Na Mchungaji Bryson Lema, Ufufuo na uzima Morogoro. |
Utangulizi:
Ipo michoro ya ubaya katika
maisha.usipokuwa mwangalifu, unaweza
kuingia katika aina hii ya
michoro ya ubaya. ZABURI 38:12…[Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka
kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa.]…. Daudi alitafakari na kuona jinsi ambavyo wapo
watu wanaomwazia mabaya. Daudi mwana wa Yese, alikuwa akichunga kondoo wachache
wa baba yake kwa kuwa ndiye aliyeonekana mtoto mdogo kuliko wote, na kwamba
hawezi kuchunga kundi kubwa la kondoo.
Haa hivyo, ufalme ulimwangukia Daudi ingawa
baba yake (Yese) hakuwa anaonekana kama ndiye atakayefaa kutawala. Ndiyo maana Yese hakumuita Daudi
mbele ya Nabii Samweli, kwa sababu
alidharauliwa kuwa hakufaa, ingawa ndiye
ambayeMungu alitaka apakwe mafuta kuwa
mfalme.
Wanadamu wanaweza kukuona haufai lakini
ujue kuwa Mungu haangalii kama wandamu wanavyokuwazia. Halipo jambo
linaloweza kukupata ambalo
halijatengenezwa. Uonapo kitu, ujue kina mwanzo wake. Kila kitu huanza
kwa mchoro. Ukiona mti mahali ujue kuna siku mbegu ya huo
mti ilidondoka ardhini,ikafa na baadae ikachomoza kuwa mche wa huo mti.
Unapoiona pengine ndoa yako ina vurugu,
ujue kuwa huo mgogoro haukuibuka tu wenyewe, bali
ipomsababu ya kutokea hicho kilichotokea. Ndiyo maana YOHANA 3:16…[Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele.]… maana yake
Mungu hataki hata mmoja apotee. Tena neno linasema Mungu antuwazia mema.sasa
iweje maisha yangu hayapo jinsi neno hili halijatokea kwako? Siyo rahisi kwenda
salama kama haujafanya juhudi za kuufuta huo
mchoro.
Daudi baada ya kumuua Goliathi, akinamama walianza kumsifia kwa nyimbo
wakisema”Sauli ameua eflu,lakiniDaudi kumi elfu”. Jambo hili liliamsha hasira kwa mfalme Sauli akaanza kutengeneza michoro ya kumuangamiza
Daudi.
ZABURI
56:5-6….[Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu
yangu kunitakia mabaya. 6 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa
kuwa wameniotea nafsi yangu.]….
Daudi alikaa na watu na kuona jinsi wale anaoishi nao wanavyojificha na kumjadili
kisirisiri.
Hata leo hii wapo watu ambao bila
kujua bado wanapita kwenye zile njia za michoro yenye kuleta uharibifu kwenye
maisha yao. Wapo waliokaa vikao kwa kuumia tu
wanapoiona ndoa yako imetulia. Tena mbaya zaidi, pale unapowatangazia
kuwa mshahara wako umeongezeka, ni kosa lingine kubwa kwao. Adui wanapoichora
hii michoro, huweka na mipaka ya hiyo
michoro. Huweza kuitengeneza kwa
maana kuwa,watoto wako watasoma vizuri hadi sekondari, lakini wakifika chuo
kikuu pale tu wanapomaliza
wanachanganyikiwa. Maadui hawa ndio ambao hawataki mtu aishi yale maisha
ambayo Mungu aliyakusudia.
Usichokijua ni kwamba hata fedha yako mwenyewe inaweza kuchorewa
michoro. Ndiyo maana wengine pale wapatapo fedha, magonjwa hujitokeza au misiba
ya kila mara. Adui huitengeneza michoro
hii ili kwamba fedha inapoingia ipate matumizi
yasiyokusudiwa. Wengine kila mishahara inapoingia mwisho wa mwezi,
husiha baada ya muda mfupi,na matokeo yake unaingia katika mikopo kwenye maduka ya wafanya biashara. Wengine hununua
bidhaa ambazo hawazihitaji, ili angalau tu fedha yako isikae salama kwako.
Leo ni siku ya kuifuta hiyo michoro ya
maadui za maisha yetu kwa Jina la Yesu.
Ninacho kifutio ambacho ni damu ya
Yesu,iuliyomwagika miaka zaidi ya 2015
iliyopita.
MUNGU
ANASEMA JE KWA WACHORA MICHORO?
Imeandikwa katika ZABURI 41:5-7…[Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake
likapotea? 6 Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo, Moyo wake hujikusanyia
maovu, Naye atokapo nje huyanena. 7 Wote wanaonichukia wananinong'ona,
Wananiwazia mabaya.]… Mungu wangu
hamzuii mtu kuniwazia mabaya.nikijuacho mimi
ni kuwa maisha yangu
yapomikononi mwa Bwana Yesu. Leo naamuru
kuwa, Kila anitakiaye mabaya, aibu ikakae nyumbani kwake kuanzia leokatika Jina
la Yesu. Kama ulifikiri huo mchoro ni wa
kuniua, ujue umekosea, kwa sababu hilo
tatizo ulilotengeneza kwangu linamfanya Yesu aliye ndani yangu atoke nje na kuondoa kila mchoro ulioniwekea. Hakuna tatizo la
kunipoteza, kwa sababu mimi niliwahi kufa, naikazikwa na siku ya tatu
nikafufuka. Wewe uliyenichorea mchoro
imenifanya nifahamu kuwa kumbe mimi
ni shujaa, na kile nilichoa nacho
kinawasumbua mioyo yenu.
Ole wako wewe uliyechora mchoro maisha yangu. Ole wako wewe unayecheza na
ndoa yangu bila kujua kuwa mume na mke watoka kwa Bwana. Huo mchoro wenu uliua
lile jitu lenye kutenda dhambi, na sasa ameibuka mwingine asiyekufa tena, Kwa sababu hakuna kufa zaidiya mara moja.
Kumbe ilitakiwa ule mwili wa dhambikupitia mchoro wenu. Hii ni saa ya kuvaa
ule utukufu. Yusufu alitoka jela na
kwenda kutawala. Kama alivyotoka Yesu Kristo toka kaburini, siku ile ya tatu na wale walinzi wakapigwa usingizi
wakaamka wakalikuta kaburi li tupu, vivyo hivyo na wewe uliyenichorea mchoro
ninakupiga usingizi, na utakapoamka utakuta mchoro na kaburi uliloniweka
lipo tupu. Vita ikiibuka mtu
hubadilishiwa jina.hata askari atokapo
vitani haitwi tena askari, bali hiitwa shujaa. Shida huleta ushindi.
Yesu ambaye analo jina kuu kulikomajina yote,alizaliwa katika shida,kwenye
hori ya kulishia ng’ombe. Hata Samsoni
alipokuwa anaendelea kusaga ngano katika mateso yake, zile nywele zikaanza kuota tena.
Kama wewe upo hapa na haujaokoka ni ngumu
kuondoka kwenye huo mchoro. Ni
saa yako kuamua kumpa Yesu Kristo maisha yako
na kupata uwezo wa kuitumia Damu ya Yesu ili kufuta michoro iliyotengenezwa kwa ajili ya maisha yako.
© Information
Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778
Comments