![]() |
Na Moses Chapa. |
Unapookoka nawe umechaguliwa kuwa mfalme na kuhani ktk dunia hii,utavilithi ulivyotakiwa upewe maana wewe kipenzi cha Mungu basi atakupa thawabu.Usiogope chuki nayokujia sababu ya wokovu wako Daudi ktk safari yake ya kumuua Goliath akaanza kupata umaarufu watu walimsifia,na hapo Sauli akaanza kumchukia 1SAMWELI 18:8 Basi Sauli akaghadhibika sana na maneno haya yakamchukiza,akasema wamempa Daudi makumi elfu na mim wamenipa elfu tu.Kuna nin tena awezayo kupata isipokuwa ufalme!.Sauli aliingiwa na wivu kuona anapendwa,wewe nawe unapendwa na Mungu adui anaingiwa na wivu akitaka kukuzimisha.Wakati watu wanakuchukia usiofu ujue unapendwa nao wamejua.
..Mungu alikuwa anampenda sana Daudi,Sauli akaingiwa na wasiwasi kuona Upendo ule utakuja kumketisha katika kiti cha ufalme,naye atachukua nafasi yake,hivyo akamchukia sana akitaka kummaliza..Lakini katika chuki ile Daudi hakuteteleka kiimani ndo kwanza alizidi kumtegemea Mungu,chuki ile iliimarisha imani ya Daudi...Na katika chuki zote alizozipata Daudi hakuonyesha kulipiza kisasi kwa Sauli alingoja haki ya Mungu mtetee ije kumlipizia kisasi juu ya Yule anayemchukia..Chuki kitu kibaya sana,adui anaitumia kama siraha yake ili kukukatisha tamaa usifikie malengo yako,Daudi alichunga moyo wake usiingiwe na chuki..Siku zote usilipize ubaya kwa ubaya,bali ubaya kwa wema,kwani Daudi katika kutendewa mabaya na Sauli hakuingiza chuki ndani ya moyo wake alijua wivu wa Sauli tu kuona yeye ameachwa na Mungu na Daudi amependwa na Mungu...Daudi alirudisha wema kwa Sauli,KWANI ALIKUWA NA ROHO WA MUNGU hivyo alikuwa na moyo wa ajabu kwani aliushinda ubaya kwa wema,alikuwa mtu mwema hata kwa adui yake.Ingawa Sauli alimchukia kwa miaka 15 akiitafuta roho yake naye akikimbia nyikani,lakini akatafuta kulipiza wema. Biblia inasema katika
2SAMWELI 9:3
Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.
Basi siku zote unapofanikiwa vita inaibuka juu yako kwakuwa ni wivu wa adui tu kuona unaenda kuchukua nafasi yake atawatumia watu kukuzuia..
Mambo ya chuki yapo katika Familia,makazini,mashuleni katika jamii watakuchukia kwakuwa tu ni wa tofauti na wao,wewe upo nuruni wao wapo gizani,wewe umepata na wao wamekosa..Ni wivu wa kuona utakuwa juu yao...Usirudishe ubaya wanaokufanyia siku moja Mungu wako atakulipizia...
MBARIKIWE...
Comments