AKILI YA KUMILIKI HAZINA NA MALI

Pastor Paul Joshua katika huduma.
NA SNP PAUL JOSHUA (UFUFUO NA UZIMA KIGOMA)


2 Wakorintho 8:9 Maana mmejua neema ya bwana wetu Yesu kristo, jinsialinyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake,
Yesu alikubali kuwa maskini ili sisi tuwe tajiri, alikubali kuzaliwa katika familia ya selemara ili sisi tuinuliwe. Sasa kama Yesu alikuwa maskini ili sisi tuwe tajiri inakuwaje sisi tuwe maskini na tunaishi maisha yakuhangaika.
2 nyakati 1:10 basi sasa nipe hekima na maarifa , nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi.
Solomoni alikuwa mjanja alimuomba Mungu hekima na maarifa, kama huna hekima na maarifa hata ukipewa mali hutaweza kuzitumia. Solomoni aliomba hekima ili aweze kuongoza watu wa bwana. Kumbuka hata ukipewa vitu vizuri kiasi gani lakini kama huna hekima ya kuvitumia vitakushinda au kutoeka kabisa.
Hagai 2:8 fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema bwana wa majeshi.
Kila kitu ni mali ya bwana, lakini leo chakushangaza mtu akiwa tajiri kidogo tu anaitwa freemason, hii ni kwasababu watu wamefungwa akili. Kwakuwa Mungu wetu anakila kitu nasi yatupasa kupata kila kitu nasio kuwa na mawazo finyu ya kuwa matajiri ni freemason. Ikiwa freemason wanamali nyingi sisi yatupasa kuwa nazo zaidi ya wao kwakuwa mali ni za baba yetu
Kama fedha na dhahabui ni mali ya bwana basi ni mali ya wana wa Mungu, (walokole) iwezekanaje baba anadhahabu halafu wewe ni maskini.
Baba yetu anasema fedha na dhahabu ni mali yake, waone watu umejaa dhahabu, na tena watu wakikuuliza waambie ni metoa kwetu. Neno linasema bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu, ikiwa yeye ni baba name namiliki mali za baba.
Inatakiwa tumiliki, tena leo tumwambie shetani ya kuwa kukosa pesa sio asili yetu, kupanga sio asili yetu, kuombaomba sio asili yetu, sisi ni watu wambinguni,
Acha tuone kwetu palivyo na ili tujue sisi tunatakiwa tuishije au tuweje.UFUNUO 21:21 NA ILE MILANGO KUMI NA MIWILI NI LULU KUMI NA MBILI; KILA MLANGO NI LULU MOJA. NA KILA NJIA YA MJI NI DHAHABU SAFI KAMA KIOO KIANGAVU. Kila kitu na dhahabu ni mali yake, hata barabara zake ni dhahabu.
mali za baba yetu lazima tuziishi, kama kwa baba yetu ni kuzuri kiasi hicho iwezekanaje sisi tuishi maisha ya ajabu,
Tatizo walokole wamekuwa waombaji na wanenaji tu, lakini hawana mali na wanalala njaa,wanalidhika na hali hiyo, ukiwaambia kuomba wataomba lakini maskini, lakini baba yao tajiri, Yakobo alimng’ang’ania bwana mpaka akabarikiwa, aliliona hili, alijua kuwa baba yake anavyo vyote hivyo akataka ambariki, akasema afadhali nimekutana nawe leo lazima unibariki. Yakobo akambana bwana.
Inatakiwa na wewe mbane baba yako, umwambie ikiwa barabara zako zimejengewa dhahabu lakini mbona mimi sina kitu, mng’ang’anie bwana mpaka japo aliondoka anachechemea lakini amebarikiwa. Akaitwa Israel. Walokole wamerogwa na kufungwa akili ili wasimjue baba yao alivyo, katika vifungo vibaya ni akili, bora mtu afunge mikono na miguu akuachie akili. Ndo maana Sulemani alikuwa mjanja aliomba hekima na maarifa. Wachawi kabla hawajafungwa sehemu nyingine wanafunga akili.
Usipouchukia umaskini huondoki,
Simama imara wewe ukiinuka na wanao wameinuka, ukibarikiwa na wanao wamebarikiwa.
Isaya 45:3 nami nitakupa hazina za gizani, mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni bwana nikuitaye kwa jina lako naam, Mungu wa I srael.
Hazina zimefichwa gizani na watu wagiza. Katika eneo ambalo shetani amefunga watu ni katika kupata mali maana anajua kuwa mlokole akiwa tajiri ni hatari sana,
1) Ataomba bila mawazo , kuna mtu anaomba lakini anawaza atakula nini.mwingine amefunga tatu lakiki anawaza baada ya hapa nitafungulia nini.
2) Ataheshimika, tatizo walokole wanadharaulika sana; ili watu wakuheshimu lazima uwe na mali, kama ni maskini watu hawawezi kukueshimu.
3) Fedha inapeleka injili ya Yesu, (wataendaje wasipopelekwa) na hapo ndipo shetani ana bana anawabana watu wa Mungu wasimiliki
Leo kama tunaweza kutoa pepo na wakatoka na tunaweza kuita mali na zikaja. Tumepewa nguvu za kupata utajiri, Mungu anatupa nguvu za kupata utajiri na sio utajiri tatizo akili imelogwa.
Kama unaweza kutoa pepo kwanini usimiliki. Kama unaweza kusambaratisha adui zako kwanini usimiliki. Ndani yako wewe kuna nguvu.
Ili uheshimike lazima umiliki mali, walokole wazamani walidharauliwa kwakuwa hawakuwa na kitu, walionekana kama watu waliokosa kazi. Hata ukiomba kiasi gani kama huna kitu watu watakudharau tu, ni kweli anaupako, kama unaupako wakutoa pepo kwanini usilete pesa? Hapo ndio walokole tujiulize ni wapi tumepindishwa na wachawi. Tatu kavu mara kwa mara kwanini zisilete pesa?
Kuna sehemu ambapo shetani ameshika. Tunakazi yakuvihamisha vitu kutoka katika ulimwengu war oho na kuvileta mwilini, neno linasema Mungu katubariki kwa Baraka zote za rohoni na za mwilini, katika ulimwengu wa roho umeshabarikiwa, Mungu akikutazama anakuona bonge la tajiri lakini unaombaomba.
Mithali 3:16 anawingi wa siku katika mkono wake wa kuume, utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
Utajiri na heshima vinaendana.ili wapentekoste waheshimike lazima wamiliki, wasitambulike kwa kuomba na kulialia tu bali kkwakumiliki pia. Yaani inatakiwa kile unachokiomba waanze kukiona kwa macho.
Hata wamama wanatakiwa kusimama na kusaidia familia, hakuna mama wa nyumbani, usimwachie baba tu kutafuta mali
Unafunga mpaka unachoka, unafanya maombi halafu unakaa badala ya kuchukua hatua, ukidai unamngoja bwana, utangoja mpaka utakoma
Unaposema umeokoka acha watu washuhudie waokovu wako wa rohoni na wa mwilini. Ndugu ufanikiwe na kuwa na afya kama roho yako ifanikiwavyo. Ndio maana nasema amka kwa jina la Yesu
Mwenye mali masaa anayo tumia ni sawa na wewe tatizo ni kichwa (akili)

Comments