu yao. Na Wewe ni shahidi juu ya kila kitu.

Hiyo ni quran tafsiri yan sheikh Farsy, Basi iliposomwa, nikastuka kusikia kuwa kumbe hata Allah nae ni Mchunagi, basi, Jamal akapewa maiki, akaambiwa, “Wewe umesema kuwa kila mchungaji ni Mbwa, na quran imesema kuwa Allah ni Mchungaji, Je unakubali kuwa Allah mungu unae mwabudu ni Mbwa?” Jamal kushika maiki akawa mzito, basi Wakristo wakalipuka kwa makofi, huku wakisema, Yesu Yesu Yesu, Muhubiri akamwambia Jamal, “Mbona kigugumizi?” wewe umesema wachungaji wote ni Mbwa, sasa unakubali kuwa Allah ni Mbwa maana nae ni mchungaji?” akawa anasitasita kujibu, basi huku sisi tukanywea kabisa, Yule Muhubiri akamwambia msomaji, ngoja tuongeze aya nyingine, soma Quran 2:104” Akasoma, nayo inasema.
Quran 2:104. Enyi mlio amini! Msiseme: "Raa'ina", na semeni: "Ndhurna". Na sikieni! (amri) Na makafiri watapata adhabu inayoumiza,
Kisha akaambiwa msomaji asome ufafanuzi wa aya hiyo katika Tafsiri hiyo ya sheikh Abdulla Saleh Farsy, ufafanuzi ukasomwa, nao unasema.
2:104 Waislamu walikuwa wakati mwingine wakimwambia Mtume “Raa inaa” (Yaani kuwa ukituchunga kama mchungaji mzuri anavyochunga wanyama wake, kwani sisi waislamu ni wajinga, hatujui la madhara wala la maslaha)…. Msomaji akaambiwa, mpe Maiki Jamal, aliposhika Maiki, akaammbiwa, “ Haya, Tumemuona mchungaji wa pili huyo anaitwa Muhammad, nawe umesema kuwa kila mchungaji ni Mbwa, sasa unakubali kuwa Muhammad ni Jibwa?” Hapo kibao cha kusangilia kimegeuka, mwanzo tulikuwa sisi wakati huo ikawa zamu ya Wakristo, Jamal alibaki ameduwaa, mpaka nikajiuliza, Hawa jamaa ni wachawi nini? Mbona inakuwa hivyo? Jamal akasema, “ hao Wachungaji ni Wa kanisani, Basi hapo Wakristo wakacheka, huku wakishangilia, Muhubiri akamwambia, “Wewe mwanzo si ulisema kuwa kila mchungaji ni mbwa, sasa imekuwaje tena umegeuka? Tena sifa hizo za I SAYA 56:1-11 zinamwangukia Muhammad mmoja kwa moja, maana maandiko yametaja sifa za Mchungaji ili awe Mbwa,
1. Hawana Maarifa (Hawafahamu neno)
2. Wana Choyo sana.
3. Hawashibi

Muhubiri akamwambia Msomaji, tumeona Muhammad ni Mchungaji, sasa tumtazame kama sifa hizo tatu, kama anazo au hana, Akaambiwa asome Quran 7:157
157. Ambao kwamba wanamfuata Mtume, Nabii, asiyejua kusoma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa
Akasema, kwa mujibu andiko hili Muhammad, hana maarifa ya kusoma na kuandika, hiyo ni sifa moja ya Mchungaji Mbwa, kwa kuwa Sifa ya Mchungaji mbwa, ni kutokuwa na maarifa na kutolifahamu neno, na Muhammad ni Mchungaji, ambae hajui kusoma neno wala kuliandika, neno, huyo atakuwa nani?
Sifa ya pili, mchoyo, Ikasomwa quran 33:55
53. Enyi mlio amini! Msiingie nyumba za Nabii ila mpewe ruhusa kwenda kula, sio kungojea kiwive. Lakini mtakapo itwa basi ingieni, na mkisha kula tawanyikeni, wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii naye anakustahini, lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa jambo la haki. Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Wala haikufalieni kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu
Muhuburi akasema, hapa Muhamamd ameonyesha uchoyo wa hali ya juu, kwa kuwataka waislamu wenye njaa wasiende kwake, kupiga stori, ili chakula kiive, bali mpaka watakapopewa ruhusa, ina maana kama asipokuitwa nawe una njaa, basi huna ruhusa ya kula, na jambo la kukaa kusubiri Chakula kiive, ni jambo ambalo, linamkwaza Muhammad, kwa sifa hii ya Uchoyo, atakuwa nani?
Kisha kikasomwa kitabu cha Historia ya Mtume Muhammad kilichoandikwa na Mohammed RIDAY wa Mombasa Kenya, Uk wa 176, Paragraph ya 5 Kinasema,
“Mtume Muhammad alikuwa hali chakula, mpaka ashikwe na Njaa, na akila hashibi…..”
Muhubiri akauliza tena, kwa kuwa sifa ya ya tatu ya Mchungaji mbwa, ni kutokushiba, na Muhammad tumeambiwa alikuwa akila hashibi, kwa mujibu wa andiko hilo atakuwa nani? Msomaji akaambiwa ampe Microphone JAMAL, ili ajibu swali hilo, me nikasema, afadhali hata IDDY jana, kuliko leo, Wislamu tukaona hapa kumeshachafuka, Hapa Mtume (S.a.w) anaenda kutukanwa, Kabla JAMAL, hajasema chochote Waislamu tukavamia Ile Meza ya Maswali…….. UTAENDELEA KESHO.

Comments