CHUMBA ZA KUTOLEA USHAURI KINAPASWA KIWEJE?

Na Mchungaji Peter Mitimingi
(The counseling environment).
COUNSELING TRAINING

1. Ni muhimu kutilia maanani mpangilio wa viti, fanicha, ni aina gani ya viti vilivyopo kwenye chumba cha ushauri. (masofa) huwa sio mazuri wakati wa ushauri.
2. Zingatia ukubwa wa chumba cha kutolea ushauri.
3. Chumba kidogo sana kinaweza kumfanya mshauriwa ajisikie vibaya hasa kwa wale ambao wamefanyiwa ukatili wa kubakwa au ukatili.
4. Pia kisiwe chumba kikubwa sana kitakacho watengenisha mshauri na mshauriwa kwa umbali.
5. Mshauri kukalia kiti cha kuzunguka hakiruhusiwi kwenye chumba cha ushauri.
6. Mshauri na mshauriwa wakae katika viti vinavyofanana yaani vya aina moja sio mshauri anakaa kwenye kiti kama bosi na mshauriwa anakaa kwenye kiti kidogo, hiyo hairuhusiwi.
7. Meza (desk) hairuhusiwi wakati wa ushauri kusiwe na meza kati ya mshauri na mshauriwa. Mshauri anapaswa kuweza kumuona mshauriwa kuanzia kichwani mpaka miguuni wakati wa ushauri sasa ukiweka meza hutaweza kumuona mshauriwa in full.
8. Chumba cha ushuuri hakipashwi kuwa na Tv au Radio iliyowashwa wakati huduma ya ushauri inaendelea.
9. wa tendo la ndoa. Hata hivyo mshauri anaweza asiwe na chumba kizuri cha kutolea ushauri kwa hiyo mteja anapaswa kukubaliana na hali inayo kuwepo.
10. Chumba cha kutolea ushauri kisiwe kimebandikwa mapicha picha ya aina yoyote kwani baadhi ya mapicha yanaweza kumfanya mshauriwa akajaa hofu zaidi au yakamkumbusha vitendo vibaya alivyowahi kufanyiwa.
Mfano:
Picha za watu wanpigwa au kunyanyaswa
Picha za vitisho
Picha za manyoka
Picha za watu wanagombana
Picha za mambo ya mapenzi
Picha za walevi au wavutaji
Picha za makahaba nk.

Comments