KWANINI NI LAZIMA KUULINDA MOYO KULIKO YOTE UYALINDAYO?

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tena katika siku nyingine tule na kushiba Neno la MUNGU. 

Kwanini Ni Lazima Kuulinda Moyo? 
Mithali 4:23 ''Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.''

-Ni Kwa Sababu Tabia Ya Mtu Hutoka Moyoni Na Sio Rohoni. 
-Ndugu Yangu, Ulinde Woyo Kuliko Yote Ulindayo. 
-Moyo Ndio Uliobeba Maamuzi Yako. Ukipenda Mabaya Hiyo Ni Kwa Hasara Yako Na Ukipenda Mema Hiyo Ni Kwa Faida Yako. -Ishi Maisha Ya Wokovu Maana Ndio Mpango Wa MUNGU.
- Ufanye Moyo Wako Umtii KRISTO Na Neno Lake. 
-Hakikisha Moyo Wako Hauingiliwi Na Kuipenda Dunia 
-Hakikisha Moyo Wako Hauvamiwi Na Wapangaji(Mapepo). 
-Mtii BWANA Mwenye Uzima Wako Wa Milele Kuliko Kuwatii Wanadamu. 
-Tii Biblia Siku Zote.
Mathayo 5:8 ''Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona MUNGU. ''

=Sababu 8 Zinazotufanya Tuulinde Moyo Kuliko Vyote Tulindavyo Ni Hizi. 

1.    Moyo Unalindwa Ili Usitoe Mabaya.
Mathayo 15:19 '' Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano; ''. 

2.    Kwa Moyo Mtu Humwamini YESU Hata Kupata Uzima.
Warumi 10:10 '' Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.   ''

3.    Moyo Ni Shamba La Kupandwa Neno La MUNGU.
Mathayo 13:15 '' Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. ''
 
  4.    Moyo Hutoa Chemchemi Za Uzima.
Mithali 4:23 ''Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.''

5.    Moyoni Mwa Mtu Hukaa KRISTO.
Waefeso 3:17 '' KRISTO akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;   ''

6.    Moyo Ni Makao Ya ROHO MTAKATIFU.
2 Kor 1:22 ''  naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.''

7.    Moyoni Ni Mahali Pa Amani Ya MUNGU.
Wakolosai 3:15 ''  Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. ''

 8.    Moyo Ni Mahali Pa Upendo Wa MUNGU.
Warumi 5:5 ''na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.   ''

 Biblia Inasema Tuulinde Moyo Kuliko Vyote Tulindavyo(Mithali 4:23). 

Kwa Jinsi Gani Utaulinda Moyo Wako? 

=Moyo Wako Utaulinda Kwa Kuzingatia Haya Mambo 8. 

 1.   Ili Uulinde Moyo Wako Weka Neno La MUNGU Kwa Wingi Moyoni Mwako.
Zaburi 119:11 '' Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. ''

2.    Ili Uulinde Moyo Wako Epuka Vikundi Vibaya.
1 Kor 15:33 '' Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. ''
  -Tena Biblia Takatifu inaendelea kusisitiza kwamba 
''Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.  Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. -Zaburi 1:1-3''

3.     Ili Uulinde Moyo Wako Usifikiri Mambo Ya Mwilini.
Warumi 8:8 '' Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.''

4.     Ili Uulinde Moyo Wako Hakikisha Unasahau Mabaya Yaliyopita.
Isaya 43:18 '' Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.   ''

5.    Ili Uulinde Moyo Wako Hakikisha Unaridhika Na Ulichonacho.
Mithali 15:16 ''Kuwa na mali chache pamoja na kumcha Bwana; Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.   ''

6.    Ili Uulinde Moyo Wako Jitahidi Kuomba Mara Kwa Mara.

1 Wathesalonike 5:17 ''Ombeni bila kukoma;''

7.     Ili Uulinde Moyo Hakikisha Unamtafuta BWANA Kila Wakati.
Zaburi 34:4 ''Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.   ''

8.    Ili Uulinde Moyo Wako Usikubali Kutawaliwa Na Mawazo Mabaya.
Zakaria 8:17 ''wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA.   ''

 MUNGU Wangu Na Akubariki. Mtii KRISTO Na Hakikisha Unajazwa ROHO MTAKATIFU Na Anza Kuenenda Kwa ROHO.
- Ikatae Dhambi, Iogope Dhambi, Ikimbie Dhambi Na Usifanye Dhambi. 
-BWANA YESU Yu Karibu. 
-Shika Wokovu Asije Mtu Akakunyang'anya. 
-Hata Kama Utadharaulika Lakini Mtii BWANA YESU Na Usimwache Hata Kidogo.
Kumb 6:5 '' Nawe mpende BWANA, MUNGU wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. ''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana
. Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili. MUNGU Akubariki.

Comments