NYUMBA YA UTUMWA
Siku ya kutoka kwenye hiyo nyumba ya utumwa ni leo. Farao wa Misri
anafananishwa na shetani kwa maisha ya leo. Siyo kwamba mtu hapendi kuja
kanisani, au hataki kuomba, au hataki
kuacha uvutaji sigara. Yote haya hayawezi kutokea hadi pale huu utumwa utakapoondolewa.
Haijalishi hiyo nyumba ya utumwa imewekwa na nani. Ni saa ya kuondoka
katika nyumba ya utumwa. Ni saa ya
Tanzania kufunguliwa kutoka kwenye Nyumba ya Utumwa. Tanzania siyo maskini,
wala watu wake siyo maskini. Shetani ameiweka nchi katika hali ya umaskini.
Siyo mpango wa Mungu kuwa jinsi
ulivyo.wapo watu waliokuendea kwa waganga wa kienyeji.unaweza kuwaangalia watuwa
nyumbani/familia yako na kusema, hawa hawawezi
kuniendea kwa waganga wa kienyeji
kwa sababu ni watu wanaoenda kanissani.kwenda kanissani siyo hoja, bali hoja ni mtu kuwa na Yesu moyoni mwake.
Ukiwa umefungiwa kwenye nyumba ya utumwa ujue kuwa yupo pia mwenye nyumba
hiyo ya utumwa. Maisha hayaanzii kwenye
ulimwengu wa mwili, bali kwenye ulimwengu wa roho usioonekana. Haijalishi adui
zako walikufunga lini au mwaka gani. Ni saa ya kutoka kwenye nyumba ya utumwa.
Vipo vifungo tofauti tofauti, kwa sababu
vingine havifai hata kuwemlezea mtu. Shetani anawatumikisha watu.ndiyo maana
wapo watu wanaitwa walevi, lakini binafsi hawapendi kuwa walevi. Kile kifungo ndicho kinachomtumikisha
mtu kuwa mlevi au kufanya jambo asilopenda kufanya. Unapoitwa mtumwa, ni
sharti kufanya kadiri anavyotaka ufanye bwana wako. Shetani ana watu
wake (mawakala) anaowatumia ili kuweka wengine magerezani.
Kila mahali waliponifunga nisioe au nisiolewe, walionizuia nisipate
kazi,walionizuia nisiwe tajiri leo ni siku
ya kutoka kwa ushindi wa Jina la Yesu. Upo kama ulivyo lakini siyo kwa
mpango wa Mungu. Wapo watu waliotengeneza huo ugumu katika
maisha yako. Kila nyumba ya utumwa ina tofauti na nyingine kutokana na
aina ya kafara iliyotolewa na adui yako. Yupo adui anayetoa kafara ya njiwa au
kuku, na ikeshatolewa kwa mganga wakienyeji damu ya hawa ndege husababisha
ufukuzwe kazi au ndoa yako isitulie. Wapo
wengine wanaotoa mbuzi au ngo’mbe au hata roho ya mtu. Aliyetoa kafara
ya kuku au njiwa ni tofauti na aliyemtoa mtu / mwanane wa kuzaa. Mashetani
waliopewa chakula (damu) kwa ajili hii, husimamia majukumu yao kwa umakini
kuhakikisha kwamba kile walichoamuriwa kufanya kinafanyika barabara.
Yesu Kristo alitolewa kafara iliyo kuu kuliko zote na ndiyomaana inanyamazisha
kafara zingine zote. Imeandikwa YOHANA
3:16..[Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.]… Maana yake ni
kwamba, Damu ya Yesu ambaye
hakuwa na dhambi ina UWEZO kuliko damu zote za wanyama na wanadamu wenye dhambi
waliotolewa kafara kwa ajili yako.
Mafanikio ya mtu huanzia rohoni. Akiwepo Mbunge au mtu yeyote mashuhuri na ambaye anaonekana
amefanikiwa, ujue aidha amepata hayo mafanikio kutoka kwa Mungu aliy hai
(Jehovah) au kwa Shetani.
KUOKA
6:9…[Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini
hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa
mgumu.]… Mtu
anapokuwa katika hali ya utumwa, hawezi kuelewa kitu chochote.
Ugumu wa maisha ya utumwa uliwafanya
wana wa Israeli wasiweze kumsikilisza
Musa. Usiwe na huzuni, kwa sababu yupo Yesu Kristo awezaye kukuondoa katika huo
utumwa. Hakuna jambo gumu asiloliweza Baba Mungu wa Mbinguni.
Imeandikwa “Kila
pando asilolipanda Baba wa Mbinguni
litakwenda kung’olewa”. Hizi ni kazi za shetani. Wote waliokaa na
kuleta mapando yao ya kuonea watu lazima leo yakang’olewe kwa Jina la Yesu. Wote
waliopanga mipango yao ili maisha yangu yasifanikiwe lazima wapigwe kwa Jina la
Yesu.
Shetani ana sifa moja kubwa ya kujigeuza geuza. Imeandikwa katika LUKA
13:11….[Na
tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na
minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.]…Huyu pepo wa udhaifu ndiye aliyepindisha huo
mgongo. Huyu mama angeenda hospitalini angeonekana mgongo umepinda.shetani kwa
hiyo anaweza kuingia ndani ya mwili wa mtu na kugeuka kuwa pepo la
udhaifu, aidha kwenye tumbo,mgongoni
n.k. na kufanya tatizo lako liwe la kugeuka geuka. Ukienda hospitaliniwataliona
tatizo lakini ukipewa dawa hauponi. Kila kitu kwa hiyo huanzia rohoni. Nampenda
sana Yesu Kristo kwa sababu popote
alipopita akakutana na utumwa alikuwa anawaweka watu wale huru. Yesu
Krsito amekuja hapa leo kuzikata kamba za utumwa kwa Jina la Yesu.
Saa ya Bwana kuyaangalia maisha yako na yangu imefika. Ni saa ya Bwana
Yesu anayekaa ndani yangu kushuka na
kutembea na kuondoa kila utumwa mlionivisha. Kwa mateso yale nimemfahamu Mungu wa kweli zaidi. Wote
walionitesa ni saa ya Bwana kuwashughulikia. AYUBU 23:10….[ Lakini yeye aijua njia niendeayo;
Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.]… Leo ni saa ya kuondoka kwenye lile jaribu tena kwa ushindi.
Aliyesimama kinyume na wewe asikutishe kwa sababu walioko upande wako ni wengi
kuliko hao maadui zako.
ISAYA
14:3....[Tena itakuwa katika siku ile, ambayo Bwana atakupa raha baada ya
huzuni yako, na baada ya taabu yako, na baada ya utumishi ule mgumu
uliotumikishwa;]… Ni saa ya Bwana kunisimamisha tena,ni
saa ya Bwana nkunipa raha tena.kila
walichokipanga kwenye ndoa yangu au katika maisha, yangu imekwisha. Jemedari wa kweli Yesu Kristo yupo ndani ya Nyumba hii
leo kubadilisha mipango yote ya maadui
zako ili uwe na uzima tena uwe nao tele.
Huwezi kutoka utumwani kama bado hujampokea Yesu Kristo.kama hujaokoka ni
vyema ufanye maamuzi leo ili uweze
kutoka kwenye hiyo Nyumba ya Utumwa.
© Information
Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778
Comments