EAGT CITY CENTRE WAHAMIA MAKAO MAPYA MTONI MTONGANI

Sehemu ya umati wa waumini wakitembea kuelekea makao mapya, Mtoni Mtongani kwa Mgaya karibu na daraja la juu la Reli ya Tazara.


 


Ukizungumzia maombi kujibiwa, basi kanisa la EAGT City Centre wanajua nini utakuwa unaongelea, kwani siku ya Jumapili tarehe 7 ilikuwa sikukuu kwenda kwenye ufunguzi wa Hema ya Washindi lililopo Mtoni Mtongani kwa Mgaya, mahala ambapo watakuwa wanakutania baada kuwepo kwenye viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Mwalimu Nyerere, maarufu kama Sabasaba kwa muda wa miaka 5. 

 
Kwa mujibu wa Mchungaji Katunzi eneo hilo jipya lenye uwezo wa kuchukua takriban waumini 2,500 lina mpango endelevu ambao utawezesha kuchukua jumla ya waumini 7,200. Na hapo ndipo EAGT City Centre itadumu. Na baada ya kufika, hatua inayofata ni kupanuka zaidi.
 
Ufunguzi huo ulihusisha waumini kuhama na viti vyao kutoka Sabasaba hadi Mtoni eneo ambapo kanisa lipo, na kisha kufunguliwa rasmi na Mchungaji Kiongozi Florian Josephat Katunzi, na kushuhudiwa na wageni mbalimbali waliofanikiwa kufika siku hiyo. Ibada ya kwanza kanisani hapo itafanyika tarehe 14 Juni, ambapo pia tarehe 5 mwezi Julai ndipo tukio kuu la ibada ya shukurani pamoja na kuwekwa wakfu litafanyika. 
 

Taswira inavyoonekana kwa ndani 
 

Unaweza pia kuwa sehemu ya hizi baraka kwa kutoa mchango wako utakaofanikisha kufikia lengo la ujazo wa watu 7,200 ndani ya miaka mitatu, kwa kuwasiliana na kutuma mchango wako moja kwa moja na Mchungaji Florian Josephat Katunzi kupitia namba 0754367826 ama 0784367826 na pia kupitia 0718267171 
 
Credit:Gospel Kitaa

Comments