USHUHUDA:NYUMBA YA GHOROFA ISIYOKALIWA NA WATU


Huu ni  ushuhuda wa Mmishenari Mtanzania anayehubiri Injili Nchini Madagaskar. Kwa sasa ni miaka karibu mitano tangu aanze Huduma huko.
Alipoenda mara ya kwanza alifikia kwenye mji ambao hakuna mtu aliyewahi kusikia jina 'YESU'! Alifanya Huduma kwa miaka miwili watu wengi wakaokoka.
Miongoni mwa waliookoka ilibidi ufanyike utaratibu waanzishiwe Chuo cha Biblia. Mahitaji yote muhimu yalikamilishwa na wakabaki wanatafuta jengo la kupanga.
Katika kutafuta walielekezwa nyumba moja ya ghorofa mbili ambayo tangu ijengwe hajawahi kuingia mtu. Ilikuwa na mapepo, tangu ilipokamilika, mtu yeyote (akiwemo aliyeijenga) akiingia mlangoni huambulia bakora, na hawaoni wanaompiga!
Watumishi walipopata taarifa hiyo, wakamtafuta mmiliki wa nyumba hiyo, walipomuuliza kodi kwa mwezi walishangaa akiwaambia dola 10 sawa na sh 17,000/- kiasi ambacho ni kidogo mno kwa nyumba nzima ya ghorofa mbili! Watumishi walilipa kodi ya mwaka na masomo yakaanza, wanafunzi wakawa wanalala hapo.
Baada ya miezi kadhaa, mwenye nyumba alikuja kuuliza iwapo na yeye anaweza akaingia na asipigwe bakora kama zamani! Hiyo ilikuwa ni nafasi nzuri ya kumuelezea uweza wa Mungu katika Jina la Yesu.
Hadi sasa Watumishi bado wanalitumia jengo hilo, na hakuna cha kupigwa bakora wala pepo la namna yoyote!

Comments