NIDHAMU KWA KIJANA NI JAMBO LA LAZIMA.


BWANA YESU atukuwe ndugu yangu.
karibu nikupe maarifa ya ki-MUNGU ya kukusaidia na kukuvusha.
Leo nazungumzia kijana  na nidhamu.
Kutoka 20:12 ''Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, MUNGU wako. ''
-Heshima ni jambo muhimu sana kwa kijana.
-Heshima inaweza ikasababisha ukaishi maisha marefu.
-Nidhamu inaweza ikasababisha ukapata kazi.
-Nidhamu inaweza ikasababisha ukapata nafasi ya kiungozi ambayo haikukustahili hata kidogo.

Nidhamu hubeba mambo matatu(3).
1.   Uvaaji.
2.  Matamshi.
3. Utumiaji wa fedha.

=UVAAJI.
1 Timotheo 2:9-10 ''  Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa MUNGU.''
-Biblia inasema wanawake wavae mavazi ya kujistiri haimaanishi kwamba wanaume wasijistiri bali hata wao hawatakiwi kutembea uchi. vijana ni kundi ambalo liko katika jinsia zote yaani jinsia ya kike na jinsia ya kiume hivyo andiko kama hili hapo juu linawahusu na vijana pia.
-Kijana unatakiwa uvae kwa nidhamu.
-Kijana hatakiwi kuvaa vazi ambalo litaacha maswali.
-Ukivaa nguo ambayo inaleta maswali kwa watu wewe huna nidhamu.
-Kuna nguo wewe binti huruhusiwi kuvaa mbele ya baba yako. unadhani ni kwa nini?
-Na kama kuna nguo hutakiwi kuzivaa mbele za wazazi wako au wakwe zako basi tambua kwamba sio huko tu ndio hutakiwi kuzivaa nguo hizo bali hata kwa watu wengine wenye heshima zao hutakiwi kuzivaa na hakika watu wote duniani ni wenye heshima zao.
-Kama unavaa nguo ambazo ni mbaya kuvaa mbele za wazazi wako basi hakika wewe huna nidhamu.
-Kuna nguo zimetengenezwa kabisa maalumu kwa ajili ya makahaba tu. lakini dada zetu wengi wanavaa nguo hizo hizo za kikahaba, hiyo ni nidhamu mbaya.
-Jambo la kujua pia ni kwamba wanaume hupenda kwa kuona lakini wadad hupenda kwa kuhisi au kwa hisia. mavazi mengi yamewaacha mabinti bila kuolewa maana vijana lazima tu wanadhani kwamba wewe ni kahaba kumbe una heshima zao ila mavazi yamekuharibia. inawezekana kabisa dada ukivaa kikahaba unapigiwa sana miluzi na vijana hiyo haimaanishi kwamba wewe ni mzuri sana ila hiyo inamaanisha kwamba vijana wale wanadhani wewe ni kahaba na unapatikana kirahisi tu maana wewe ni hamnazo. kumbe ni binti mwenye heshima zake lakini mavazi yamemharibia. ndugu kuvaa mavazi mabaya ni taarifa kwamba huna nidhamu.
-Kuna mavai ya wadada huwafanya vijana wawapende ila ni kwa muda mfupi tu kisha wanaendelea na kutokuwapenda wadada hao, mwenye sikio na asikie.
-Kijana wa kiume unavaa mlegezo na kuonyesha nguo ya ndani tena chafu, huko ni kukosa nidhamu.
-Mlegezo uliletwa mwanzo na mashoga huko ulaya maana ili mtu ajulikane kwamba ni shoga basi alivaa mlegezo, watu wakiona waovu walipokuwa wanamuona mtu wa mlegezo basi waliweza hata kupiga mluzi ili asimame kwa ajili ya mambo ya kishetani maana watu kama hao shetani ameingia mzima mzima.
-Mwanaume umesuka, mwanaume unavaa hereni, huko ni kukosa nidhamu.
1 Yohana 3:20-21 ''  ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana MUNGU ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa MUNGU;  ''
=MATAMSHI.
1 Petro 3:10 '' Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. ''
-Kuna maneno hayana nidhamu.
-Kinywa kilichojaa matusi hapo hakuna nidhamu.
-Maneno yako mazuri yanaweza kusababisha ukaolewa au ukapata mke.
Tabia mbaya ni mzigo hata kwa wazazi.
Mithali 17:27 ''  Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara.''
-Maneno machafu yanaweza kuwafanya watu wakuone hufai hata kama unafaa.
Yakobo 3:2 '' Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu. ''
-Mtu asiyejikwaa katika kunena huyo ni mtu mkamilifu.
-Wengi sio kwamba wanajikwaa kusema maneno mabaya au matusi bali ni tabia zao na tabia hizo zinaweza kuwakosema vitu vingi vizuri, tabia hizo zinaweza kuwakosesha baraka zao. kuongea matusi ni kukosa nidhamu.
Mithali 10:20 '' Ulimi wa mwenye haki ni kama fedha teule; Moyo wa mtu mbaya haufai kitu.  ''

=NIDHAMU KATIKA FEDHA.
Mithali 3:9 ''Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. ''
-Pesa inahitaji nidhamu kuitunza, usipoitunza lazima itakukimbia.
-Unapata pesa lakini hata zaka hutoi, huko ni kukosa nidhamu.
-Unapata fedha lakini hata sadaka kanisani unaangalia ka pesa ambako hata kununua pipi huwezi ndiko unatoa sadaka, huku mfukoni una laki 9, huko ni kukosa nidhamu.
-Jijengee kuweka hakika, lakini pia hakikisha unaweza hazima mbinguni kwa kumtolea MUNGU sadaka, hiyo ndiyo nidhamu sahihi kwa kijana.
-Ukikosa nidhamu ya laki moja(100,000/=) MUNGU hawezi kukupa Milioni moja(1000,000/=)
Zaburi 24:1 ''1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake. ''
-Kumheshimu MUNGU kwa mali yako ni jambo jema
-Kumheshimu BWANA kwa kipato chako ni nidhamu nje.a
-Mweshimu MUNGU kwa kumtolea zaka na sadaka. MUNGU anasema
Mithali 8:18 ''  Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia.''
-Naamini kuna vitu vizuri umejifunza. ndugu tendea kazi neno la MUNGU wala usiliiache likupite. Neno kama hili haliji tu kwa akili za kibinadamu bali ROHO MATAKATIFU ndiye anayehubiri kupitia watumishi wake na lengo la MUNGU ni wewe usibaki kama ulivyokuwa baada ya kujifunza.
Mithali 13:11 ''  Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa. ''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
mabula1986@gmail.com
+255714252292.
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili

Comments