KANUNI ZA MAVUNO

Na Mchungaji Peter Mitimingi

Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.((Mathayo 9:37)
1. MAVUNO NI MENGI LAKINI SIO KILA MTU ANAWEZA KUVUNA.
2. MASHAMBA NI MENGI LAKINI SIO KILA MTU ANAYEWEZA KULIMA.
3. MAGARI NI MENGI LAKINI SIO KILA MTU ANAYEWEZA KUENDESHA.
4. MAKANISA YANA WAKRISTO WENGI, LAKINI WAVUNAJI NI WACHACHE.
5. WALOKOLE NI WENGI, LAKINII WAVUNAJI NI WACHACHE.

Mathayo 22:14
"Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache."
Jiulize swali wewe ni miongoni mwa wale wengi walioitwa au ni miongoni mwa wale wateule wachache.

Ni mapenzi ya Mungu sote tuwe wavunaji katika shamba lake.


SIFA 5 ZA MVUNAJI
Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. (2 Timotheo 2:15)

1. MVUNAJI NI LAZIMA AWE MWENYE JITIHADA BINAFSI "Jitahidikujionyesha" asisubiri kusukumwa sukumwa ndio afanye.
2. MVUNAJI LAZIMA AWE AMEPATA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU NA KWA WANADAMU PIA. (umekubaliwa na Mungu)
3. MVUNAJI HAPASWI KUWA MWENYE AIBU WALA KUSITASITA WAKATI WA KUVUNA. (mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari).
4. MVUNAJI NI LAZIMA ALITUMIE NENO LA MUNGU KWA HALALI NA KWELI. (ukitumia kwa halali neno la kweli). Asilitumie neno la Mungu kama kitega uchumi au kujipatia Umaarufu.
5. AWE NA MZIGO JUU YA MAVUNO ATAKAYO YAVUNA.
Wavunaji wengi wanamzigo wa kuvuna lakini hawana mzigo wa kutunza mavuno.Wana mipango na mikakati mingi ya kuyaendea mavuno, lakini wana mipango michache au hakuna kabisa mipango ya kutunza mavuno.
JE WEWE UNAZO SIFA HIZO ZA MVUNAJI??

Comments