KWA NINI UNATAKIWA KUOKOKA SASA!?.

Na Nickson Mabena.

"Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia; Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA; TAZAMA SIKU YA WOKOVU NDIYO SASA". 2KOR 6:2
Yesu alikuja Duniani katika Mwili, kwa lengo la kumtafuta Mwanadam aliyepotea,
Na Alipoondoka Akawaachia Watumishi wake Kazi ya kuihubiri Injili, na ndio Maana Leo nimekuandikia Ujumbe huu!
Watumishi wa Kweli wa Mungu tunapokuhubiria habari za Yesu tunakua tunakua tunakutakia Mema sana, na ni Upendo wa Mungu tu ndio unaotusukuma kufanya hivyo!.
Kitu cha Kwanza unachotakiwa kukifanya, mara tu usikiapo Neno la Mungu ni kuliamini, Kisha kufanya Maamuzi ya Kumfuata Yesu, tangu saa hiyo ulipoliamini Neno la Mungu!.
Ndugu msomaji, Biblia inasema Saa ya Wokovu ni Sasa. Usijipe Moyo kwamba, utaokoka ukishaoa au Kuolewa.
Wengine husema Wataokoka wakisha kuwa Wazee!. Unaona Sasa hivi Ukiokoka, utakosa kufaidi Utamu wa Dunia!
Nikwambie tu, Kwa Yesu ni Kutamu kuliko utamu wowote wa Dunia hii,
Ndugu unayesoma Ujumbe Huu, SAA YA WOKOVU NI SASA. AMUA SASA...
Saa ya Wokovu ni Sasa kwa Sababu kuu Mbili!.
1. Hujui Siku wala Saa ya Kurudi Yesu!
Yesu anakuja Kuchukua Watakatifu tu, waliooshwa kwa Damu yake. Na Atakuja bila taarifa, ni Ghafla tu, yaani kufumba na kufumbua.

Ndipo Neno la Mungu linasema, "Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu". MATH 24:42
2.Hujui siku wala Saa ya Kifo Chako.
Mwanadamu, Sikia neno la Bwana, Tubu leo, maana hujui siku ya Kufa Kwako!.
Na Baada ya Kifo ni Hukumu (Ebr 9:27). Hakuna Sala yoyote ya Kumshawishi Mungu akubadilishie mahali pa kukuweka ukisha kufa!.

Mahali pa Kwenda unapachagua ukiwa hai, na sio baada ya Kufa!.
Usidanganyike, hata Dunia Nzima tukiomba kwamba Uwekwe Mahala Pema Peponi, kama Uliukataa Wokovu wa Yesu Kristo basi wewe ni Wa Motoni tu!.

NJOO KWA YESU SASA, AMUA SASA, UNATAKIWA KUOKOKA SASA.
MUNGU AMEKUPA NAFASI YA KUISHI MARA MOJA, BAADA YA KIFO HUKUMU!.

Kwa Nini Unamkataa Yesu hadi Leo!?,
Kwa nini Ukomae na Uovu hadi Leo!?.

WOKOVU ni wa Kwako Binafsi, Usimuangalie Baba, Mama wala Ndugu au rafiki yeyote anayekushawishi ukatae Kuokoka, Yeye wala hana Mbingu ya kukupeleka!.
Yesu pekee, ndiye mwenye Mbingu ya Kukupeleka!!.
Acha Dhambi, Kataa dhambi, Ikimbie Dhambi...
NJOO KWA YESU!.
By Mwalm Nick
0712265856 watsap#

Comments