JINSI YA KUFANYA ILI KUWEZA KUOMBA KWA MASAFA MAREFU.

Na Mtumishi Peter Lukuta.
Nimekuwa nikipata maswali mengi kwa watu yahusuyo Mambo mbali mbali lakini katika ujumuishaji wangu nikagundua katika maswali yoote %70 Yananauliza ni nini chakufanya ili kuweza kuomba kwa Muda mrefu, Sasa kutikana na hilo leo nimeona nikuletee mbinu hizo za kufanya ili kuweza kufaulu zoezi hili la kuomba kwa masafa marefu,
MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU
Kubadilisha mtazamo uliyonao kuhusu maombi, Kuna kadhia nyingi iliyojengeka mioyoni mwa wengi kuhusiana na swala la maombi ya muda mrefu, wengi wanatamani tu kuyafanya lakini wanajikuta wanashindwa kutokana na kile kilichopandwa mioyoni mwao, ipo mitazamo potofu juu ya maombi kama ifwatayo, kunawatu wanaamini kwamba kuomba kwa muda mrefu ni Neema, Ni karama, Ni nguvu ya Roho Mtakatifu, Hii mitazamo isipofutika ndani yako kamwe hutaweza kuomba kwa muda mrefu kwasababu ni mitazamo potofu ambayo haina ukweli ndani yake, siku zote huwa nawaambia watu kwamba KUWA MWOMBAJI SIYO NEEMA,, WALA KARAMA, MAOMBI NI JUHUDI ZA MTU BINAFSI kuwa muombaji ni maamuzi ya mtu binafsi, Mimi nilipokuwa mchanga kiroho nilifundishwa sana habari za maombi na nilisikia watumishi wakifundisha kwamba kuomba kwa sana ni nguvu za Roho wa Mungu na Neema Mimi niliamini hivyo na nikakaa ili kuisubiri hiyo Neema inishukie na Hiyo nguvu inishukie lakini siku zikazidi kuyoyoma na sikupata, Siku moja nikajiuliza kwamba kwanini Mimi siwezi kuomba masafa marefu kamaa mama Mchungaji wangu anayeomba masaa7 kila siuku, hii iliniumiza sana maana nilitamani kuwa kama yeye lakini kwakuwa niliamini ni karama basi nikarithika maana sina hiyo karama, lakini Siku Moja nilikaa na yule Mama nikumuuliza siri ya mafanikio yake ya kuweza kuomba kwa Muda mrefu akaniambia hivi, NIMAAMUZI NA MAZOEZI, Akaniambia hakuna Neema wala nguvu itakayokushukia na kukufanya ombe bali ni JUHUDI yako mwenyewe hiyo ndiyo itakusaidia hasa pale unapofanya mara kwa mara kwa kumaanisha na hatimaye mwili unazoea halai hiyo na kuiona kuwa ni kawaida, Nami nikajaribu kuyatafuta maandiko nikagundua kweli kuomba siyo Neea wala karama bali ni Juhudi na ndiyo maana Hata Paulo hakuomba kwa karama bali aliomba kwa Juhudi yani kile kilichomfanya Paulo awe mwombaji ni JUHUDI zake mwenyewe 1WATHESALONIKE 3:10, nahata kanisa la kwanza wote walikuwa waombaji kwasabu ya JUHUDI zao MATENDO YA MITUME 12:5.

Baada ya mimi kupata siri hii niliamua kuanza na mazoezi Unajua kila kitu ni mazoezi na baada ya kuanza mazoezi niligundua kwamba HAKUNA KAZI RAHISI KAMA KUOMBA, nilianza kuomba Na kila nilipotaka kuomba kabla nilidhamiria kwanza kwamba Nitakapopiga magoti hapa sinyanyuki mpaka nimalize masaa mawili, hivyo nikafanya hivyo kila siku nikawa napiga magoti kuomba naomba lakini kuna wakati najikuta nachooka sana na Shetani ananiambia Akilini kwamba SASA INATOSHA USIJITAABISHE MUNGU AMESHAIONA NIA YAKO, mimi nilitambua hii ni nia ya Shetani anayoileta Akilinimwangu lakini nikawa najiuliza kwamba HIVI MKULIMA ANAPOLIMA HUWA HACHOKI? jibu napata kwamba anachoka tena sana ndiyo maana utamkuta na chupa yake ya Kidumu chake cha Maji pembeni kinamsubiria analima kidogo kisha anakunywa maji lakini haachi kulima kwa kisingizio cha kucho kwasabu anajua faida atakayoipata baadae kwenye mavuno kulingana na tabu yake, Sasa baada ya kujiuliza maswali hayo niliamua sasa kuendelea na maombi hata kama ndani nasikia kuchoka Hivyo sikuacha kuomba mpaka yale masaa mawili niliyoyapanga yakatike ndipo nitahitimisha maombi hayo, Unajua mwana wa Mungu hakuna Muimbaji aliyeweza kuimba pasipokuchukua mazoezi na pia kuwa na mwalimu mzuri wa kumfundisha kuimba, Vivyo hivyo na kwenye maombi haiwezekani mtu kuweza kuomba pasipo kuchukua mazoezi na kuapata pia mwalimu Mzuri atakayemfundisha habari za Maombi, sasa niliendelea na hali hiyo Nikaazimia moyoni mwangu kwamba sasa Kila siku lazima nimalize masaa ma4 kwenye maombi ya mfululizo nikawa nafany hivyo ikaenda nikapanda mapaka masaa Saba Nikapanda Masaa Nane Nkapanda Mpaka masaa Kumi hivyo nikauzoesha mwili kwa kuutesa kila siku Hatua kwa Hatua hata ukazoea kuomba kwa masafa marefu, Hivyo kuomba kwa masafa marefu ni sawa tu na kuimba kwa muda mrefu Muimbaji haimbi kwasababu Amejawa na Roho ya kuimba no bali anaimba kwasabu anapenda na ameamua kuimba, Jnamuonaga Muimbaji jasho linamtoka sauti inakauka lakini ahaachi anajipaganoyokonde anaendelea hii yote ni kwasabu ameamua sikwamba hachoki anachoka sana likini kwasabu amedhamiria haachi kufanya na hivyo ndivyo ilivyo kwenyemaombi, sasa kuna lileandiko linalotumiwa vibaya linalosema Roho Hutusaidia kuomba, Hili andiko halimaanishi kwamba Roho anatuombesha hapana mimi niliamini hivyo na sikuona matokeo,, Maana ya Andiko hili ni kwamba Roho ndiye anayetufanya tuombe katika roho yani tuzame ndani ya Roho na kutuletea ile hali ya kuugua ndali hata kulia machozo na pia ndiye anayetupa Muongozo wa kwamba ni aingani ya maombi ya kuomba kwenye kila eneo, lakini Siyo kwamba Eti Roho anashuka na kukufanya uwe muombaji hapana kuwa muombaji ni maamuzi Ya mtu mwenyewe kwa hiari yake. Maandiko yanazungumza habari ya Nguvu kila mtu hujiingiza kwa Nguvu LUKA 16:16. bilbia haisemi kwamba kila mtu ANAINGIZWA no soma vizuri utaona inasema HUJIINGIZA yani anazitumia nguvu zake kwa mambo ya Ufalme wa Mungu sasa hapa inategemea anazitumiaje huenda anazitumia kuhubiri, Kuimba, Kufanya kazi za kanisa Au Kuomba hivyo ilikuweza kuomba kwa masafa marefu ni lazima kuzitumia nguvu zako katika kuomba yani kuzitoa nguvu zako zote hapo,
DHAMIRA YA NDANI YA MOYO IWAZE MAOMBI TU
Kila mwanadamu anakitu moyoni mwake anachokiona kuwa ni chathamani, ambacho anakiwaza kila wakati, moyo wake unakiona kuwa ni chathamani ni chamuhimu sana kuwanacho hivyo kutokana na hilo anajitahidi kufanya kila liwezekanalo ili aeze kukipata, sasa kuanzia sasahivi kifute kitu hicho moyoni na kwenye nafasi yake weka maombi, maombi ndiyo yachukue nafasi ya kitu hicho moyoni mwako, yani yaone maombi kuwa ni kitu cha muhimu kupita vyote niafadahali ukose muda wa kufanya kingine lakini upate Muda wa kuomba kwasabu Maombi yamebeba kila kila kitu ndani ya maosha ya mtu, Maombi yamebeba Afya, yamebeba Uchumi, yamebeba Kibali, yamebeba Nguvu ya Ushindi, yamebeba Wokovu maana hakuna atakayeokoka kama hakuna muombaji anayeomba ili watu waokolewe ndiyo sababu hata Yesu hakuzaliwa pasipo maombi ya Ana, Bint, Fanuel LUKA 2:36-38. Hivyo maombi ya Ana yalituletea wokovu ndiyomaana nasema ndani mwa maombi kuna wokovu, hivyo ni lazima maombi yatazamwe kwa mtazamo huo maombi yanaleta vitu bali vitu havileti maombi huwezi kuwa muombaji kwasabu unagari bali unaweza kuomba ukapata gari huo ni mfano hivyo maombi yanatangulia mbele ya vitu vyote kabla ya vitu yaanze maombi.

NGUVU YA ROHO ITAKUAKAMATIA NJIANI
Nguvu ya Roho haitangulii mbele ya mtu bali huja katikati ya safari, Siku ya kwanza aliposhuka Roho Mtakatifu hakuwakuta Mitume barabarani wanarandaranda hovyo wala hakuwakuta Kwenye viosk wanakula mishkaki na chipsi no bali aliwakuta Ghorofani wanasali kwa moyo mmoja MATENDO YA MITUME 1:14. MATENDO YA MITUME 2:1-4. Hivyo Roho aliposhuka hakuwakuta wamelala usingizi no aliwakuta wanasali kwa moyo mmoja ndipo akawajaa nndani yao wakaaza kunena kwa lugha kama Alivyowajaalia sasa hii inaonyesha ya kwamba Roho haanzi yani hamuanzi mtu bali mtu ndiyo anaanza kisha Roho anakuja njiani na kumtia nguvu za kuendelea na nguvu hiyo haifanyikazi nje ya matakwa ya mtu no bali inafanyakazi ndani ya matwa ya mtu kwa kadiri ile alivyojiachilia maana Roho halazimishi Yohana anabainisha kuwa upouwezekano wa kuotoa Roho kwa kipimo YOHANA 3:34. Hii inamaanisha kwamba Roho anapenda na anataka sana watu waombe au watumikie sana kusudi la Mungu lakini wao humtoa Roho kwa kipimo yani wanafanya kwa kipimo cha matakwa yao na siyo matakwa ya Mungu, Mimi nimezoea maombi kwa muda wa miaka 8 nimeishi maisha ya Maombi huwa maranyingi sana inanitokea ninapokuwa kwenyemaombi kuna wakati Natakakukatisha maombi niendelee na majukumu mengine lakini kila nikitaka kufanya hivyo ndani yangu nasikia Msukumo wa kuendelea kuomba sasa Huyu ni Roho anataka niendelee kuomba lakini swala la kuendelea amakutokuenelea ni lakwangu mwenyewe naweza tu kukatisha hata kama ndani bado kunamzigo na huku ndiko kumtoa Roho kwa kipimo maana hapa unakuwa umeomba kwa kipimo kile unachokitaka wewe lakini siyo kile anachokitaka Mungu hivyo hali hiyo inaponitokeaga juwa sinyamazi na siachikuomba bali naendelea mpaka hapo Ujle mzigo utakapoisha na wakati huo wakuendelea kuchoka huwa kunanijia njiani lakini siachi kuomba pamoja na hiyi hali ya kuchoka maana najua sipotezi bali nafanya kazi yenyefaida hivyo siangalii mwili bali naliangalia liletarajio la ushindi kutokana na maombi yangu, hakika niliona miujiza ya Mungu ambayo ilinifanya nipigwe vita hata kuitwa Fremason.

UDHAIFU WA MWILI NI USHINDI KWA SHETANI
Usiendekeze udhaifu wa mwili Yesu alisema roho iladhi lakini Mwili ni dhaifu MATHAYO 26:41. hapa Yesu kakukurupuka tu kulisema neno hili, bali alilisema hili kwa ile picha aliyoina mbele yake kwa wanafunzi wake, Aliisoma miyo yao akagundua kwamba Imejaa visingizio tele vya kutokuomba lakini Yesu alipovisoma visingizio hivyo ndani ya mioyoyao akajua kwamba vinatokana na kutokuujua ukweli juu ya Mwili maana wao waliwaza kwamba Yesu anaomba sana kwasabu ananeema Ana Karama, Ana Roho ya Mungu wakafikiria kwamba Ukiwa na Roho wa Mungu tu basi utaweza kuwamuombaji kama Yesu mwenyewe, Baada ya Yesu kuuona Ujinga huo na giza liliwafunga mioyo ndipo akawafumbua macho kwa Kusema ROHO IRADHI LAKINI MWILI NI DAHIFU. maana yake ni kwamba Kama niyi hamtaki kuomba kwasabu ya Mwili basi mjue kamwe hataweza kuomba milele kwasabu Mwili NIDHAIFU na bado utaendelea kuwa dhaifU, Hapa Yesu hakusema Miili Yenu ni dhaifu no bali alisema Mwili nadhaifu akiwa na maana ya kwamba hata yeye mwenyewe binafsi mwili wake ni dhaifu na hii ndiyo sababu aliomba kimkombe kimuepuke maana wmili wake uligoma kwenda msalabani kitu ambacho kiliipelekea roho kuugua kiasi cha kufa maana inajua hasara itakayotokea endapo Mwili hautasulubiwa, ndiyo maana Yesu ilimbidi akautie mwili ganzi kwa maombi ya kukesha usku kucha hatimaye mwili ukafaganzi na kukubali wkenda kusulubiwa, Hivyo Yesu aliposema ROHO IRADHI LAKINI MWILI NI DHAIFU alimaanisha kwamba KUNAVITA KATI MWILI NA ROHO vinashindana hivyo ili mtu aweze kushinda ni lazima aupuuze mwili asiusikilize kwa hiyo Hapa aliwaabanishia mitume kwamb MIMI SIMBI KWASABU YA KUJAWA NA ROHO BALI NAOMBA KWASABABU NIMEUPUUZA MWILI SIUENDEKEZI, hii ndiyo siri ya Ushindi wa Yesu kwenyemaombi sasa Yesu anataka ufute hizo sababu za kuufuata mwili maana huko ni kutafuta kufa bali Mungu anataka tuishi kwa maombi hivyo kamwe usitarajie kama Mwili utakuruhu uombe no hilo halipo kuomba ni kuamua kuomba.

USIACHE KUOMBA OMBI HILI NI MUHIMU SANA KWAKO
Ukiisha maliza toba tu maana hakuna maombi kabla ya toba kutubu na kuomba rehema NILAZIMA kabla ya yote kisha baada ya hapo Ombi lako kubwa kwa Mungu yani ombi la pili tu baada ya toba Omba Kuwa muombaji mlilie Mungu Mwambie nata kuwa muombaji Usiombe kuwa mwana maombi no Omba kuwa Muombaji maana wapo wanamaombi wasiyoomba, mwambie Mungu nimeamua kuishi maisha ya Maombi ya Sunami nisaidie Bwana, omba sana ombi hilo usiliache litakusaidia Mungu kuugeuza moyo wako na kuanza kuyaishi maombi , litakufanya kuumbika ndani yako Kiu ya kuomba Mimi sijaacha ombi hilo mpaka leo tangu nianze kuomba na nimeona matekeo makubwa. Tena unamwambia Mungu kabisa nataka kuomba masaa kadhaa Ma4 au 6 hata 10 inawezekana.=LUKA 1:37.

Ahsante kwa kunifwatilia Ahsante kwa kulike page yangu ambayo imekusudia kubadilisha maisha ya watu watoke kwenye ulokole wa Mazoea na ulegevu na kuingia kwenye UANAFUNZI halisi wa Yesu.
Pia karibu kwenye Group letu jipya kabisa kwenye Whtsapp la FUNGUO ZA UFALME Group hili ni kwaajili ya watu wapya tu Kama wewe upo kwenye yale mawili ambayo yamejaa usitume Ombi maana sitokuunganisha nataka watu wapya ambao wamekosa nafasi kwenye yale magroup ya KISIMA CHA UTAKASO na MLIMA WA UAMSHO ambayo yamejaa ndiyo sababu nikatengeneza hili la tatu la FUNGUO ZA UFALME kama wewe haupo kwenye Group zile za kwanza na ungependa nikuunge kwenye Group hili jipya Nitumie Masage Kwenye Whtsapp Yangu 0767 503054 nitakuunganisha
ZIDIKUBARIKIWA

Comments