MALI ZA KICHAWI

Na Askofu mkuu Josephat Gwajima, ufufuo na uzima.

“Sineni ili kuwaamuru, bali kwa bidii ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu. Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. 2 WAKORINTHO 8:9~10
Yesu ni Mungu alitoka mbinguni akavaa mwili wa binadamu akaja duniani akazaliwa kwenye familia ya kimasikini japo alikuwa tajiri ili sisi tuwe matajiri. kama sisi hatuwezi kuwa matajiri basi kifo cha Yesu kilikuwa cha bure lakini tunatakiwa tujue kwamba Yesu alifanyika kuwa masikini ili sisi tuwe matajiri.
Heshima ya mtu inaendana na utajiri wake.
“Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote. Basi sasa, Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako tukufu.” 1 MAMBO YA NYAKATI 29:12~13

Umasikini humletea mtu dharau na kutokuthaminiwa.
MITHALI 3:16~18
“Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto. Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani. Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye.”

Duniani kuna watu wengi wenye utajiri ambao sio wa uhakika na haudumu lakini utajiri wa Mungu unadumu kuliko utajiri wa wasiomcha Mungu.
“Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu. Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.” MITHALI 4:18~19
Mungu ametupatia msingi wa Utajiri na agano la Utajiri kutoka kwa Ibrahimu.
“Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu. Akaendelea kusafiri kutoka kusini mpaka Betheli, mahali pale palipokuwapo hema yake kwanza kati ya Betheli na Ai; napo ndipo palipokuwa na madhabahu aliyofanya hapo kwanza; naye Abramu akaliitia jina la Bwana hapo. Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng'ombe na kondoo, na hema. Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja.” MWANZO 13:2~6
Leo tunasema Mungu wa Ibrahimu kwasababu Ibrahim ni Baba yetu wa Imani na pia sisi ni warithi wa Baraka zake utajiri wake.
“Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, Bwana akambariki. Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana. Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu.” MWANZO 26:12~14
Utajiri wa Ibrahimu ulirithikwa kuanzia kwa watoto wake mpaka vizazi vilivyofuata. “Baraka inaleta ukuu sana na kustawi sana”. Isaka alikuwa na mradi wa kilimo na hapa tunajifunza kwamba tukitaka kupata Baraka za Ibrahimu ili kutajirika na kuwa na heshima na ukuu ni lazima mtu uwe na kitu cha kufanya ili kupitia hicho kitu Mungu akubariki kwa Baraka za Baba Ibrahimu.
“1 Basi Yakobo akasikia maneno ya wana wa Labani, wakisema, Yakobo amechukua mali yote ya baba yetu; na kwa mali ya baba yetu amepata fahari hii yote. 9 Hivi Mungu akamnyang'anya mali yake baba yenu, na kunipa mimi. 16 Maana mali yote ambayo Mungu amemnyang'anya baba yetu, mali hiyo ndiyo yetu na ya wana wetu. Basi yo yote Mungu aliyokuambia, uyafanye.” MWANZO 31:16
Yakobo naye alikuwa tajiri kupitia kwa tajiri asiye mcha Bwana. Esau alitengana na Yakobo ili kuepusha kuchanganya mali zake na Yakobo kwasababu walikuwa na mali nyingi sana.
“Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng'ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye.” MWANZO 36:6
“Wamisionari walipokuja Afrika miaka kadhaa iliyopita lengo lao lilikuwa kutuletea nuru ya injili ili tujiendeleze wenyewe Kusoma Biblia na kufanikiwa. Tupo hai kusudi tumtumikie Bwana na tumiliki mali ili tukirudi mbinguni tufurahie kazi tulizozifanya hapa duniani.”
Wana wa Israeli waliondoka mistri na mali nyingi na hawakuacha hata kwato sababu Mungu wamisri waliingiwa na hofu kuu ya kuuawa kwa wazaliwa wao wa kwanza kwenye kila familia. Biblia inasema wayahudi waliondokaa kwa maringo na mali za wamisri.
“Injili ya Yesu kristo ianze kugusa kila mtanzania mojamoja kwa jina la Yesu”
Ukiri”
“Nimenunuliwa ili nimiliki, nitiishe na nitawale kwa damu ya Yesu kristo”
“Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia.” MITHALI 8:17~19

Alimfanya mtu kwa mfano wake ili atawale.
“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu” MWANZO 1:26~29
KWENYE B IBLIA KUNA INJILI YA WOKOVU NA INJILI YA UFALME
maana ya Injili ya wokovu ni kwamba tumesamehewa dhambi, tunaishi maisha matakatifu, tunahubiriwa hatakama huna hela mbinguni hakuna hela, hatakama huna chakula mbinguni hakuna chakula, hata kama unataabu mbinguni kuna raha. Injili hii ya wokovu inauwezo wa kumgeuza mtu mbaya mwovu kitabia awe mtu mzuri na mcha Mungu, inamfanya mtu abadilike tabia zake na kuwa mtu mzuri Injili ya Wokovu inahubiriwa kwa watu wengi kwa mfano:- “Toka kwa shetani uje kwa Yesu, usiibe, usiseme uongo, tenda mambo mema uende mbinguni n.k. Watu wengi wanafahamu na wamehubiriwa sana injili hii ya wokovu

Lakini hii haitoshi kubakia kwenye Injili ya Wokovu pekee tunatakiwa kama wana wa Ufalme wa Mungu tuhamie kwenye injili ya ufalme injili ambayo ilitabiriwa kuwepo nyakati hizi za mwisho. Injili ya ufalme itahubiriwa kila mahali na kwenye injili ya Ufalme tawala na falme za dunia zinageuka ziwe falme za Mwanakondoo, Sisi ni mabalozi wa Yesu kristo na tunayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu.
Yesu kristo alikuja duniani kutengeneza ufalme na sisi ni mabalozi wa ufalme huo hapa duniani. shetani ni mungu wa dunia hii na amepofusha watu fikra za watu wengi kiasi kwamba wanaamini mtu wa Mungu anatakiwa awe masikini asiye na mali na ukuu ili wamtawale kwa mali zao, watu wamejaza fikra zao kwamba mtu wa Mungu akiwa na Utajiri huyo sio mtu wa Mungu. Wanaamini hivyo kwasababu wanafahamu siri ya utajiri na wanaelewa mtu wa Mungu akiwa tajiri na mkuu watashindwa
kumpelekesha na kumwamulia cha kufanya kwa utajiri na ukuu wake alio nao ndiomaana wana mpinga na kutaka kumnyanganya hata kile alicho nacho. Pamoja na hayo yote zile nyakati alizozitabiri Yesu zimewadia kwamba watu wa Mungu wawe wakuu na matajiri na kuwa na nguvu ili injili ya Ufalme ihubiriwe duniani kote kwa mamlaka ya Jina la Yesu kristo.
“Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.” ZABURI 82:6

“Kizazi jeuri na kinahitaji kuhani jeuri na zamani kulikuwa na wahubiri waliokuwa wanalia mpaka watu wanageuka na kutubu kwa Mungu lakini leo hii ukianza kulia unawekwa kwene idara ya watu wanyonge wasioweza kuongoza “watu wanaolialia”, Akaja mhubiri aliyekuwa anavua nguo na kuwakemea watu mpaka watu wanatubu na kubadilika nia zao lakini leo hii ukivua nguo na kuwaambia watu wageuze nia zao wanakuona umechanganyikiwa na wanaweza kukupeleka kwenye hospitali ya vichaa. Kizazi hiki jeuri kinahitaji mhubiri/kuhani jeuri asiyekwepesha maneno yake asiyeangalia mtu na cheo chake mhubiri anayeshusha milima na kujaza mabonde kwa uwezo wa Mwanakondoo Yesu kristo.”
MITHALI 22:7
“Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.”
Wenye dhambi na waovu wanamiliki uchumi halafu watu wa Mungu wanabaki hawana kitu kwa kupofushwa akili zao wasimiliki. Mungu ni Baba yetu na aliumba dunia na kutuumba sisi kwa mfano wake na tunaliamini jina lake na asili yetu ni kutawala kila kilichopo baharini (gesi, mafuta…), angani (sayari zote) na kila kiendacho juu ya nchi (wanyama, madini ardhi…).

Unatakiwa utafsiri vitu kwa namna ambayo haikuangamizi, mtazamo ndio unaokuangamiza unatakiwa ubadili mtazamo wako.
Tangu zamani wafalme walipokuwa wanateka nchi walikuwa wanachukua mali, watu wenye akili na watu wa muhimu na kuwaacha masikini na watu walio wanyonge.

“Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, Nebukadreza a, mfalme wa Babeli, alikwenda Yerusalemu akauhusuru. Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake. DANIEL 1:1~2
“Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi. Akamchukua Yekonia mpaka Babeli; na mama yake mfalme, na wake zake mfalme, na maakida wake, na wakuu wa nchi, aliwachukua mateka toka Yerusalemu mpaka Babeli. Na mashujaa wote, watu elfu saba, na mafundi na wafua chuma elfu moja, wote pia wenye nguvu, tayari kwa vita, hao wote mfalme wa Babeli aliwachukua mateka mpaka Babeli. WAFALME 24:14~16
“Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji; wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi; tena wanatangaza habari ya desturi zisizokuwa halali kwetu kuzipokea wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi. Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora. Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.” MATENDO YA MITUME 16:16~25
kuna aina za pepo ambao wanakaa ndani ya watu kwa lengo la kuwatajirisha watu wa mji mfano wafanya biashara, mawakili, wabungu, mawaziri, majaji(makadhi) na watu wengine lakini wakikemewa na kutolewa ndani ya mtu husika, mji wote utataharuki na faida za waliokuwa wanamtegemea zinapotea kabisa kwasababu ameguswa aliyekuwa anawapa hizo faida na utajiri.
Matajiri wa efeso walipomwendea Yule binti mwenye mashetani yenye uwezo wa kuona mambo yajayo, kuwatabiria na kuwapa maelekezo ili wafanikiwe wakakuta Yule binti hana kitu tena ametolewa na Paulo. Cha kushangaza mahakama ilikubali kuwaaibisha na kuwafunga akina Paulo kwenye chumba cha ndani cha gereza kwa kosa la kutoa mapepo yaliyokuwa yanawatajirisha watu wakubwa wa mji wa efeso na wafanyabiashara.
Kosa walilolifanya kina Paulo lilikuwa ni kuharibu mzunguko wa fedha wa kishetani. Mungu alikuwa anafahamu mzunguko huo wa kishetani na alikuwa na mpango wa kutawala mji wa efeso na kuzizungusha fedha za mji ule kupitia kanisa. Kwenye miji mikubwa yupo anayemiliki fedha zake na ukifanikiwa kumpiga Yule unauteka na kuugeuza kuwa ufalme wa mwanakondoo na jambo hili ni jepesi machoni pa Bwana
Ulipowadia Usiku wa manane watu wote walipokuwa kimya hakuna msaada msingi wa gereza ukatikisika, milango ya gereza funguka na Paulo akatoka gerezani na walewale waliomweka gerezani wakaokoka na kumpokea Yesu na mji wote ukaokoka na fedha za mji zikaingia kwenye ufalme wa Mungu . Bila shaka matajiri na viongozi na wote wa mji ule waliokoka na kanisa la wafilipi lilianza na ule mzunguko wa fedha ya kishetani ukatokomezwa ndiomaana Paulo kwenye neno lake anasema
“Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu.” WAFILIPI 4:15
Hii inamaanisha ukimpiga anayeshikilia mzunguko wa fedha za mji kwa namna ya kishetani, mzunguko huo utahamia kanisani na kumilikiwa na Mungu kwaajili ya ufalme wake.
MATENDO YA MITUME 13:6~11
“Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake BarYesu; mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.”

Kisiwa cha patho badi kipo mpaka leo na kipindi kile utawaala duniani ulikuwa wa warumi, kulikuwa na Gavana aliyekuwa na msaidizi wake mchawi, Gavana huyo alisikia injili ya Paulo akihubiri akaamua kumwalika nyumbani kwake amhubirie lakini Yule msaidizi wake alikuwa na uwezo wa kumfanya gavana aseme ndio au hapana kwenye kumpokea Yesu Kristo. Paulo alipofika alimhubiria Gavana huku Yule mchawi akiwa anamvuvia moyo wa kutokukubali kuamini na kuokoka lakini Paulo alimwona na kumtia upofu asione.
Uchawi unaweza kuwamiliki watawala wakafanya maamuzi yasiyo na maana. Kuna watu ambao maamuzi yao yanafuatana na Wachawi nyuma yake. Unapoomba ni vizuri kuwaombea na wale waliokuzunguka sababu wanaweza kulogwa wasikusaidie kukupigisha hatua.
“Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake.” AYUBU 20:15~16
Fedha ipo lakini imememzwa na shetani lakini Mungu anasema atayatapika na atayatoa tumboni mwake.
Mungu aliruhusu hayo yute yatokee kwa Yesu ili sisi tujifunze. Mungu alitaka tujifunze kutokana na mfano huu kwamba duniani kuna mali ambazo zinapatikana kwa njia ya kishetani. Utajiri huu hapa duniani tulipewa na Mungu pale alipo tuumba sababu alitupa uwezo wa kumiliki na shetani alikuja kuichukua ile mali na kutoka kwa Adam akaimiliki na kwasababu hiyo Mungu alimtuma mwanaye wa pekee Yesu kuja ili kuturishia ile mali iliyofichwa mahali pa siri na kuigeuza dunia kuwa ufalme wa Mwanakondoo.

“Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.” YOEL 2:25
“Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.” ISAYA 42:22
“Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.” LUKA 4:3~8
Kumbe shetani anaweza kuwapa watu utajiri na sisi tuliookolewa kama Wana wa Ufalme wa Mbinguni hatutakiwi kumwendea shetani bali tutumie mamlaka aliyopa Yesu Kristo ili tumnyanganye na kumtapisha mali zetu na tumiliki sawa na makusudi ya Mungu hapa duniani kwa jina la Yesu. Hazina yetu ipo na lazima tumyanganye kwa jina la Yesu.
Yona alimezwa na samaki akiwa anaelekea tarshishi samaki alipommeza akageuka akaenda kumtapikia ninawi na akawahubiri watu wa ninawi watubu Mungu atawahukumu ndani ya muda wa siku arobaini ndipo waninawi wakafunga na kuomba na ni mahala pekee kwenye Biblia ambapo watu na mifugo walifunga kwa muda wa siku tatu na Bwana akawasamehe wakaishi.
“Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu; nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema Bwana wa majeshi. Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi. Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi.” HAGAI 2:6~9
Maombi”
“Baba Mungu kwa mamlaka ya Jina la Yesu kristo ninazufuata mali zangu zilizofichwa mahali pa siri ninamtapisha aliyeimeza kwa jina la Yesu, kila aliyeshikilia utajiri wangu, ubunifu wangu, biashara yangu, mzunguko wa fedha yangu ninamfyeka kwa jina la Yesu imeandikwa “sikuja duniani kuleta amani bali upanga” ninatumia upanga wa Yesu kristo kuwafyeka mashetani wote, wachawi wote, waganga wa kienyeji wote kwa damu ya Yesu, ninamiliki juu ya nchi utajiri, hazina na mali zote kwa jina la Yesu imeandikwa “ ninaitapisha hazina iliyopo angani, baharini na nchi kavu kwa jina la Yesu, ninamiliki utajiru heshima, nguvu na utukufu kwa mamlaka ya Yesu kristo kwa damu ya Yesu Amen.

Comments