MAFUNDISHO YA KWANZA!

Na Mtumishi Nickson Mabena

Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu, napenda kukukaribisha kujifunza somo hili, ili tupate ufahamu na uelewa Mzuri Juu ya Neno la Mungu!.
"Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu" 1Petro 2:2
Somo langu leo, ni Mafundisho ya Kwanza, nataka nizungumzia jinsi mafundisho ya kwanza yanavyoweza kumfanya Mtu akawa na Ufahamu Mzuri kuhusu Mungu, au anavyoweza akawa na Ufahamu mbovu kuhusu Mungu.
Biblia Imetuagiza, ili tuukulie Wokovu, lazima tupate MAZIWA YASIYOGHOSHIWA, hayo maziwa ndio Mafundisho ya Kwanza!.
Kwa kuwa yapo Mafundisho yasiyoghoshiwa, basi naweza nikasema yapo Mafundisho yaliyoghoshiwa!.
Leo hii kumezuka ubishani na malumbano baina ya Dini na Dini, au Dhehebu na Dhehebu, Kundi flani na Kundi lingine, au Watu na Watu, yote husababishwa na Tofauti ya Mafundisho ya Kwanza Waliyoyapata watu hao!.
Mfano, Mtu amefundishwa Kwamba Pombe sio Dhambi, na akapewa na Maandiko ya kusimamia, lakini Mwingine amefundishwa Pombe ni Dhambi na Amepewa na Maandiko ya Kusimamia. Watu hawa, wanaweza wakawa na nia njema ya Kumfikia Mungu, lakini kinachowatofautisha, na hata wakati Mwingine kubishana kabisa, sababu inayowafanya wawe hivyo, ni Mafundisho ya Kwanza Waliyoyapata!.
Mwingine, amefundishwa Yesu ni Mungu, mwingine ameambiwa Yesu si Mungu, Mafundisho ya Kwanza yanawatofautisha hawa watu!.
Wengine, Kwenye Mafundisho ya Kwanza ameambiwa Kuna Kuokoka Duniani, mwingine ameambiwa hakuna Wokovu duniani. Mafundisho ya Kwanza yamewatofautisha watu hao.
Na Mifano mingine mingi, ambayo wewe unaijua!.
Lengo langu ni hili, Nataka Ujue kwamba Si Kila Mafundisho ya Kwanza ni ya Kweli, upo hivyo ulivyo ni Kwa sababu ya Mafundisho ya Kwanza uliyoyapata.
Mtu yeyote unayetumika kuwafundisha Watoto, Tafadhali Usiwafundishe Watoto uongo. Wafundishe Kweli ya Neno la Mungu,
Ukiendelea kuwafundisha Uongo, Jua kwamba Unatuandalia Kizazi Potofu, kisicholijua Neno la Mungu, Kizazi kisichojua Nguvu za Mungu!.

Unatutengenezea Kizazi kinachoendelea na uovu, huku kikilingia mafundisho ya kwanza waliyoyapata!
Mafundisho ya Kwanza yamewapoteza wengi sana, wengi walikua Mbali kabisa na Mungu, lakini wakadhani wapo salama, hadi Pale Neema ya Mungu ilipoingilia Kati, ndipo walipojua kwamba wamepotea!.
Pengine na wewe Umepotea, lakini kutokana na Mafundisho uliyopewa, unajiona Upo salama..
Mafundisho ya Kwanza yanakutia moyo, kisa aliyekufundisha ulimwamini sana, kutokana na Cheo alichonacho!.
Hata unakataa Mpango wa Mungu kwenye maisha yako, hutaki kukemewa uovu wako, kutokana na Elimu ya Awali uliyopewa na watu!.
Geuka Sasa uyakubali mafundisho yenye Uzima, ambayo Roho Mtakatifu ameyaweka kwa Watumishi wake!.
MAFUNDISHO YA KWANZA, YANAWEZA KUKUFANYA UKAWA MBALI SANA NA MUNGU,AU UKAWA NA MAHUSIANO MAZURI NA MUNGU!.
Wewe upo wapi!??, Ni Maombi yangu kwa Mungu, Roho Mtakatifu akusaidie, uyapambanue Mafundisho uliyoyapata, ili ujue kwamba ni ya Mungu, au.....!!.
MWALIMU UNAYEFUNDISHA NENO, FUNDISHA NENO LISILOGHOSHIWA, FUNDISHA KWELI YOTE!.
Mungu akubariki kwa kuusoma Ujumbe huu!.
By Mwalm Nick
0712265856 Watsap#

Comments