KILA MMOJA AJUE KUUWEZA MWILI WAKE KATIKA UTAKATIFU NA HESHIMA.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Kwa furaha sana nakukaribisha tujifunze Neno la MUNGU la uzima.
1 Thesalonike 4:4-5 ''kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;  si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua MUNGU.'' 
-Kuuweza mwili?
 Ndio ni kuuweza mwili katika utakatifu na heshima.
Mwili umewashinda wengi kuuendesha katika utakatifu na heshima. Lakini agizo la Biblia kwa watakatifu wa KRISTO ni lazima au ni sheria kuuweza mwili katika utakatifu na heshima.
Siku moja nikiwa Zanzibar tulikuuwa na Mchungaji wangu tukishuhudia nyumba kwa nyumba, tulifika nyumba moja karibu na Kisauni na kuwakuta watu, tukaanza kuwashuhudia habari njema za ufalme wa MUNGU. Tulieleza madhara ya dhambi lakini dada mmoja akasema semeni yote ila uzinzi haiwezekani kuacha,  nikamkazia macho na kumwambia hilo ndilo la kwanza kuacha kama ukiamua. Yule dada alisema '' wewe ni kijana mdogo tu je wewe huwa hufanyi uzinzi? maana unaonekana hujaoa'' nikamwambia kwamba tangu niokoke 2008 sikuwahi kufanya uasherati. yule dada akacheka sana na jibu hilo hakuliamini, mchungaji akasema tuondoke, tukaondoka. Nikajifunza kwamba maelfu ya watu ufahamu wao umepotoshwa na sasa wanaamini kuna dhambi hawawezi kuacha kumbe ni hila tu za shetani kuwashawishi kwamba hawawezi kuacha ili wasipopata neema ya kumpokea YESU na kutubu basi waende motoni. ndugu yangu kama una ufahamu kama wa huyo dada kwamba hawezi kuacha ngono nakuomba badili mtazamo huo wa kishetani na amua kuokoka na kaa mbali na vishawishi wa uzinzi. ni lazima uuweze mwili wako katika utakatifu na heshima.
Kama umeokoka na kufanyika mteule wa MUNGU hakikisha unakaa mbali na dhambi ikiwemo dhambi ya uzinzi. jitambue na amua maana kuna nguvu kubwa katika maamuzi mazuri.

1 Kor  6:15-20 ''  Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya KRISTO? Basi nivitwae viungo vya KRISTO na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na BWANA ni roho moja naye. Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la ROHO MTAKATIFU aliye ndani yenu, mliyepewa na MUNGU? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni MUNGU katika miili yenu.''
-Sio wote walioshindwa kuuweza mwili wana mapepo. Bali kuna wengine wameshindwa kuuweza mwili katika utakatifu kwa sababu tu hawajamua kumpendeza MUNGU.
-Wengine wameshindwa kuuweza mwili kwa sababu  tu hawautaki uzima wa milele maana kama wangeuhitaji kweli uzima wa milele basi wangempokea YESU na kuomba kusaidiwa kwa wachungaji  mbinu za kushinda tamaa ya mwili.
- Kuna ambao wameshindwa kuiweza miili yao kwa sababu tu ufahamu wao hawajaamua  kulipokea Neno la MUNGU na kulitii.

 Warumi 8:8 ''Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza MUNGU.''

Mafundisho ya kukemea uzinzi na uasherati ni mengi sana na mara nyingi sana umefundishwa kanisani lakini mbona hujalitii neno la MUNGU?
Mafundisho ya kukemea uzinifu ni mengi sana makanisani lakini watu wameshupaza shingo zao ambazo zinakaribia kuvunjika. maana ukishupaza shingo mwisho wake ni kuvunjika.
-Dhambi ya muda mfupi imewaponza maelfu ya watu.
-Vichocheo vya dhambi hii ni vingi sana na kila siku wachungaji makanisani wanaonya juu ya wateule kujiingiza katika mitego ya dhambi hii.
-Mwili umekuwa tatizo kwa walio wengi.
-Watu wengi wameshindwa kuuweka mwili katika utakatifu autakao MUNGU.
-Mwili unawatesa wengi sio katika uzinzi tu bali hata mavazi.

1 Kor 6:13 ''  Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini MUNGU atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa BWANA, naye BWANA ni kwa mwili '' 

-Binti yuko tayari kutembea matiti nje ili tu kumfurahisha shetani.
-Kijana yuko tayari kutii mwili kwa kuwa shoga ili tu kumtukuza shetani.
-Mwanamke yuko tayari kutembea nusu uchu ili tu dunia ya wazinzi ijue kwamba na yeye yupo.
-Watu wako tayari kuvaa mawigi  ya kila aina ili tu kuonyesha kwamba MUNGU alikosea kuwaumbia nywele fupi. U nani wewe unayemkosoa muumba wako?

Isaya 45:9 '' Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono?''

-ndugu Nakusihi tu kwamba uweze mwili wako katika utakatifu na heshima. Kama kuna nguo huwezi kuzivaa mbele ya baba mkwe au mama mkwe wako kwanini unazivaa mbele za watu wengine wenye utu na heshima kama ya hao unaowaogopa?
Kipi bora kumwogopa baba mkwe au kumwogopa MUNGU?
Watu waliowengi huvaa vizuri na kiheshima mbele za wakwe zao tu au mbele ya baba zao tu ambao labda wawe wakali.

Wagalatia 5:19-21 ''Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU.''
-Mwili wako hakikisha unauendesha katika utakatifu na heshima.
-Kama wewe ni mtumishi wa MUNGU  mhubiri au mwimbaji au yeyote hakikisha huvai nguo zisizo na maadili maana kweli itatukana kwa ajili yako.
-Kama una tabia mbaya ewe mtumishi wa MUNGU  hakikisha unatubu leo na kugeuka na kuanza kumbariki MUNGU maana ukiendelea na tabia mbaya basi Wokovu utatukanwa kwa watu wa mataifa jambo ambalo ni baya sana.

Matendo 20:28 '' Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo ROHO MTAKATIFU amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments