KAFARA YA DAMU


Neno Kafara limeandikwa mara 19 na neno damu limeandikwa zaidi ya mara 350 kwenye Biblia.
“Nikauambia moyo wangu, Haya, nitakujaribu kwa njia ya furaha basi ujifurahishe kwa anasa. Na tazama, hayo nayo yakawa ubatili.”Mhubiri2:1
Katika maisha kuna watu wanaotoa kafara ya damu, inaweza kuwa ya mtu au ya mnyama yeyote yule. Kwa jina jingineinaitwa sadaka kwa mashetani/ miungu.
“Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.”1wakorintho 10:20
Mashetani wanaweza kupewa sadaka na wakapokea, duniani watu wanatoa kafara kwa ajili ya mambo fulanifulani.
Kwenye historia kuna mambo ya kafara yalifanyika.

“Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana.”Mambo ya walawi 18:21
Miungu ya moleki ni kama ya baali na ashtoresh na huyu mungu ametoka kanaani kabla ya wayahudi hawajaingia katika nchi hiyo. Wakanaani walikuwa wanatoa kafara ya watoto waokwa kuchomwa moto, mungu moleki alikuwa anakwenda kutolewa kafara na mtu anayetaka kufanyikiwa.
“Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu awaye yote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waketio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.Tena kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yo yote, hapo atoapo katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue; ndipo mimi nitamkazia uso wangu mtu huyo, na jamaa zake, nami nitamkatilia mbali, na hao wote wamwandamao katika uzinifu, ili kufanya uzinifu pamoja na Moleki, watengwe mbali na watu wao.”Walawi20:2-5
Mungu anawapa sharia wana wa Israeli ili wasifanye hivyo na mtu atakayeonekana amepokea sadaka ya amaleki au kutoa sadaka mimi sitamkubali na kumkatilia mbali.
“Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu. Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.” 1Wafalme11:7
Kemoshi alikuwa ni mungu naye na suleimani alikuwa anamtolea sadaka, wakati huo mtu alikuwa anamtoa mtoto wake kafara ili mambo yake yafanyikiwe yaende vizuri.
“Naye akainajisi Tofethi, iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti yake motoni kwa Moleki.”2wafalme23:10
(Neno Mwana linamaanisha mwanaume na binti linamaanisha wa kike)
“Nanyi mlichukua hema ya Moleki, Na nyota za mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu; Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.”Matendo 7:43
Kwenye agano jipya kulikuwa na amoleki aliyekuwa anatokewa sadaka na watu.
(Mafundisho ya Yesu kristo na Biblia kama hayafundishwi na maisha ya watu yanakuwa hayana maana yeyote kwenye maisha.)
“nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu; “Yeremia 19:5
Tunaona Mungu wa Yezabeli alikuwa anaitwa baali na wanauhusihano wa karibu.
“Nao wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwateketeza wana wao na binti zao motoni; jambo ambalo mimi sikuliagiza, wala halikuingia moyoni mwangu.”Yeremia 7:31
Mungu kwenye jambo hili halitaki sababu alimwambia Ibrahimu kwa wakati ule walikuwa wanatoa kondoo kabla ya kuja Yesu ili kufanyika ishara lakini sisi leo hatutoi kafara ya kondoo tena sababu Yesu alifanyika kafara kwaajili yetu, Mungu alimjaribu Ibrahimu kama anamtii.
“Tena naliwapa amri zisizokuwa njema, na hukumu ambazo hawakuweza kuishi kwazo;nami nikawatia unajisi kwa matoleo yao wenyewe, kwa kuwa walipitisha motoni wote waliofungua tumbo; ili kuwafanya kuwa ukiwa, wakapate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”Ezekieli: 20:25
“Akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.”Kutoka1:16
Sadaka hizi zilikuwepo tangu zamani mpaka watu wa Mungu wakajiingiza ndani yake na kuzifanya.
KWANINI WATU WANATOA KAFARA YA DAMU

“ Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana kuliko wote waliomtangulia.Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia.Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria.Ahabu akaifanya Ashera; Ahabu akazidi kumghadhibisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.” 1
wafalme16:30-34

Wakati Yezabeli anatoa sadaka za wanadamu na mambo mbali mbali akatokea iyeli mbetheli ambaye akaamua kuujenga Yeriko upya (ule ukuta ulioangushwa na wana wa Israeli na Joshua akawalaani ambao walijaribu kuujenga mji ule tena)
Joshua 6

Joshua alisema mtu akianza kuujenga mji huu atafiwa na mwanawe wa kiume, na akiendelea atafiwa tena, nchi inapotoa kafara kuna mambo ya kishetani yanawezeshwa kutendeka ndani ya nchi.
(Kwa damu ya Yesu ninazizuia kafara ya damu juu ya nchi ya Tanzania kwa jina la Yesu)
(ninaamuru mtu aliyetoa kafara ili kufanikisha jambo lake naamuru apate udhaifu kwa jina la Yesu)

Huyo mtu akaamua kumtoa kafara mwanaye ili afanyikishe msingi wa jambo alilolianza,
Akatoa na damu ikamwagika katika damu, na alipoanza kujenga ukuta akamtoa mwanawe segugu ili afanikiwe kupata damu ya kafara ili inene kuukamilisha ujenzi wake.
Kuna mtu anakwenda kanisani lakini tatizo lake haliishi kumbe kuna mahali damu imemwagwa inanena ubaki palepalena tatizo lako.
Mtu anayetaka kuliondoa kanisa hili la agano jipya hatafanikiwa kwa jina la Yesu, sisi ni wakristo wa Agano jipya tuisiokufa ‘kijingakijinga’ sababu tuna maarifa, tunaangalia udhahifu wa Petro, Yohana tunajifunza kutokana na udhahifu wao, kanisa la kwanza lilikuwa halina andiko linalosema “nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo” utukufu wa mwisho wa kanisa la mwisho utakuwa mkubwa kuliko kanisa la kwanza, hii ni saaa ya Ufufuo na Uzima Duniani ndio maana Biblia inasema
“nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui” maneo haya Petro hakuyaona yalikuwa kwenye moyo wa yakobo, na kanisa hili halitasimamishwa na Binadamu wala mtu yeyote, sisi ni kanisa litakaloona ujio wa Yesu kristo.

“Imeandikwa Nitaijaza dunia na maarifa ya utufu wangu kama vile maji yanavyoijaza Bahari” maana yake Mungu anataka kuijaza dunia kwa maarifa haya tunayojifunza.
Kuna mahali ukipagusa nchi nzima inatikisika sababu umegusa kafara yake.
KAFARA YA DAMU

Kutoa sadaka ya binadamu ilikuwa ni mila ya wamoabu na ilikuwa mtu akitoa sadaka mambo yake yanafanikiwa. Mfalme alipoona anashindwa kupigana na waisraelialimchukua mwanaye akamchoma moto na wana wa Israeli ambao walikuwa wanakaribia kufanikiwa wakapatwa na uzito wakarudi nyuma na kushindwa.
Huyu mfalme alitoa sadaka kwaajili ya wayahudi na mashetani waliingia kwenye damu ile na kuanza kupiga kelele ndipo wayahudi wakaanza kurudi nyuma.
Kwenye maisha yetu mtu unaweza ukawa unakaribia kupata kazi nzuri na kufanikiwa au unakaribia kupenya kwenye jambo fulani. Inawezekana ile bidii uliyokuwa nayo hapo mwanzo kwenye jambo fulani haipo tena na umeanza kurudi nyuma. Lakini unajishangaa unaanza kurudi nyuma kumbe kuna mtu ametoa sadaka ya kafara ya damu mahali ili usifike unapotaka kufika.
Damu ina sauti, damu inazungumza
“Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.” Mwanzo4:10

Huyu ni kaini amemuua ndugu yake habili na wako wawili na ile damu, kaini aliulizwa na Mungu akajifanya hajui chochote yeye siye mlinzi wa ndugu yake, Mungu akamwambia damu ya ndugu yako inanililia, kumbe damu inapomwwagika mahali sauti yake inasikika.
(mtu asiyekuwa na Yesu ana mganga wake wa kienyeji)
“Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako” Mwanzo4:11

Ajali inapotokea damu inamwagika chini na kwenda kwenye moyo wa nchi (kuzimu) na kumezwa huko.
“Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.” Mwanzo9:4
Damu ni uhai wa mtu, sio wote walio hai wanaweza kufanya mambo fulanifulani unaweza kumkuta mtu hasikii, hawezi kuzungumza, haoni, hawezi kusimama, ana kifafa maana yake uhai wake hauwezi kumpatia kupata mambo hayo.

“Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali.” Mambo ya Walawi 17:14
Uhai wote uko katika hiyo damu, mtu yuko hai na ananusa, anaona, anazungumza, anasema, anagusa sababu uhai uko kwenye damu ndio maana uhai wa damu ya kaini uliweza kuzungumza.
“Na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.” Waebrania12:24
Tumepata damu mbili moja inaneena mema, aokoke, afanikiwe, asafiri, awe na afya nzuri, aolewe, azae, na kuna damu nyingine inanena mabaya, afe, achanganikiwe, asiolewe, augue, apatwe ukoma, kuna damu inanena mabaya.
Damu ya mtu ina lita tano hadi nne nahii damu ya Yesu inaweza kuosha dunia nzima lakini sio ile damu yenye seli bali ni ile sauti ya damu ya Yesu ndiyo inayonena, inakwenda hadi nyikani, bungeni, inakwenda mahala popote inasema waokolewe, wafunguke, wawe huru, wapone, washinde, wawe jasiri. Wale wanaotaka kupona Damu ya Yesu inasema kwa kupigwa kwangu mmeponywa, wale wa kutokuzaa inasema hatakuwepo aliye tasa wala wa kuharibu mimba. Damu ya Yesu inasema mema kwenye ulimwengu wa roho.
Ukristo nguvu zake ni kwenye Damu ya Yesu. Watu wengine maarufu wakiwemo mabudha na wafalme na mitume walikufa na damu zao Yesu alikufa na damu yake inanena mema naukristo umejengwa kwenye damu ya Yesu, kama ukitaka kupona ni ndani ya damu ya Yesu, Taifa lililolaaniwa linakombolewa na damu ya Yesu. (amua kutamka damu ya Yesu kila siku utashangaa utakavyo ngara na kustawi).
Kuna damu inenayo mabaya inayotolewa na mtu kutokana na wivu na anaamua kwenda kwa mganga wa kienyeji mchawi ili akatoe damu, ile damu inanuiziwa inene mabaya kwamba fulani afe, asizae, asifaulu, damu haiwezi kunyamaza sababu ni uhai inazungumza na kuna ama ni ndigu yako ameamua kufanya hivyo.
“Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu. Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na ujuzi, umeketi chakulani ndani ya hekalu la sanamu, je! Dhamiri yake mtu huyo, kwa kuwa yu dhaifu, haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?” 1korintho8:9

Damu ya Yesu inanena ili uwe tajiri lakini mtu anaweza kumwaga damu ili familia fulani anayoionea wivu jinsi walivyo inazungumza wawe maskini, wasifanikiwe, na watu wengi hawana maarifa wanakuwa wanashukuri Mungu tatizo limewapata walipokuwa wameshapata fedha, wengine wanatoa Damu ili ulaaniwe ukianzia mahali fulani mpaka ukifika mahali fulani, mfano taifa linaweza kuwa limelaaniwa na ardhi imefungua kinywa chake na imepokea damu, unakuta mtu amelaaniwa alale asiulize maswali.
Unaweza kuona watu wanakufa kwa ajali kumbe kuna mtu au watu mahali wametoa kafara ili kufanikisha jambo fulani kwenye Taifa, Sisi tunanyunyiza damu ya mwanakondoo kwenye barabara zote za Tanzania kwa damu ya Yesu.

“Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama, wote walioona hasirajuu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako. Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.” Isaya41:10
Unaweza kuwa unatatizo na unaliona lakawaida mfano unachukiwa na watu, unapata vitu baadaye unapoteza, ukilala unaota ndoto mbaya, unaugua magonjwa mara kwa mara, kumbe kuna mtu nyumbani kwako ametoa kafara ya damu ili hayo yakupate, Mfano mungu moleki alikuwa anawekewa mtoto kwenye mikono yake ili ateketee kwa moto na mtoto alipokuwa akilia kwa moto uliokuwa unamchoma ile kelele yake ilikuwa inamaanisha kuimarisha tatizo lililokusudiwa litokee inaitwa kafara ya kuimarisha ngome iliyobomolewa ili iimarike.
Sisi wakristo yuliookolewa hatuna mahafali ya vita vya kiroho tunapigana mpaka dakika ya mwisho Yesu atakapokuja ndio maana Paulo alisema ‘Imani nimeilinda vita nimepigana ninaona ninanyunyizwa’.
Kafara nyingine zinatokea kwa kuchomwa moto, mfano mwizi anapochomwa ile ni kafara na anapolia kwenye ulimwengu wa Rohoni kuna mashetani wanaichukua ile sauti yake na kuimarisha ngome za kafara iliyokusudiwa.
KUIMARISHA NGOME MAANA YAKE NINI?
Ile sauti ya laana walioitengeneza hapo walipotoa kafara inapokuwa imekoma wanachukua damu na kuiimarisha ngome ya tatizo waliolijenga kwaajili yako.
Unapokuwa mwanafunzi wa Yesu ukisema kwa jina la Yesu ninainyamazisha sauti yeyote inayozungumza mabaya juu ya uso wangu, kazi yangu, ndoa yangu ninainyamazisha kwa jina la Yesu. Wakristo wengi wamefundishwa hawana mamlaka.
“Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.” Luka 10:19
“Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu“ Marko6:7
Sio lazima uwe kanisani hata ukiwa kwenye gari, bungeni, mahakamani, shuleni, unasema “kwa jina la Yesu baba mdogo, jirani, unapoona kwa mfano Bibi, rafiki au mtu yeyote unayekwenda kwa mganga wa kienyeji nakufunga kwa damu ya Yesu” hapo unaposema kule aliko anapatwa na uzito wa kwenda kwa mganga wa kienyeji na anaposhindwa kwenda uwewe unafanikiwa.
Kwenye ulimwengu wa Roho kuna mtu amenuiza kwa kafara na kila jambo linalotokea limefanikishwa na mtu mahali limefanikishwa kwenye ulimwengu wa roho uwe wa kupata na kupoteza, uwe mtu wa kuibiwa, kukataliwa, kupingwa kumbe ni kafara iliyotolewa mahali
“ Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.”
Yohana14:13

Kila mtu anamjua anayemtaabisha na kama unamjua unasema ewe shangazi sekigawa nakufunga kwa jina la Yesu uache kwenda kwa mganga wa kienyeji kutoa kafara, lazima ujifunze wewe mwenyewe kuamuru kuwanyamazisha kwa damu ya mwanakondoo, mafundisho mazuri sio yale ya kukariri sala achana nayo na ujifunze kupigana vita na kutumia mamlaka ya Damu ya mwanakondoo.
“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” Waebrani 4:12
Inawezekana mtu anayekuloga anaweza kuwa karibu na wewe na wachawi wanakuloga huku wanakusaidia ili andiko litimie adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake, yule mtu wa nyumbani anakwenda kumwaga damu anakuwa ananuizia damui mfano anapofanya biashara ife asifanikiwe, aibiwe, augue, akataliwe, asipate kazi, afeli, achukiwe na mashetani wakisikia ile damu ikinena wanaenda kuungana nayo na maneno yalionuiziwa.
Kuna watu wanakula vizuri wana maisha mazuri lakini hawana Amani wana hofu ya kifo kumbe kuna damu imenuiziwa mahali ili hayo yawatokee, mashetani yanakula damu, udi, ubani na yanakuwa yametumwa kumwendea mtu yamtie hofu, unakuta mtu anafedha sana na hawasaidii ndugu zake kumbe zile fedha zimetokea kwao, ukisema kwa jina la Yesu ninamfunga yule mjomba anayekwenda kwa mganga wa kienyeji na ukisha mfunga utaanza kuona unafanikiwa na kuna mashetani mengine yametumwa kunuizia uso ukunjamane wakati ni kijana, (kwa damu ya Yesu ninanyamazisha damu iliyonuiziwa juu yangu).
Kuna mtu mahali iwe ni serikalini, makanisani, jeshini, polisi ambaye kazi yake ni kunuizia damu ili watu wasifanikiwe. Unatakiwa ujue unamamlaka ya kunyamazisha damu yeyote iliyonuiziwa juu ya familia yako, kazi yako, biashara yako, elimu yako.
Kila anayemwamini Yesu ni mwanafunzi wa Yesu, Ufufuo na Uzima ni tofauti sio lazima ukaombewe na mchungaji unasimama mwenyewe kwa mamlaka ya jina la Yesu.
“ Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.” Yohana14:14
“ Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa” Mathayo7:7
“ Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.” Yeremia33:3
Kuna damu nyingine inamwagwa ule umahiri wako wa kutenda kazi unashuka, unakuta ofisini kuna mtu anakuona unatumwa sana na yeye anaona ukiondoka wewe yeye atapata nafasi hiyo na anaamua kwenda kwa mganga kutoa damu ili wewe unapokuwa umetumwa au kupata promosheni ufanya makosa na kuumwa kichwa au kupatwa uvivu kumbe ni ile kafara inafanya kazi.
Mungu amemuumba mwanadamu kwa mfano wake awe muumbaji mwenza sababu Mungu aliumba kwa kusema na ikawa na wewe ukiwa mfano wa Mungu unatakiwa useme nakataa kuchumbiwa na kuachwa, nakataa magonjwa, nakataa kukataliwa, nakataa kufeli, nakataa mafarakano kwenye ndoa yangu kwa damu ya Yesu.
Tumeona uhai wa kitu umo ndani ya damu, na tunaposema damu ya Yesu tunauleta uhai wa Yesu.
KWA DAMU YA YESU NINAMFUNGA MTU YEYOTE ALIYEMWAGA DAMU KWAAJILI YANGU ILI MIMI NIHARIBIKIWE NINAMFUNGA KWA DAMU YA YESU, NINA MFLYEKA KWA JINA LA YESU, NINAMPONDA KWA DAMU YA YESU.
Unamkuta mumeo akiwa nyumbani humpendi akitoka unampenda kumbe umenuiziwa ndoa ile isambaratike, kila kinachotendeka kwenye ulimwengu wa mwili kimeanzia kwenye ulimwengu wa rohoni, Rohoni pakiwa pazuri mwilini panakuwa pazuri na Rohoni pakiwa pabaya mwilini panakuwa pabaya pia.
Mahala ambapo panafanyiwa kafara ya damu panaitwa madhabahu ya damu, ya wachawi, Ni vizuri kukataa jina lako lisitajwe kwenye kikao cha wachawi unasema “ninaamuru jina langu lisitajwe tena kwenye madhabahu za wachawi kwa jina la Yesu”.Unapoomba nyamazisha laana na damu hizo zinenazo mabaya juu yako na familia yako kwa mamlaka ya jina la Yesu na damu ya Mwanakondoo Yesu kristo na kubomoa madhabahu hizo.
 

Comments