BAADHI YA SABABU ZINAZOFANYA VIJANA WENGI WAOGOPE KUINGIA KWENYE NDOA;


1.Wengi Hawaelewi Hata Maana Ya Ndoa Na Kusudi La Ndoa [Yaani Kwanini Mungu Alianzisha Ndoa]; Hivyo Inakuwa Ngumu Kuingia Ndani Ya Jambo Usilolijua Linatendaje Kazi Na Kanuni Zake
2.Wengi Wanasingizia Kigezo Cha Umri; Wanasema Bado Ni Wadogo Hivyo Hawawezi Majukumu Ya Ndoa... Ndoa Si Jambo La Umri, Ni Suala La Kuwa Na Uelewa Tosha Juu Ya Ndoa Na Kanuni Zake, Na Mtazamo Sahihi Wa Kimawazo [Right Mindset] Unaokusaidia Kuwa Tayari Kwa Ajili Ya Kuwa Mke Mwema Au Mme Bora
3.Wengi Hawajui Namna Ya Kuwapata Wenzi Sahihi Wa Maisha Yao; Hivyo Wanafanya ANA ANADO Na SANDAKARAWE; Wanajaribu Kubahatisha Kuhusu Wenzi Wa Maisha, Halafu Baadaye Wanakumbuka Kuwa Ukishamweka Ndani Ndo Imetoka, Hivyo Wanaingiwa Na Hofu Ya KUKOSEA KUCHAGUA
4.Wengi Wanaangalia Hali Zao Za Uchumi Walizonazo Sasa [Hasa Akina Kaka] Na Kupiga Hesabu Kwamba Itakuwaje Wakiongeza Na Mke Na Majukumu Ya Familia? Kitu Cha Muhimu Si Mali Uliyonayo Sasa; Kitu Cha Muhimu Ni AKILI YA MAISHA ULIYONAYO, AMBAYO INAWEZA KUKUPA PESA; Huo Ndio MTAJI SAHIHI... Acha Hofu, Mwaminini Mungu. Kuna MILANGO INAFUNGUKA UNAPOOA..."Apataye Mke Apata Kitu Chema, Apata KIBALI [UPENDELEO] Kwa BWANA" (Mithali 18:22)
5.Akina Dada Wengi Hasa, Wanapenda SECURITY; Wanashindwa Kufanya Maamuzi Sahihi Kwa Kuangalia Hali Za Wale Vijana Wanaowafuata Kuwataka Uchumba Na Ndoa... Dada Yangu; Kila Mtu Ana BRIGHT FUTURE: Kikubwa Hakikisha Ana UPENDO WA DHATI, UPENDO WA KIMUNGU, NA PIA AWE NA AKILI ZA MAISHA... AWE NA MAWAZO YANAYOWEZA KUWA PESA NA UTAJIRI [Haya Ni Bora Kuliko Pesa, Maana Pesa Yaweza Kuisha Ila Mawazo Haya Yataleta Pesa Tena]
Kama Mkaka Hayuko Vizuri Sasa KIUCHUMI, Haimaanishi Mwisho Wake Pia Uko Hivyo. Kama Ana MTAZAMO SAHIHI KUHUSU MAISHA [RIGHT MINDSET] Huyo Anaweza Kukufurahisha Kwenye Maisha, Maana Muda Wowote Akipata Fursa Atafanya Makubwa!

Kwa Leo Niishie Hapa;

Comments