HIVYO VYA GIZANI VITAKUUA!

Na Nickson Mabena

"Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa." YOH 3:19-20
Nimelazimika kuandika ujumbe huu kwako msomaji, baada ya wiki iliyopita mwanamke mmoja alinitumia picha yake akiwa UCHI,
Akaniambia, alitaka nimuone tu alivyo.
Kilichonishangaza zaidi, ni kwamba mwanamke yule ni Mtumishi, tena anahuduma kubwa tu anatumika Madhabahuni.
Nikagundua ya kwamba yapo mambo yanayoendeshwa na watu gizani, yanafanyika kwa vificho.
Ndipo nikapata msukumo wa kukwambia wewe unayeendelea na Uchafu wako gizani,

Ujue tu, hivyo vya gizani vitakuua. Haupo salama hata kidogo,
Uchafu unaoendelea nao kwenye Simu yako utakuua tu!.

Unajiona upo sawa, sababu watu hawakuoni, nikupe taarifa tu, ya kwamba Mungu anakuona.
Umetoa Mimba kwa siri, umezini kwa siri, Umefanya uasherati kwa Siri,
Unatukana kwa siri.
Unawadanganya mabinti kwa Siri,
Huo uovu unaoendelea nao kwa siri Utakuua,

Ni heri Leo Ukaamua KUTUBU na Kugeuka, Acha Dhambi Mara moja,
Kimbilia kwa Yesu upate Uzima!.

Neno la Mungu linasema, watu wanapenda Giza kuliko nuru. Matendo Maovu yanakufanya umkatae Yesu ambaye ni NURU ya Ulimwengu!.
Unamchukia Yesu ili Matendo yako yasikemewe!.
Nuru imekuja kwa Ajili yako, Njoo Nuruni kwenye Uzima,
Vya Gizani vitakuua Kijana!.
SHETANI HANA KARAMA YA RAHA!.
Usomapo Ujumbe huu, Ujue Yesu amekuona na Anataka Ubadilike, Uache njia zako Mbaya,
Safisha Mapito yako.
Ipo Damu ya Yesu inayosafisha, Damu ya Yesu inayotakasa,
Mruhusu Tu Yesu aingie Ndani yako afanye Makao,
Yupo tayari kuingia anasubiri umruhusu,

Maana anasema "Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlangu, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.". UFUNUO 3:20
NJOO KWA YESU!.
By Mwalm Nick.
0712265856 Watsap#

Comments