FURAHA KUGEUKA KILIO!.

Na Nickson Mabena.

Nina sababu nyingi Sana za kukwambia habari njema za Yesu Kristo,
Sababu ya Msingi zaidi ni jinsi Mwisho wa Mwenye Dhambi ulivyo Mbaya Sana.
Kili nikiufikiria Mwisho wako, jinsi ulivyo mbaya, nakuonea huruma naamua kukuandika Ujumbe wa Kukusaidia, ili uweze kurejea kwenye Mstari Wa Mungu!.
Neno la Mungu linasema hivi "Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto". UFU 20:15
Mwisho wa Wenye Dhambi woote, ni katika Ziwa liwakalo Moto na Kiberiti, Neno la Mungu linasema ndipo kutakapo kuwako Kilio na kusaga Meno!.
Furaha yote ya hapa duniani, na shangwe pamoja na kujirusha kwako vyote vitakua KILIO NA KUSAGA Meno,
Kwa nini unaufanya Moyo wako kua Mgumu ndugu yangu?, Si Umkubali tu huyu Yesu ili Akubadilishe,
Uwe kiumbe Kipya, ya kale yote yatapita, tazama yatakua Mapya!.
Unasema unakula Ujana, Utakuja Kujuta hata Utasahau kama umewahi Kula Ujana!.
Ukiwa ndani ya Yesu, utakua wa thamani, sana. Ujana wako utakua wa Maana Sana, Ubinti wako utakua Wa Thamani ndani ya Yesu!.
Vijana Wamekuchezea kwa Sababu huna Yesu, Wamekuharibia maisha yako ya sasa na ya baadae.
Rudi Msalabani upate Msamaha, urudishiwe na Amani yako.
Huko ulipo Si Salama, Mwisho wake ni JEHANAM YA MOTO.
Kwa Yesu Kuna Uzima, Amani, Furaha,
"Bali waoga, wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili." UFUNUO 21:8

KILA NIKIFIKILIA JINSI FURAHA YAKO ITAKAVYOGEUKA KUWA KILIO NA KUSAGA MENO, NAJISKIA KUKWAMBIA UJE KWA YESU, ILI JINA LAKO LIANDIKWE KWENYE KITABU CHA UZIMA!.
Geuka, Njoo kwa Yesu!.
By Mwalm Nick.
0712265856 watsap#

Comments