KIJANA HAKIKISHA UNAZISHINDA JANGAMOTO ZA UJANA WAKO.

BWANA YESU atukuzwe ndugu zangu.
Karibu kula chakula kitamu cha kiroho.
Leo nawazungumzia vijana.
Changamoto Nyingi Za Vijana Ni Tamaa Za Ujanani Na Ngono. Changamoto Hizi Huwapata Vijana Kwa Sababu Hawampendi kujishughulisha na mambo ya MUNGU MUUMBA Wao Kwa Mioyo Yao Yote. Biblia inasema 
''Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia-Zaburi 4:4'' 
-Ni vijana wachache sana ambao watatafakari utakatifu katika vitanda vyao. wengi huwaza mabaya tu ya uzinzi, wengi hutumia muda kama huo kuangalia picha na video  za ngono kwenye simu zao.  Wengi hutumia muda huo kutumiana meseji za mapenzi na kupanga mikakati ya kukutana kesho yake kwa ajili ya uovu.

-Wangempenda MUNGU wangekuwa na hofu ya MUNGU itakayowafanya wasitende dhambi.
-Kama Vijana Wangempenda MUNGU Basi Wangetii Maagizo Yake.
-Wangetii Neno Lake Na Kwa Kumtii MUNGU Na Neno Lake Vijana Wasingeteswa Na Tamaa Chafu Za Ujanani. 
-Kwa Kumtii MUNGU Vijana Wasingekumbwa Na Utoaji Mimba Baada Ya Kutenda Dhambi. 
-Kwa Kumtii MUNGU Vijana Wasingekumbwa Na Kujiua Au Kujidhuru Kwa Sababu Ya Kuachwa Na Wazinzi Wenzao. 
-Kwa Kumtii MUNGU Hakika Vijana Wasingefeli Masomo Kwa Sababu Ya Kutawaliwa Na Mahusiano Ambayo Ni Pando La Shetani Maishani Mwao. 
Biblia Iko Wazi Kabisa Kwamba Ili Kijana Aishi Maisha Mazuri Ni Lazima Amtii MUNGU Huku Akilifuata Neno La MUNGU.
Zaburi 119:9 '' Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. ''

 -Kijana Nakuomba Umtii BWANA Kupitia Neno Lake, Kuna Vijana Hadi Wamekufa Mapema Kwa Sababu Tu Walikosa Utii Kwa MUNGU. 
-Ndugu Nakuomba Acha Dhambi, Ogopa Dhambi, Ikimbie Dhambi Na Usifanye Dhambi. 
-Ukikubali Na Kumtii BWANA YESU Utakula Mema Ya Nchi. Tumia Ujana Wako Kwa YESU.
BWANA anasema 
 '' Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; -Isaya 1:16-19 '' 
-Ukikubali na kutubu na kumtii BWANA hata leo uatakubaliwa na MUNGU.

          VITU VITATU(3) HATARI KWA KIJANA.

       1.   KIBURI. 

-Kiburi kimewashusha wengi sana.
-Kiburi Ni Kuwadharau Wengine. 
-Kiburi Kimeua Huduma Nyingi. 
-Kiburi Ni Mwanzo Wa Maangamizo Yote
Mithali 29:23 '' Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. ''. 
-Kama Una Roho Ya Kiburi Kijana Mwenzangu Hutafika Popote. -Kiburi Ni Chanzo Cha Migomo. 
-Ukiwa Na Kiburi Maana Yake Wewe Ni Adui Wa MUNGU
1 Petr 5:5 '' Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. ''. 
-Kinyume Cha Utii Ni Kiburi . 
-Mtu Mwenye Kiburi  hafai kabisa na   
-Kiburi Ni Hatari Kwa Vijana.
 Kuna Kijana Akijiona Tu ana Ndevu anabadilika Na Hakuna Jinsi Unaweza Kumsaidia Ili asiishie Pabaya. Kuna Vijana Kuwa Na Sauti Nzito Utii Wote Unaondoka. Kuna Vijana Kuota Kidogo Matiti Wanajiona Ni Wakubwa Na Wanajiona Hawahitaji Msaada Wa Mtu Yeyote. 
Ndugu Zangu Kiburi Ni Kibaya. Mtii MUNGU Na Watii Wazazi Wako Wa Kimwili Na Wazazi Wa Kiroho. ''Ningejua'' Huja Baada Ya Kupata Majanga. Na Kama Majuto Ni Mjukuu Basi Kiburi Ni Mzazi. Yaani Ndiye Anayeweza Kumzaa Majuto. '
 Tumia Ujana Wako Kwa YESU.

             2.    PESA.

Pesa  Pia Inaweza Kuwa Jambo Hatari Kwa Kijana. 
Kuwa Na Pesa Sio Dhambi Ila Tabia Ya Kupenda Pesa Ni Mbaya

Waebrania 13:5 '' Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. ''. 

-Ukiwa Na Tabia Ya Kupenda Pesa Huwezi Kuona Ibada Ni Muhimu Kuliko Biashara Yako. 
-Ukiipenda Pesa Lazima Tu Ikupeleke Pabaya. 
-Ukiipenda Pesa Huwezi Kutoa Fungu La Kumi. 
-Ukiipenda Pesa Lazima Pesa Itakupelekea Uwe Msaliti

Waamuzi 16:4-5 '' Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila.  Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja. '' 
-Huyu Delila alimsaliti Samsoni kwa yeye kupenda pesa.
-Pesa Isikutawale Maana Ikikutawala Itakupeleka Pabaya
Mathayo 26:14-16 '' Wakati huo mmoja wa wale Thenashara, jina lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani, akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha. Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi apate kumsaliti. ''.

-Kumbuka Kwamba Kanuni Ya Kupokea Ni Kutoa, Wote Tunahitaji Pesa Lakini Hatuwezi Kufanya Machukizo Ili Tupate Pesa. 
-Hatutakiwi Tuitii Pesa Bali Pesa Ndio Itutii Sisi.
- Anayeitii Pesa Anaweza Hata Kudanganywa Na Waganga Wa Kienyeji Kisha Kuua Wazazi Wake Ili Apate Pesa Kumbe Ndio Kujiangamiza Mwenyewe. 
Biblia Inasema Tusiwe Na Tabia Ya Kupenda Maana Yake Pesa Isitutawale Hata Uhusiano Wetu Na BWANA MUNGU Ukaharibika Kwa Sababu Ya Pesa.
- Kuna Watu Kwenye Mawazo Na Akili Zao Wamejaza Pesa Kuliko Neno La MUNGU Na Hawana Muda Wa Neno Hata Dk 2 Lakini Ajabu Hata Hiyo Pesa Hawana

  3 UASHERATI.

Moja Ya Mambo Ambayo Hayatakiwi Kwa Kijana Basi Ni Uasherati. 
-Uasherati Umeleta Madhara Makubwa Kwa Vijana. 
Biblia Inakataza Uzinifu

Kutoka 20:14 ''Usizini.   ''. 

-Kama Vijana Wamekuwa Watii Kwa MUNGU Wangeitwa Heri. -Leo Huduma Nyingi Zinakufa Kwa Sababu Ya Uzinifu. 
- Uasherati Leo Umezaa Hadi Uuaji Na Kutoa Mimba

2 Samweli 13:10-17 '' Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu.
 Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa. Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza. Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake. ''.


 Leo Kuna Wazazi Wanahaha Kwa Sababu Ya Mimba Za Utotoni Za Vijana Wao. 
-Kuna Wamama Wakongwe Leo Wanalea Watoto Wachanga waliokimbiwa Na wazazi wao vijana Kwa Sababu Ya Kutokutii Neno La MUNGU Kwa Mabinti Hao.
- Tungemtii MUNGU Tungefanya Vyema Sana Vijana Wote

Mathayo 5:27-28 '' Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. ''. 

Uasherati Haufai Hata Kidogo. 
- Uasherati Una Madhara Makubwa. 
-Uasherati Unaweza Hata Kukupeleka Motoni. 
-Uasherati Unaweza Kuleta Mahangaiko Kwa Wazazi Wako. -Uasherati Unaweza Kukuletea Ukimwi.
- Uasherati Unaweza Kusababisha Baadae Usiweze Kuolewa Au Kuoa Kaa Sababu Kila Mtu Akisimuliwa Kuhusu Wewe na kukimbia. 
-Kuna Familia Leo Unakuta Bibi Analea Wajukuu Hata 7 Huku Wazazi Wa Watoto Hao Wameshafariki Kwa Ukimwi Huku Wakiwa Vijana.
Vijana wenzangu leo nawaonya ili mwanze kumcha MUNGU katika ukweli wake.
Mhubiri 12:1 '' Mkumbuke MUUMBA wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.'' 
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana
. Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili. MUNGU Akubariki.

N.B. (Kwa wale wanaobadilisha masomo yangu sehemu za mwisho na kujiandika wao na kuweka namba zao za simu na kuomba pesa za kukuza huduma zao kupitia ujumbe wangu,hiyo ni mbaya. share somo, weka katika blog yako ila usibadilishe chochote na pia fundisha watu kupitia ujumbe huu, print na usambaze kokote kwa njia yeyote maana hapo utakuwa unahubiri injili. mmepewa bure toeni bure. binafsi sijawahi kuandika masomo ili nipate pesa hata kama nina uhitaji wa pesa. ubarikiwe)

Comments