NGUVU YA MKRISTO, YAPATIKANA KWA ROHO MTAKATIFU.

Na Nickson Mabena

Bwana Yesu asifiwe, karibu tena kwa ajili ya kujifunza Neno la Mungu...
“Lakini Mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wanchi.” Matendo 1:8.
Roho Mtakatifu sio Nguvu, bali anazo Nguvu.
Yesu aliwaahidi wanafunzi wake (WAKRISTO) kwamba watapokea nguvu siku Roho Mtakatifu akiisha kuja kwao. Katika kweli hii ya Neno la Mungu nataka wewe Msomaji ujue ya Kwamba, Katika maisha yako ya UKRISTO bila kuwa na Nguvu za Roho Mtakatifu hutaweza kusonga Mbele, wala hutaweza kuishi Maisha ya ushindi, kwani kuna vikwazo vingi sana ambavyo vinaweza kukurudisha nyuma.

Ingawa Roho Mtakatifu ana kazi nyingi sana kwenye Maisha yetu, ila sitaki kuzungumzia hizo kazi katika somo hili, hapa nitaelezea nguvu zake, na umuhimu wa nguvu zake kwetu!.
Wakati nakifuatilia kitabu cha Matendo ya Mitume, ambacho kinaelezea sana kanisa la kwanza jinsi lilivyotembea na Mungu, na Mungu alikua akijidhihirisha kwa namna ya ajabu sana, na mojawapo ya siri niliyoiona ni kwamba walimtaka Mungu na Nguvu zake,
tofauti na wakati huu, Roho Mtakatifu amewekwa pembeni, huoni akapewa nafasi kubwa, huoni watu wakijazwa Roho Mtakatifu kama zamani, ndugu msomaji, wewe Mwenyewe tafuta mda na ukisome vizuri kitabu cha Matendo ya Mitume, utayaona Mengi sana kuliko haya ninayokuandikia.
Swali mojawapo ambalo najiuliza, ni kwamba WAKRISTO watawezaje kumshinda Shetani bila ya kuwa na Nguvu za Roho Mtakatifu!?.
Neno la Mungu linasema hivi “Mtakeni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote.”
1 Nyakati 16:9.

Sasa kwa nini Kanisa linamtaka Mungu, na halitaki Nguvu za Mungu!?, Kanisa linamuhitaji Roho Mtakatifu sana, sio Mda wa kung’ang’ania mapokeo ya viongozi wetu wa dini, Bali ni Mda wa kuzitafuta Nguvu za Mungu, unayeusoma ujumbe huu, unamuhitaji Roho Mtakatifu sana. Huwezi kusonga mbele wala kufanikiwa katika ufalme wa Mungu bila ya kuwa na nguvu!.
Roho Mtakatifu sio nadharia (theory), ni halisi kabisa, ahadi ya Roho Mtakatifu si kwa ajili ya watu wengine, Bali kwa wote waliotubu, na kuamua kuziacha dhambi zao, na kumfuata Yesu kikamilifu, Maandiko yanasema
“Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wotewalio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”. Mdo 2:39

Kama wewe umeokoka, una haki ya kujazwa Roho Mtakatifu, na kunena kwa Lugha Mpya. Hutakua mnyonge tena, pia hutapooza tena, huduma yako haitadumaa tena, utakua kiroho hadi mwenyewe utajishangaa!.
Tafuta uso wa Mungu, tafuata Nguvu za Mungu, Mtafute Roho wa Mungu ili uwe Mshindi siku zote!.

Kwa leo naomba niishie hapa, naamini umepata kitu cha kukusaidia, jitahidi uyatendee kazi maneno ya Mungu uliyojifuza humu!.
Mungu akubariki sana!.......

Salamu Zangu kwako (0712265856 watsap number)

Comments