MAOMBI YA KUMWITA MUNGU ILI AITIKE KWA KUKUPA USHINDI.

Na Mtumishi Peter Mabula.
MAOMBI YA KUMWITA MUNGU ILI AITIKE KWA KUKUPA USHINDI.

Ninakushukuru JEHOVAH BWANA katika jina la YESU KRISTO kwa maana fadhili zako ni za milele. Ninakushukuru maana unasikia maombi yangu na unasema katika Neno lako kwamba ''Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu. - Zaburi 55:17'' hakika muda wowote nikuitapo BWANA unataitika na kunishindia katika jina la YESU KRISTO
Tazama pia BWANA umeahidi katika Neno lako kwamba '' Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. - Yeremia 33:3 ''. Wewe MUNGU BABA hujipingi na neno lako ndio maana nina ujasiri mkuu kukuita ili uitike katika maisha yangu maana umeahidi kuitika Neno lako kwamba tukikuita tukiwa watakatifu na tunaoamini katika wewe MUNGU wa miungu, tunapokea. BWANA YESU nakuita katika familia yangu ili uitike kwa kuleta uzima, itika BWANA katika ndoa yangu kwa kuleta furaha na upendo, amani na maelewano. itika MUNGU wangu katika masomo yangu, nipe akili nzuri na fungua ufahamu wangu ili nielewe. itika BWANA katika ufahamu wangu ili nilijue kusudi lako katika maisha yangu. Itika BWANA YESU katika ukoo wangu, itika kwa kuondoa mizimu na kila laana ya ukoo, itika BWANA kwa kuondoa kila aina ya mkosi na balaa katika maisha yangu. wewe MUNGU ni Mwaminifu sana na ahadi yako ni ndio siku zote. BWANA itika katika kanisa letu kwa kuleta uamsho na moyo wa toba kwa kila mtu, itika BWANA katika kazi yangu kwa kuleta faida na upendeleo. itika BWANA katika kiroho changu kwa kunipa mafunuo na agizo la kufanya. itika BWANA katika utoaji wangu, natamani niwe nakutolea kile kinachokubariki MUNGU wa uzima. itika BWANA kama nine lako nisemalo kwamba tukikuita MUNGU wetu utaitika. MUNGU BABA nakusihi mfalme uitikie katika kile nilichooomba mtumishi wako maana ahadi yako ni ndio na kweli siku zote. BWANA nikumbuke na unijibu sawasawa na Neno lako. Asante MUNGU BABA maana katika wewe nimeomba na kupokea , asante BWANA YESU maana kupitia jina lako nimeomba na kupokea. nakuinua MUNGU wa mbinguni maana umejibu maombi yangu na sasa naenda kuona katika ulimwengu wa mwili juu ya kile nilichoita kwako kupitia maombi yangu. MUNGU uliyemsikia Nabii Yona akiwa ndani ya tumbo la nyangumi nakuomba BWANA nami nisikie na kunijibu maombi yangu nikiwa katika tumbo la matatizo na magonjwa. asante BWANA maana nimeomba kwa imani na ninaamini napokea sasa.  naziamini kazi zako MUNGU wetu na hakika najua umejibu BWANA. katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea .

Amen amen.



KAMA ULIPEWA VAZI LA KIPEPO OMBA MAOMBI HAYA KUFUTA BALAA ZILIZOKUSUDIWA KWAKO.


Kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ewe vazi la kushindwa, leo ninakukataa kwa Jina la YESU KRISTO. Ninakataa vazi la kichawi, vazi walilonipa wazazi, vazi litokalo kuzimu nalikataa kwa Damu ya Mwanakondoo. Vazi la kunifanya nionewe, mavazi ya urithi na ya uganga wa kienyeji nayakataa kwa Jina la YESU KRISTO. Leo nayakataa mavazi niliyovishwa ili niwe malkia wa kuzimu, nakataa mavazi yenu kwa Damu ya Mwanakondoo. Nakataa vazi la umaskini, vazi la magonjwa nililovishwa,Nakaa kwa Jina la YESU KRISTO. Vazi la bibi nalipiga. Nazivua nguo za rohoni walizonivisha wachawi nyakati za usiku, nayakataa mavazi yao yote ya kipepo kwa Jina la YESU KRISTO. Ninakataa mavazi ya wafu. Nalivua vazi lenu. Vazi la kukataliwa nalivua kwa Jina la YESU KRISTO. Vazi la ukoo la kushindwa nalivua kwa Damu ya Mwanakondoo. Achia maisha yangu ewe vazi la kuzimu kwa Jina la YESU.

Nalikataaa vazi lolote nililovishwa kwenye msiba nililopewa wakati wa msiba. Leo nalikataa kwa Jina la YESU KRISTO.kila vazi linalohusiana na wafu, leo nalivua kwa Jina la YESU KRISTO.
Nalivaa vazi la neema ya BWANA, nalivaa vazi la hashima, vazi la upendeleo, vazi la kuonekana, vazi la kupata kazi, vazi la utajiri, vazi la kusifiwa na kuinuliwa katika Jina la YESU KRISTO .
. Amen

Comments