Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini
Tanzania,Flora Mbasha mwisho wa wiki hii amefanikiwa kufanya uzinduzi wa
album yake mpya kabisa na pia kuzindua Bendi ya muziki ambayo ataanza
kufanya nayo huduma za kimuziki wa injili kuanzia sasa.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo alikua
ni mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh.Freeman
Aiakel Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Same mkoani Kilimanjaro.
Uzinduzi huo uliambatana na burudani ya
nyimbo za injili kutoka kwa wanamuziki mbalimbali ambao waliambatana na
Flora mbasha katika kuiweka wakfu DVD yake mpya pamoja na Bendi,Miongoni
mwa wanamuziki walihudhuria uzinduzi huo ni pamoja na Ambwene
Mwasongwe, Upendo Nkonne, Joseph Nyuki, Christopher Mwahangila,
Christina Matai, Neema Gasper, na Furaha Isaya.
Video na Picha za Uzinduzi huo ni kama
zinavyoonekana hapa chini kama zilivyopigwa na Uncle Jimmy ambaye
alikuwepo eneo la tukio
 |
Mh.Freeman Mbowe akizungumza jambo wakati akizundua Album hiyo |
 |
Mwanamuziki Flora Mbasha akiwa VIP Hall kabla ya kuingia Ukumbini |
 |
Back Vocal au waimbaji wa bendi hiyo ya Flora Mbasha wakijiweka sawa kabla ya kuingia ukumbini |
 |
Mwanamuziki Ambele Mwasongwe akiperfom katika Uzinduzi huo |
 |
Mh,Freeman Mbowe |
 |
Mh.Freeman Mbowe akiwa na ujumbe wake wakiingia Ukumbini huku ulinzi ukiwa umeimarishwa |
 |
Mh,Freeman Mbowe akiwa na ujumbe wake ndani wakiwa meza kuu kama mgeni Rasmi katika uzinduzi huo |
 |
Mh,Freeman Mbowe akiizindua DVD album yake Flora Mbasha |
 |
Mwanamuziki Upendo Nkonne |
 |
mwanamuziki Flora Mbasha |
Comments