Mwimbaji wa
nyimbo za Injili Tanzania Bahati Bukuku amejitokeza rasmi mbele ya
uongozi wa chama cha muziki wa injili nchini Tanzania na kutoa taarifa
yake rasmi kuamua kusimama pamoja na mmoja kati ya wanaotangaza nia
kuwania uraisi nchini Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
CCM,Mh.Edward Lowassa anayetarajia kutangaza nia yake mjini Arusha.
"Bahati Bukuku
ametoa taarifa rasmi kwa uongozi wa Chama cha Muziki wa Injili nchini
Tanzania CHAMUITA na kubainisha wazi kwamba atakua ni miongoni mwa watu
watakao kuwepo mjini Arusha katikaViwanja vya Shekh Amr Abedi kumuunga
mkono Mh. Edward Lowasa anapoenda kutangaza nia katika harakati za
kusaka Uraisi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.
 |
Kutoka
kushoto ni Rais wa CHAMUITA Addo Novemba, Mwimbaji wa nyimbo za Injili
Tanzania Bahati Bukuku, na Katibu Muenezi wa CHAMUITA Stella Joel
|
Mmoja wa Viogozi wa chama hicho cha Muziki wa injili Tanzania Katibu Muenezi wa CHAMUITA Stella Joel ameeleza
kwamba wao kama viongozi wamemuelewa na wanamtakia kila la heri katika
safari yake na shughuli nzima ya kumuunga mkono Mh. Edward Lowasa".
Credit:Mjap inc blog
Comments