IJUE SALA YA BWANA ILI UNAPOISEMA UWE NA UHAKIKA UNATEMBEA SAWA NA SALA HIYO


Bwana Yesu aifiwe!
Namshukuru Mungu ambaye anatupa uzima siku zote na kutuweza kuwa mahali hapa ili tuendelee kujifunza Neno lake kila siku.
Ni neno la Mungu pekee ndilo linaloyuhamisha imani hadi imani; na utukufu hadi utukufu.Na ni Neno pekee ndilo linatufanya kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo na kutuweka huru mbali na dhambi na mateso yote,,,Bwana Yesu asifiwe!!.

Na Emmanuel Kamalamo.
Somo letu linatoka kitabu cha Mathayo 6:9-13.Maandiko yanasema,,,"Bali ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Utupe leo riziki yetu.
Utusamehe makosa deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu.

[ Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu na hata milele.Amen ]
Wanafunzi wa Yesu walipowaona wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wakisali na wao wakaja kwa Yesu wakamwambie awafundishe kusali kama wanafunzi wa Yohana.
Hatuwezi kujua n sala ipi na ilikuwa inamfumo upi ndani yake wenye kuwafanya kuwa katika mapenzi ya Mungu. Lakini Yesu anawapa sala nyingine tofauti na ya wanafunzi wa Yohana, kama ingewafaa na wao angewaambia na ninyi salini kama wao, maana Yohana ni Mtumishi wa Mungu.

Fahama jambo hili, si kila "SALA" uliyopewa kanisani kwako inaweza kuwa sala ya kukusaidia kukusaidia kuyajua "MAPWNZI YA MUNGU" maana kuna baadhi ya sala ni mapenzi ya wanadamu.Najua utauliza,,,,"Emmanuel unamaanisha sala yangu haina mapenzi ya Mungu ndani yake?... Sikia nikwambie, Yesu asingewabia Wanafunzi wake,,,"NINYI SALINI HIVI" Ukitazama kauli hiyo ya Yesu utagundua ya kwamba sala ya Yohana waliokuwa wanasali haikuwa sawa na ile aliyowapa wao, maana yake "SALA YA WANAFUNZI WA YOHANA" waliyopewa na Yohana inawezekana walikuwa wanamuombea Yohana atiwe nguvu au asiingie majaribuni; Biblia haikuandika waliomba namna gani, lakini tambua haikuwa sala sahii ya kuwasaidia "KIROHO".
Sala hii ya Yesu anayowapa wanafunzi wake inawafunulia "MFUMO WA UFALME WA MBINGUNI NA JINSI YA KUTEMBEA NDANI YA UFALME HUO"
Hii sala ina upana wake kwa mtu anayepewa sala, najua tuna isema kila wakati katika nyumba zetu za Ibada.

Sasa tuangalie umuhimu wa sala hii waliyopewa wanafunzi wa Yesu na ambayo na sisi tunaitimia sala hii maana iko katika mfumo ulele wa kiufalme wa Mungu na ndiyo tunapaswa kutembea nao.
JAMBA LA I.
Unapoambiwa usali,,"BABA YETU ULIYE MBINGUNI, JINA LAKO LITUKUZWE" lazima uwe na uhakika ya unalitukuza jina hilo wakati ukiwa umefanyika "MWANA WA MUNGU" Maana huwezi ukamuita Baba wakati hajakuzaa mara ya pili.Maandiko yanasema,,,"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo a kufanyika watoto wa Mungu" (Yohana 1:12) Kwa hiyo wanafunzi wa Yesu walipewa nafasi ya kumuita Mungu awe Baba yao kwa sababu walimpokea Yesu na (WALIOKOKA) na kukubari kutembea naye.
Kwa hiyo kama hujaokoka, huna sifa ya kumuita Mungu (Baba) maana hutakuwa na uwezo wa "KULITUKUZA JINA LAKE NDANI YAKO" Katika Injili ya Luka 11:2 maandiko yanasema,,," JINA LAKO LITAKASWE" Ok, sasa angalia pamoja na mimi lile neno "JINA LAKO LITAKASWE/ JINA LAKO LITUKUZWE" maana yake Jina la Yesu alitakase "KULITENGA" na kulipa heshima ndani yako. Ni sawa na mtu aaposema Bwana Yesu asifiwe, na hajaokoka (aishi katika mapenzi Mungu) salamu hiyo haina nguvu ndani yake maana yake hakuna alichotendewa ndani yake cha kumfanya asimsifu Krsto.

Wakristo wengi wamekaririshwa sala hii, hata wakati wa kulala mtu anasema sala hii, lakini anayesema sala hiyo hana "MAHUSIANO" mwenye jina hilo hivyo sala yake inakuwa kelele mbele za Bwana.
Ili uwe na uhalali wa kusema,,,"BABA ANGU ULIYE MBINGUNI JINA LAKO LITUKUZWE" hakikisha umelitakasa (Kulittenga kuwa Takatifu) Jina hilo moyoni mwako.

JAMBO LA II.
Unaposema,,,"UFALME WAKO UJE" maana yake umeuita utawala mbinguni au mfumo wa maisha ya ufalme huo uje ndani yako na uweze kutembea ndani yake. Unaposema "UJE" maana yake unakuja na haukai hewani lazima uingie ndani yako na uhishi sawa sawa na ufalme huo, maana maandiko yanasema,,,"...Kwa mana tazama ufalme wa Mungu umo ndani yenu" (Luka 17:21)
Kwa hiyo ukisema,,"UFALME WA MUNGU NJOO NDANI YANGU" oooh! sikia nikwambia lazima tabia zako za (ULEVI WA POMBE, SIGARA, UCHAWI, WIZI, UASHERATI, UZINZI, WIVU, HASIRA, FITINA, NK) lazima viondoke ndani yako, kama hutaweza kuviacha huo Ufalme hawezi kuingia ndani yako; Maana ni "UFALME WA MWANA WA PENDO LAKE" yaani Yesu Kristo ambaye ufalme wake ni wa uzima wa milele, Yesu akiingia ndani yako lazima aingize ufalme wake.

Kama natania kawaangalie watu ambao wanasema ni "WAKRIZTO" angalia maisha yao hayana tofauti na watu wa kidunia, kwa nini? wamekataa (KUOKOKA) hivyo ufalme wa Mungu hauo ndani yao wamebaki na dini zao lakini Yesu hayumo ndani, ndiyo maaa POMBE wanakunywa, UASHERATI wanafanya nk, lakini kanisani wanakwenda na wanatoa sadaka na meza ya Bwana wanashiriki vizuri lakini hawana "UFALME WA MUNGU" ndani yao.
Kwa hiyo mpendwa angalia sala hii kwa mapana ya jicho la Rohoni uone Jinsi Yesu alivyowapa sala hii tofauti na Yohana.
Kwa hiyo ujue ukisema ufalme uje lazima ukubari ukae ndani yako na utembee sawasaw na ufalme huo....Bwana Yesuvasifiwe!

Kwa leo tuishie hapo, fuatana nami katika katiks siku ya kesho.
KAMA HUJAOKOKA OKAKA SASA NEEMA YA KUSAMEHEWA DHAMBI BADO IPO.(Ufuno 3:20)
MUNGU AWABARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments