MAMBO MUHIMU YA KUTAMBUA ILI SADAKA YAKO IKUBALIKE NA MBINGU (by Mremi) KWA NINI TUNATOA SADAKA?

Na Eliapenda Mremi.
Swali ambalo linasumbua watu wengi sana leo na yamkini wengine hawapata jibu ni kwa nini tunatoa sadaka? Na wengine huuliza je Mungu anazipokeaje hizi sadaka?..au kuna faida gani katika kutoa sadaka?
1)Kwanza ukimfahamu Mungu kwa undani utapata majibu ya maswal yoote hayo. Tatizo kubwa leo watu hatujataka kumfaham Mungu kwa kina.Ayubu22-21 inasema mjue sana Mungu ili uwe na Amani..hata Sulemani aliambiwa atafute kumjua Mungu kwanza (1nyak28-9)
Kwanza sadaka ni UTUMISHI, so unahitaji wewe binafsh kumjua Mungu ukiwa kama mtumishi..hata ukifuatilia watumishi waliomtumikia Mungu waliotutangulia utagundua hawakukwepa hii hatua ya kumjua Mungu..angalia akina Ibrahimu, Isaka, Musa, Daudi' Sulemani etc.
Hawa wote utagundua hatua ya kwanza kabisa hata kabla ya sadaka zao ilikuwa ni kumjua Mungu kwanza. Unapomjua Mungu kutoa sadaka hakukupi shida coz unakuwa unajua unayemtolea ni Mungu wala sio mwanadamu

KUTOKUMJUA MUNGU- Huu ndio ugonjwa mkubwa sana unaotafuna wengi leo na ndio umesababisha utoaji wa leo umekuwa kama ADHABU fulani hivi..yaani imekuwa kama zile za wakati ule wa torati masharti mashart na kukemeana kwingi...Tujitahidi kumjua Mungu kwa kumkaribisha Yesu Kristo maishani/moyoni ujazwe na Roho Mtakatifu uwe na maisha mapya ya kusoma neno na kukaa hemani mwa Bwana kama mfalme Daudi(zab27-4)
JIFUNZE KUMTII MUNGU.
Kilichomwangusha Adam na Hawa ni kutotii maagizo ya Mungu (mwanz3:17)
1samw15-22-23,..Huyu aliambiwa aangamize vyote hakutii..Ukiharibu neno la kutii ni shida hata sadaka yako kukubaliwa na Mungu

Fikiri Mungu anasema toa gari, wewe kwa kufunika hilo unapeleka laki moja..au Mungu anakusemesha toa kiwanja au nyumba, wewe unatafutia mmbadala wake kile kilicho kinyonge..Usije ukadhani Mungu ana shida na gari yako au nyumba yako..NO..anapima kiwango chako cha utii,..Ibrahimu alipitishwa ktk hiki kipimo kupitia mwanaye mpendwa wa pekee Isaka ila yeye alifaulu mtihani..wewe umefeli mara ngapi???
TOA SADAKA KWA UPENDO.
Math22-34...Upendo lazima uambatane na kutoa..Yoh3-16..Mungu aliupenda ulimwengu akamtoa mwanawe..so Kinachotuonesha kuwa Mungu aliupenda ulimwengu ni utoaji wake kwa hiyo Mungu ndiye mtoaji number one (yoh10-17)
Hata kijamii kama unasema unampenda mkeo/mumeo lazma ujitoe kwake..kwa vijana hapa ndo watanielewa vizuri..Upendo wa maneno matupu haujajitosheleza(yoh3:16-18)..Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa kupenda sio kulazimishwa au kuhimizwa.

JIFUNZE KUAMBATANISHA SADAKA YAKO NA MAOMBI
Watu wengi wanatoaga sadaka zao kimyakimya hawasemi neno..kumbuka hata wale wanaotoaga sadaka zao kwa waganga au wafu huwa wanazisemea maneno..sasa kama shetani anajua kuzisemea neno sadaka inakuwaje Wana wa Mungu leo tushindwe kuzisemea neno sadaka zetu na ikawa hivyo?
Ebu tuone mifano michache
Luka7-2-5..hao wazee waliambatanisha maombi na sadaka alizotoa yule akida
1samw1:10-11..Hana naye aliamua kuambatanisha maombi na sadaka na Bwana akafungua njia akapata hitaji la moyo wake.
Mdo10-1-2..(mdo9-36-43) Usiache sadaka yako iende kimyakimya.,.unaenda kanisani jumapili au jumamosi tenga sadaka isemee neno..kama huna cha kusema sema hata kwa ajili ya taifa lako..hata ukimwambia Mungu hivi,..Mungu natoa sadaka hii, ponya taifa langu, ondoa ajali katika taifa langu nk nk..semea hata ndugu zako au rafiki zako kama wewe huna tatizo ingawaje sidhani kama kuna mtu hana tatizo..kama wewe huna omba hata maombi ya akiba.

SADAKA YAKO NI KAMA MBEGU
Neno linasema unapopanda ukarimu utavuna...Mkulima anapopanda mbegu zake anatarajia kuvuna..Tatizo kuna watu wakipanda leo wanataka wavune kesho..mkulima anajua kanuni ya kilimo kuwa kuna muda wa kupanda na kuvuna..Muda wa kusubiri ni muhimu sana kwa Mkulima
Wakati mwingine kuna mbegu huharibika inabidi mkulima akarudishie nyingine au saa zingine mbegu hufa kwa kukosa mbolea au kuliwa na wadudu au kukosa mvua au saa zingine Mungu mwenyewe kwa vipimo vyake anaweza kuipelekea mbegu yako kuwa ni sifuri kama ile ya Kaini (mwanz4:3-5)
Kuna mbegu/sadaka ukimpelekea Mungu huvuni ..huwezi ukampelekea Mungu vilema au vipofu ukatarajia baraka..yaani..

Unakuta kuku ana ugonjwa wa kideri au mdondo huyo ndiye analetwa kanisani
-Ngombe/mbuzi hazai au anaumbwa huyo ndo ataletwa kanisani
-Kama ni mayai huwez amin kuna watu huleta yale mabovu..mwingine analeta papai/parachichi hayafai hata kula yameozaa!
-Kwenye kapu la sadaka unakutana na pesa ambayo haitumiki
-Noti imechanika nusu/haina namba au pesa ina kutu.
Ebu jiulize mtu anayetoa sadaka kama hizo anapata baraka zipi kama sio kujichumia laana?..Mungu akusaidie usiwe mmojawapo.

MUNGU ALIYEZIUMBA MBINGU NA NCHI AKUBARIKI SANA SANA KWA SAFARI UNAYOKWENDA KUANZA LEO YA KUMTOLEA MUNGU SADAKA KWA UAMINIFU UKIMTEGEMEA ROHO MTAKATIFU KUKUONGOZA KUTOA KATIKA MOYO WA UTII, MOYO WA KUPENDA, KWA IMANI, NA KWA FURAHA..AMEN!.

Comments