BWANA YESU
atukuzwe ndugu yangu.
Karibu
tujifunze Neno hai la MUNGU wa mbinguni.Leo tuna ujumbe mzuri sana.
‘’Hapo
mwanzo kulikuwako NENO, naye NENO alikuwako kwa MUNGU, naye NENO alikuwa MUNGU.
Huyo MWANZO alikuwako kwa MUNGU. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye
hakikufanyika cho chote kilichofanyika.-Yohana 1:1-3.’’
-Huyo Mwanzo
alikuwepo tangu mwanzo.
-Huyo MWANZO
alikuwako kwa MUNGU na tena huyo Mwanzo ni MUNGU.
-Yeye
hakuanza maana vile tunavyodhani kwamba vilikuwepo mwanzoni kabla ya mwanadamu
kama mbinguni na nchi, huyo Mwanzo ndiye aliyeviumba hivyo.
-Anaitwa
Mwanzo kwa sababu vile vyote ambavyo mwanadamu anaviona au kuvijua basi yeye
Huyo Mwanzo ndiye aliyeviumba.
-Huwa nasema
hivi ‘’Ukitaka MUNGU awe na mwanzo kama vile ambavyo kila kitu kina mwanzo
utakosea’’. Ufahamu wa mwanadamu kuna mahali unagota au unafika mwisho. Inabidi
tu tufikie mwisho wa ufahamu wa mwanadamu maana hapo hatuwezi kupavuka maana
yanayovuka hapo ni ya MUNGU na anayajua MUNGU mwenyewe. Hatuwezi kumjua MUNGU
zaidi ya ufahamu wetu wa mwisho kama binadamu. Ndio maana MUNGU anasema Neno
hili
‘’ BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake,
wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa
sababu ya utajiri wake; bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba
ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu,
na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA,-Yeremia
9:23-24’’
-MUNGU wa
kweli amejifunua katika neno lake Biblia.
-Yeye MUNGU
anasema kama tutajisifu basi tujisifu tu
kwa sababu tunamjua yeye MUNGU pekee na pia tunajua mpango wake wa dunia hii na
pia tunajua kwamba yeye MUNGU anataka nini na hicho akitakacho yeye ndio
tukishike na kukiishi maisha yetu yote.
Hapo ndio tutajisifu.
Huyo Mwanzo
ni MUNGU maana yake hakuna chochote kabla yake maana yake maana yeye ndio huo
Mwanzo na huo mwanzo tuujuao sisi wanadamu ni wa viumbe tu alivyoviumba yeye
lakini yeye yuko tangu milele yote, hana Mwanzo wala mwisho.
Huyo Mwanzo ni
MUNGU na wala hakuanza ila alikuwepo milele yote. Kitabu cha Mika kinadokeza
kwamba Huyo Mwanzo alikuja kuishi duniani ili kuwaletea ukombozi wanadamu.
-Huyo Mwanzo hana mwisho wake wa kuishi.
Watu wengi
wa leo wamechanganyikiwa katika hili kama walivyochanganyikiwa mitume ila
wakauliza kwa BWANA YESU na kujulishwa ukweli.
Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. Filipo akamwambia, BWANA, utuonyeshe BABA, yatutosha. YESU akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona BABA; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe BABA? ‘’
Katika
Yohana 10:30 Biblia ya kingeleza inasema
hivi ‘’I
and my Father are one. ‘’
Yaani BABA wa
mbunguni na YESU KRISTO ni mmoja. Iliwachanganya Wayahudi na kwa sababu walikuwepo hapo hapo walijua
amekufuru maana amejiita MUNGU,
Yohana 10:31-33‘’ Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige.
YESU akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa BABA; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u MUNGU. ‘’
YESU akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa BABA; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u MUNGU. ‘’
Iliwasumbua
sana wayahudi lakini ukweli ndio huo na hakuna mjadala. Kumjua YESU KRISTO ndio
kumjua MUNGU wa kweli wa pekee. Wakolosai 2:2b Biblia inasema ‘’ wapate kujua
kabisa siri ya MUNGU, yaani, KRISTO;‘’ na Biblia inaendelea kusema
Ufunuo 1:8
'' Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema BWANA Mungu, aliyeko na
aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. ''
MUNGU BABA
ni alfa na Omega na pia MUNGU mwana ni alfa na omega. Unaweza pia kusoma (Ufunuo
22:12-21)
-Huyo mwanzo
ni MUNGU Mwenyezi.-Huyo Mwanzo ni Mwenyezi MUNGU, alikuweko zamani zote, yupo leo na atakuwepo milele yote.
-Wanadamu
mara nyingi tukijifunza mwanzo huwa tunaanzia pale ambapo mbinguni na dunia na
vilivyomo vilipoumbwa.
-Malaika
waliumbwa na huyo Mwanzo.-Viumbe vyote viliumbwa na huyo Mwanzo.
-Wanadamu waliumbwa na huyo Mwanzo.
Baada ya
anguko la Adamu wanadamu walianza kuishi
katika makusudi yao na sio Makusudi ya MUNGU muumbaji wao.
Kwa Neema
kuu Mwenyezi MUNGU akaja kutukomboa kwa Damu yake Mwenyewe.
-Kupitia
Huyo Mwanzo tunamjua MUNGU wa kweli.
-Mwanzo
ndiye MUNGU na Ibarahimu, Isaka na Yakobo.Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa MUNGU.‘’
Tito 2:13-14
‘’ tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU,
MUNGU mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili
yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake
mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema. '’
Mwanzo huyu
ametupa sisi ROHO wake, Tunatakiwa tumpokee MUNGU na tuanze kuishi katika
kusudi lake. Asiye na ROHO wake huyo sio wake,
Warumi 8:9 ‘’ Lakini ikiwa
ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi
hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO
wa KRISTO, huyo si wake. ‘’
-BWANA Mungu
anakupenda sana na hataki uendo jehanamu.
-Maamuzi ya
kwenda au kutokwenda jehanamu uko nayo wewe.
-Amua leo
kumpokea na utafanya vyema
Warumi
10:9-10,13 ‘’ Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini
moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana
kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata
wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. kwa
kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka. ‘’
-Ukimpokea
atakupa uzima sasa na uzima wa milele kama tu ukibaki katika pendo lake.
-MUNGU wetu
ni ngome imara, tukikimbilia leo tunakaa salama
Mithali 18:10 '' Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.
''
Kimbilia leo
ndugu ili ukae salama.
-MUNGU wetu
ni Mkuu sana-Jina lake ni Kuu sana.
-Uweza wake ni Mkuu sana.
-Matendo yake ni Makuu sana.
SIKU YA
MWISHO ATAKUJA KUMLIPA KILA MWANADAMU SAWASAWA NA MATENDO YAKE YA SASA AKIWA
DUNIANI.
Ufunuo 22:12-13 " Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
''
Ukitubu leo
yeye anakusamehe na anasema dhambi zako hatazikumbuka tena.
Kimbilia ili
uwe salama.
Yeremia 10:10-13 '' Bali BWANA ndiye MUNGU wa kweli;
Ndiye MUNGU aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi
yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.
Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu. Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu. Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.''
Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu. Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu. Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku
nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio
kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na
utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi
kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
Comments