UTAKATIFU KWA MTEULE NI JAMBO LA LAZIMA.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
''Yeye Asemaye, Nimemjua(MUNGU), Wala Hazishiki Amri Zake, Ni Mwongo, Wala Kweli Haimo Ndani Yake,- 1 Yohana 2:4.
-Mteule ni yule ambaye anamtii KRISTO na ameokolewa na BWANA YESU.
-Mteule lazima azishike amri ya MUNGU na kuzitii.
-Amri za MUNGU ni nyingi sana na zote mteule anatakiwa azishike. alichokikataa MUNGU na mteule wake anatakiwa akikatae, kile ambacho BWANA hataki tukitende hakika ni lazima tukae mbali nacho.
-Kuna watu hudhani kwamba amri za MUNGU ni zile amri 10 tu kumbe amri za MUNGU ni maagizo yote ya MUNGU yaliyo katika Biblia. mfano ni kuacha uchawi haiko katika amri 10 za MUNGU lakini agizo la MUNGU ni kwamba usiwe mchawi na agizo la pili la MUNGU katika hilo ni kwamba wachawi wote sehemu yao ni jehanamu. kumbe amri za MUNGU tunatakiwa tuzijue na msimamizi wa amri hizo ni ROHO MTAKATIFU.
- UTAKATIFU KWA MTEULE NI JAMBO LA LAZIMA. 
-Mteule Ni Yule Aliyempa BWANA YESU Maisha Yake Na Kuanza Kuliishi Neno La MUNGU. Biblia inasema juu ya mtu huyo kwamba amekuwa kiumbe kipya yaani amezaliwa mara ya pili. amezaliwa kwa neno na kwa ROHO wa MUNGU. Alizaliwa mwanzo na wazazi wake wa kimwili lakini sasa anampokea BWANA YESU anakuwa amezaliwa mara ya pili kwa MUNGU. Anakuwa kiumbe kipya kilicho na haki ya kuingia uzima wa milele.

2 Kor 5:17 '' Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.''

-Na Tena Kunakuwa Hakuna Hukumu Kwa Mtu Huyo Maana Ameokoka. alipookoka na kutubu dhambi zake zote zilifutwa na sasa yuko huru.
Warumi 8:1-2 '' Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU. Kwa sababu sheria ya ROHO wa uzima ule ulio katika KRISTO YESU imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. ''
-Wateule hawaki katika hukumu maana kumpokea YESU kumewaweka huru.

-Lakini Hukumu Huja Tu Pale Ambapo Ataacha Utakatifu 
Ndiposa Lazima Tujue Kwamba Utakatifu Ni Jambo La Lazima Kwa Mteule Wa KRISTO. 
Kuna Watoto Wa MUNGU Na Pia Kuna Watoto Wa shetani
1 Yohana 3:10  ''  Katika hili watoto wa MUNGU ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na MUNGU, wala yeye asiyempenda ndugu yake.''
-Watoto wa MUNGU ni wateule wa KRISTO.
-Watoto wa MUNGU ni wale wanaomtii KRISTO.
-Watoto wa MUNGU ni wale ambao hutenda haki na ni watakatifu.
 -Watoto Wa MUNGU Ni Wale Waliompokea YESU
Yohana 1:12-13 ''Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. '' 
-Hivyo Watoto Wa MUNGU Laziwa Washike Utakatifu Wa Kweli.

- Njia Ya Watenda Dhambi Ni Chukizo Kwa MUNGU
Mithali 15:9-10 '' Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali humpenda mtu afuatiaye wema. Adhabu kali ina yeye aiachaye njia; Naye achukiaye kukemewa atakufa. '' 

-Ndugu Zangu Kujua Tu Kwamba MUNGU Ni Mmoja Haisaidii Bali Kuwa Mtakatifu Wa KRISTO Ndio Jambo La Muhimu
Yakobo 2:19-20 ''Wewe waamini ya kuwa MUNGU ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?'' 
-MUNGU Ni Mtakatifu
1 Petro 1:15-17 ''bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita BABA, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. '' 
-Kumbe ni lazima tuwe watakatifu. kama mteule haishi maisha mataktifu huyo sio mteule bali anasindikiza tu wateule maana wateule lazima waishi maisha mataktifu.

-Hivyo BWANA Anatutaka Tuwe Watakatifu
Waebrania 12:14-15 '' Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona BWANA asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya MUNGU; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. ''
-Sio tuwe watakatifu tu bali Tena Anatutaka Tuwe Wema Siku Zote Amosi 5:14 '' Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi; hivyo BWANA, MUNGU wa majeshi, atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo. ''
-Si hili tu bali hata kuabudu tunatakiwa  tumwabudu MUNGU.
Ndugu, Hakikisha Unamwabudu Katika Roho Na Kweli
Yohana 4:24 '' MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.   ''

 Ndugu zangu, ni muhimu kuishi maisha matakatifu. ndio maana ninasema kwamba utakatifu kwa mteule ni jambo la lazima. 
-unajua kwanini utakatifu ni jambo la lazima? ni kwa sababu Kila Mtu Matendo Yake Yatamfuata Siku Akiondoka Duniani. Ndugu Yangu, Unadhani Ni Matendo Gani Ya Sasa Ya Kwako Yatakayokufuata? 
Kama Hutatubu Kwa BWANA YESU Na Kumpokea Hakika Matendo Yako Yote Mabaya Yatakufuata Siku Ukifa. 
Damu Ya YESU KRISTO Pekee Ndio Kwayo Tunafutiwa Dhambi Zetu, Ndugu Tubu Na Kumpokea BWANA YESU Ungali Hai, Ishi Sawasawa Na Neno La MUNGU Utafanya Vyema. Wengi Waliomdharau BWANA YESU Wangali Duniani Kwa Sasa Hao Wako Kwenye Giza Wakitamani Hata Dakika Moja Waje Duniani Na Kutubu. Ndugu, Kila Jambo Lina wakati Wake, Hata Maonyo Haya Yana Wakati Wake, Ukimkataa YESU Katika Muda Huu Yawezekana Kabisa Ukakumbuka Ukiwa Kuzimu. 
-Kumkataa YESU Na Wokovu Wake Ni Kuukataa Uzima Wa Milele. 
-Ndugu, Hujachelewa, Amua Vyema Leo. Kumbuka Kesho Yako Imebebwa Na Leo, Maamuzi Mazuri Ya Leo Yataileta Kesho Yenye Uzima Wa Milele.
BWANA YESU anasema ''
Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake-Ufunuo 22:12-14 '' 
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
mabula1986@gmail.com
+255714252292.
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili

Comments